Ifikie wakati Nchi za Africa tujitoe kushiriki Kombe la dunia

Huu unazi ndo unaharibu soka la africa..ukiangalia hizi mechi mbili ivory cost hawajacheza kitimu ..hawapeani pasi..viungo walikuwa wanapoteza mpira maeneo ya hatari mara kibao..tunakuja kulaumu penalt ya wazi kabisa..

Haikuwa na sababu ya kumkaba mtu kivile afu tena kwa nyuma hapo hata mie ningejiangusha
 
Watu bwana....nyinyi ndiyo mnaoua mpira wetu wa Tanzania yaani mashabiki wa kufuata upepo, mtu unashabikia kitu wala hujuwi unashabikia kwa nini. Kiutaalam ile ni penalty na wala haina ubishi hata wachezaji wenyewe wa Ivory Coast walijuwa hivyo na hawakubisha ila wewe mchezaji wa benchi lisilo tambulika duniani ndiyo unayejua zaidi, si ndiyo? Kama kweli uliangalia ile mechi na si kusimuliwa kwenye daladala si uliona jinsi kina Drogba walivyoshika vichwa baada ya Samaras kukwanguliwa ndani ya 18 au haukuona hii? Watu bwana. Wale walifanya vile kwani walishajuwa nini kitatokea...Kama nilivyosema, Ivory Coast had their chances ila walishindwa kuzitumia, utasema na hii pia walilaliwa na refa? Acha ubishi wa kijinga mkuu. Ule mpira ulikuwa 50/50.

Tatizo Ivory Cost hawakutaka kushinda ile mechi, walitaka watoke draw tu hata kocha alitaka hivyo ndio maana akaanzisha Drogba badala ya Bony Bony alilia sababu alijitahidi akafunga ila wajinga wa timu yake wakajisababishia penalt
 
Kazimoto alishasema before match kuwa ivory coast ime rob nafasi ya Tanzania. Mwaka huu wanhekuwa kina Mrisho Ngassa pale.

Kumbe cha mtu hakiendi bure eeeh

Kweli malipo ni hapahapa duniani....Nilikuwa uwanja wa taifa ile siku Ivory Coast wanacheza na Taifa Stars siku ile yule refa MuArgeria aliipendelea sana Kodivwaa na kuing'ata Stars,leo wamelipwa.Mnakumbuka Mwainyi Kazimoto alisemaje siku chache zilizopita?

Ila sisi nao tungemaliza mpira zamani leo hii tungejiwekea historia
 
Tanzania ikifungwa hamlalamiki hivi,kina drogba wametolewa mnalia lia hapa.

mlisikia sweden walilia pale spain walipokula mkono?

Timu zilizotoka africa ziliwakilisha nchi zao tu na sio africa ndo maana hawakuja kuomba mchango wala bendera ya TZ.

Duh we jamaa umekuwa mkali sana, mimi huwa nashabikia timu inayoonesha uhai, Tanzania ingekuwepo na isingeonesha uhai nisingejisumbua kutaka presha
 
Nimefurahi sana walivyotoka. Napenda ghana nao wapigwe,algeria nao wapigwe wasepe kwao.

Na next wc africa ipeleke timu 2 tu.

Una roho ngumu zaidi ya jiwe.
Ila Algeria walijitahidi wamepaswa endelea hawa watu weusi wengine watoke tu
 
Nimeangalia michezo hii na hususani huu mchezo ulioisha hivi punde kati ya Greece na Ivory Cost na hiki kilichofanyika ambacho kimejionyesha wazi kwa kugawa Penalt kwa mtu kuchimba chini yeye mwenyewe pasipo kuguswa kimenihudhunisha sana na pia tulejee matukio ya nyuma
1. 1990 - Cameroon na Argentina waafrica tulinyanyaswa kwa yasiyovumilika kwani kadi 2 nyekundu zilitolewa kimagumashi huku unyanyasaji wa wazi ukifanyika kutoka kwa Referee
2. 2010 - South Africa - Ghana na Uruguai Suelez alidaka mpira ambao tayari ulikuwa gori lakini cha kushangaza Refa akatoa Penalt na kusababisha Gyan kukosa na kusababisha vifo kadhaa nchi mbalimbali ikiwemo na ghana yenyewe.
3. Pia mechi ya jana ya Brazil na Cameron tumeshuhudia gori la tatu likifungwa kwa ofside ya wazi kabisa.

Ni vema CAF wakajitafakari juu ya hiki kinachotokea na ili kutusaidia waafrica nafuu tungeacha kushiriki hayo mashindano yao tukajiendeshea wenyewe mashindano yetu.
kweli kk
 
soka halifi;
sheria gani zinazopindishwa na refa; LAMPARD alipokataliwa goli lake Waingereza walilalamika hadi sasa imewekwa GOAL-LINE TEC.

wewe unaridhika na hoja za mzungu? jitambue wewe..
Ntakuja na uzi wa timu za ulaya.. Maana africa kamu uiongereza tunaacha kutatua matatizo ya msingi ya soka letu tunaangalia visingizio ambavyo havipo..kama uingireza walisingizia goli lla lampard wakalazimisha goal technology..lakini kukataliwa goli la lampard haikuwa ndo tatizo lao la msingi, maana hata world cup hii wamechemsha
 
Drogba hakuwa na sababu ya kuanza ile mechi, alikuwa mzigo wangeanzishwa wale madogo kina Bony
Kalou mchoyo sana alitaka afunge yeye ili apewe sifa
Ndo nachosema mkuu, uliona drogba alivyo kuwa mzito, hii ya kupanga kwa kuangalia majina ili wacost nigeria sana kipindi flani wakaja kuacha unaona sasa wanacheza kitimu na wanafanikiwa
 
Haikuwa na sababu ya kumkaba mtu kivile afu tena kwa nyuma hapo hata mie ningejiangusha
Watu hapa wanabisha tu lakini ile ni penalt kabisa.. Kwenye kumina nane mtu anaangalia goli hata ukimtegea kwa mbali sana ni tuta labda refaasione
 
Tatizo Ivory Cost hawakutaka kushinda ile mechi, walitaka watoke draw tu hata kocha alitaka hivyo ndio maana akaanzisha Drogba badala ya Bony Bony alilia sababu alijitahidi akafunga ila wajinga wa timu yake wakajisababishia penalt


Ok....let us assume kuwa ni kweli uyasemayo. Sasa hawa wanaolia humu JF kuwa Ivory Coast walionewa, walikuwa wanaangali mechi gani tofauti na wewe na mimi ile juzi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom