Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,023
- 18,566
Maneno mengi sana yanasemwa nchini kuwa mara nyingi Rais Magufuli anavunja katiba ya Jamhuri ya Tanzania kwa makusudi. Nakiri kuwa hata mimi kuna wakati nilishazungumzia hilo.
Baadae nilijiuliza ikiwa mimi ningekuwa ndio Magufuli, nikijua ninaweza kuvunja katiba kimakusudi na hakuna utaratibu wa mimi kuchukuliwa hatua yeyote, na pia sheria za nchi haziko kwa namna ya kufanya iwe rahisi kuchukuliwa hatua nikivunja katiba, je ningevunja katiba kimakusudi? Je, kiongozi wa upinzani angekuwa raisi angefanya hivyo?
Sasa suala la msingi ni kwamba, kwa nini Rais anavunja katiba? Lazima anakuwa na sababu - na najua sababu yake ni kwamba anafanya kitu ambacho anaona kina manufaa kwa Watanzania na Tanzania - yaani the end justifies the means. Nikatambua kwamba hiyo ndio mentality ya Magufuli, kwamba yeye akiona anataka kufanya jambo ambalo lina manufaa kwa nchi, basi yuko tayari kuvunja katiba ili kulifanya kwa manufaa ya nchi. Amefanya hivi katika mambo mengi sana.
Lakini sasa ni sahihi kikatiba? Hapo ndipo nilijiuliza sana. Nikagundua kwamba nchi yetu inatoa fursa, bila kutamka wazi, ya raisi kuvunja katiba kwa sasa. Suala la raisi kuvunja au kutovunja katiba limefanywa kuwa utashi wa raisi katika mazingira ya katiba na sheria zetu. Sasa sio kila raisi tutakaekuwa nae hapa Tanzania atakuwa na mentality au utashi wa aina ya Nyerere. Nyerere aliheshimu sana Katiba, alikuwa akitembea nayo mfukoni na kuisoma kila wakati japo alijua katiba ilimruhusu kuivunja.
Lakini ikumbukwe kuwa, mazingira ya katiba yetu kuvunjwa huenda ni jambo lilifanywa kwa makusudi kabisa kwamba tuwe na katiba inayotoa mazingira ya raisi kuivunja bila kuchukuliwa hatua katika mazingira fulani fulani ambayo anaona inafaa kuvunja katiba. Yaani kwa kifupi, tuna katiba ambayo inaruhusu raisi kuivunja kwa manufaa ya taifa, kwa hiyo raisi kuvunja katiba ni suala la kikatiba! Katiba yetu inampa raisi utashi wa kuivunja au kutoivunja. Ni sawa na mtu kuambiwa usiendeshe gari eneo hili zaidi ya 50km/hr, lakini hata ukiendesha zaidi ya 50km/hr, hutapewa adhabu. Sasa hapo ina maana kutoendesha zaidi ya 50km/hr ni suala la utashi, kama una sababu nzuri ya kuendesha zaidi ya 50km/hr ni wazi utafanya hivyo!
Kwa hiyo ifikie wakati tukubali tu, kwamba mazingira yaliyopo yanatoa fursa kwa mtu yeyote akiwa Rais wa Tanzania, (sio Magufuli pekee) kuvunja Katiba kwa makusudi na kusiwe na namna ya kudhibiti hilo. Ifikie mahali badala ya kupiga kelele juu ya Rais Magufuli kufanya hivyo basi tutafakari jinsi gani tunaweza kufanya hilo lisitokee huko mbele. Na pia kusema tunahitaji katiba mpya haitoshi, maana ni kelele tumeshaisikia sana. Suala sasa linapaswa kuwa ni nini cha kufanya ili tuwe na katiba mpya.