IFM kufanya mdahalo wa Fao la Kujitoa

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumanne, Novemba 20, 2012 06:59 Na Oliver Oswald, Dar es Salaam

CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kinatarajia kufanya mdahalo mkubwa Desemba 7, mwaka huu, kuhusu Fao la Kujitoa kwa wafanyakazi nchini. Hatu hiyo ni moja ya kutambua changamoto mbalimbali zinazolikabili Taifa kwa kuchambua mada mbalimbali zinazohusu jamii.

Akizungumza na MTANZANIA, Dar es Salaam jana, Mhadhiri Msaidizi wa Sheria za Biashara chuoni hapo, Agustus Fungo, alisema mdahalo huo utajikita kujadili masuala mbalimbali.

Fungo alisema mdahalo huo utaangazia Sera ya Hifadhi ya Jamii, sheria za mfuko, nadharia ya hifadhi ya jamii na hali halisi ya maisha ya Watanzania kwa sasa.

Fungo alisema mdahalo huo unatarajiwa kuongozwa na Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC,) Camillus Kassala.

Alisema mada nyingine zitakazojadiliwa ni pamoja na ulipaji wa kodi katika sekta ya madini, iwapo Serikali inanufaika.

“Mdahalo huu ni mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 40 ya chuo hiki na pia utahusisha shule mbalimbali za sekondari zilizopo hapa jijini.

“Lakini pia tunataka kujua ukweli kuhusu Fao la Kujitoa iwapo linakubalika duniani na taratibu zake zipo vipi, hivyo tunaamini kupitia mdahalo huu tunaweza kupata majibu,” alisema.

Fungo alisema kwamba pamoja na hayo, lakini pia mdahalo huo ni moja ya njia ya kuujulisha umma kupitia wanafunzi kuhusu msingi wa jambo hilo.

“IFM ikiwa kama moja ya taasisi za elimu hapa nchini, imeona ni vema kutumia fursa hii kufikisha ujumbe kwa jamii kupitia midahalo tunayoiandaa kwa kuwashirikisha wanafunzi,” alisema.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Makubwaaa. Visket, vitait na kata k wataweza kuchangia hoja kweli?
 
sasa hawa jamaa wanajadili kitu gani
wakati maamuzi yameshatolewa na serikali
alafu huyo mzee dr camilius kassala bado yupo? anamawazo primitive sijui atachangia mawazo gani?
 
Wanataka kuonekana na wao wamo. Ningewaona wajanja kama wangejadili fedha zilizofichwa USWIZI
 
Hiyo topic ya fao la kujitoa ishafungwa maana watu wanachukua chao, kama wao ni wajanja wajadili hela ya Uswisi basi
 
Makubwaaa. Visket, vitait na kata k wataweza kuchangia hoja kweli?

umeona mavazi tu??au ndo akili zako zinafikiri hivo?
naona umesahau kuwa wao wavaa vimini,kata k ndo hao wanaokuhudumia wewe
kuanzia bank,bima,pension fund kibao wamejaa wanahakikisha kuwa wewe unawekewa akiba yako ya baadae
kwa taarifa yako ifm shule ngumu sana na vichwa wapo tele na ukimuona mtu kagraduate hapo jua kafanya kazi ya ziada
siyo chuo chenu nlichokizoea kusoma na nyani darasani
 
msamehe bure huyu ndugu
hajui ugumu wa shule ya ifm
 
umeona mavazi tu??au ndo akili zako zinafikiri hivo?
naona umesahau kuwa wao wavaa vimini,kata k ndo hao wanaokuhudumia wewe
kuanzia bank,bima,pension fund kibao wamejaa wanahakikisha kuwa wewe unawekewa akiba yako ya baadae
kwa taarifa yako ifm shule ngumu sana na vichwa wapo tele na ukimuona mtu kagraduate hapo jua kafanya kazi ya ziada
siyo chuo chenu nlichokizoea kusoma na nyani darasani

Poleee, na futa povu!
 
katika suala kuwepo faoujitoa ni haki ya mwanachama,pawe na fursa na maamuzi yanayotegemea uamuz wa mwanachama mmwenyewe.iwapio halitawekwa sawa hili,waathilika wakubwa watakuwa waajiriwa kwenye sekta binafsi ambako ajira sio za uhakika.mfano kuna makampuni ktk biashara ya mazao kama kahawa,korosho,pamba n.k huwa hadumu sana ni miaka mitano au chini ya hapo,hivi nao wasubilie umri kustaafu ili kuchukua mafao yake?,umri wa kuishi tz ni mfupi wengi hawafikii huo umri.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom