Ifike muda na Sisi wana CCM tuache Unafiki na tukemee hii tabia ya Polisi kila mara Kuzuia Mikutano ya Wapinzani

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
Hapana hata kidogo Mimi ni mwana CCM na wala sioni Aibu kujiweka hivi wazi ila nimevumilia huu Upuuzi na sasa nasema wazi kabisa sipendezwi na hii tabia ya kila mara Wapinzani wakitaka kufanya Mikutano yao Polisi wanawazuia kwa Kigezo cha Usalama.

Hii hali haina Afya kwa CCM na kama kweli CCM inataka Kuwa Imara basi ikubali Changamoto. Inaboa na inakera kama si kuudhi pia. Hivi ni Mikutano tu ya Wapinzani nchini ndiyo huwa ina Visharia vibaya vya Usalama ila yetu Sisi wana CCM ndiyo huwa iko Shwari?

Hebu na Sisi wana CCM ifike muda basi tuone Aibu na tumuogope Mwenyezi Mungu kwani hiki kinachofanywa na Polisi ambacho nashawishika kusema kuwa kina baraka kutoka CCM Kwetu si kitendo cha Hekima na Busara na sidhani kama hata Chama chetu Kitabarikiwa kwa Upuuzi huu wa Kiuonevu dhdi ya Wapinzani nchini.

Kwani kama Sisi CCM tunajiamini kuwa tupo vyema katika Kuwaletea Maendeleo Watanzania hivi Wapinzani wakipita Kutusema vibaya huku na kule Sisi tutaathirika na nini hadi tuanze Kuwazuia na Kuwasumbua kila Uchao kana kwamba Wao siyo Watanzania na hawana Haki ya Kufanya Siasa zao hapa nchini?

Na hakuna Jambo lililonikera kama kusikia kuwa kuna Chama Kimoja ( nadhani ni CHADEMA ) walikuwa wamepanga Kufanya Dua / Maombi huko Mkoani Morogoro hasa ya Kuwaombea Marehemu wa ile Ajali mbaya ya Moto wa Petroli na cha Kushangaza Polisi wamewazuia kwa sababu ambazo hazina Miguu wala Kichwa na siogopi Kusema wazi hapa kuwa ni sababu za Kipumbavu na narudia tena kusema kuwa ni sababu za Kipumbavu ( mkinuna nuneni tu hadi mpasuke )

Kinachoniuma zaidi ni kuona wana CCM wengi wakinyamaza katika hili na kuona kuwa ni Jambo jema kabisa wakati katika Medani za Siasa na Demokrasia wala halina Afya na Ustawi mwema kwa nchi yetu kwa Siku za baadae kwani linazidi Kuzalisha Uadui na Chuki Kubwa baina ya Watanzania ambayo inaweza hata Kuathiri Usalama wetu kwa Siku zijazo.

Namalizia kwa Kusema Polisi Tanzania na Mamlaka za Kiuongozi acheni kuwaonea, kuwasumbua na kuwanyanyasa mno Wapinzania na waacheni tu wafanye Siasa zao ila nyie wapeni tu Ulinzi kama Jukumu lenu Mama na Kazi ya kujua kuwa Wao ni Waongo au Wafitini au Wachochezi mtuachie Sisi Wananchi.

Tunaposema kuwa tunamuenzi Hayati Baba wa Taifa Nyerere basi tuhakikishe tunamuenzi Kiukweli na Kuyaiga yale mema aliyokuwa akipenda Kuyafanya. Nyerere hakupenda Visasi, Nyerere hakupenda Kutengeneza Maadui, Nyerere hakupenda Kusifiwa, Nyerere hakupenda Unafiki, Nyerere hakupenda Uwongo, Nyerere hakupenda Dharau bali alipenda mno Kusikilizana na Kuheshimiana. Mambo yenu mengine mnayoyafanya sasa mnatufanya kila mara tuwe tunamkumbuka huyu Mzee na kuanza Kumlilia kwani huenda angekuwepo hai angewakemeeni na mngemuelewa.

Kuna vitu hata kama Wewe ni mwana CCM ila vinaudhi, vinakera na havivumiliki. Nipo tayari Kuchukiwa kwa huu Uzi ila najua mbele ya Mwenyezi Mungu nimesema ukweli wangu Kwenu na huenda wakati nyie mtanichukia Mimi An Eagle kwa haya niliyoyasema hapa ila kwa Mungu ataniongezea Baraka kadhaa kwakuwa Yeye hutupenda mno Watu wawazi na wakweli kama Mimi na Wana CCM wenzangu baadhi tunaojitambua.
 
Hii hali haina Afya kwa CCM na kama kweli CCM inataka Kuwa Imara basi ikubali Changamoto. Inaboa na inakera kama si kuudhi pia.
Hongera hata mama ako huko aliko najua amefurahi kuwa toka akuzae leo ndio umeandika point.
 
UNADHANI YALIYOSEMWA NA REO HUKO IRINGA YALIKUWA NI BAHATI MBAYA?UNGANISHA NA YANAYOTOKEA SASA
 
Mm sio chadema ila hyo kitu inanikera kupita kiasi aisee! Napatwa na hasra sana, alafu hapo hapo ccm wao ya kwao wanafanya!
 
CCM wanadhani wana hati miliki ya kutawala nchi hii na makamanda wa polisi wanasaka vyeo na kulinda ajira zao!
 
Msiwasingizie polisi ni watekelezaji tu, kama mnaubavu mkemeeni mwenye kiti wenu ndiye mtengenezaji wa mambo yote.
 
Mkuu Mleta uzi kama umeamua kusema kweli ni vyema ukasema bila kupepesa macho. Anayeagiza wapinzani kunyanyaswa na kunyimwa haki yao ya kufanya shughuli halali za kisiasa, ni mwenyekiti wa ccm kupitia madaraka yake ya urais. Na anafanya hivi kwakuwa yeye binafsi hawezi siasa za ushindani na hawezi kusikiliza hoja kinzani kwani atashindwa kusifiwa. Huenda kweli kuna baadhi ya wanaccm hawapendi hali hii lakini hawana uthubutu wa kuongea ukweli, hasa mahali ambapo kuna maslahi yao. Ila wanaccm wengi wanafurahia hali hii kwani, ni fursa kwao kuendelea kupata fursa za vyeo kwa njia nyepesi.

Ni dhahiri kutokana na zama kubadilika binadamu ana tabia ya kuchoka, na ccm kwa sasa imeshachokwa, hivyo haina uwezo tena wa kupambana kwa hoja, na hata kama inazo watu wamekinai tu wanataka kitu kipya. Mwenyekiti wa ccm kwa kutambua ukweli huu huku akijua kabisa upinzani ndio wenye mvuto, ni bora awazuie hata kwa ukatili ili afanye hayo maendeleo kwa matarajio watu watarudisha upendo kwa ccm. Asichofahamu ni kuwa anapingana na nature, kwani mabadiliko ni lazima yawepo ili kuwe na balance of nature.
 
Mkuu inaonekana wewe Ni ccm asili, kwa sasa ccm mkakati Ni kuhakikisha wapinzani hawapati mwanya wowote ndugu, kwao mtanzania halisi Ni mwanaccm tu.ndo maana lissu alipigwa risasi ka jambaz
 
Back
Top Bottom