Ifike mahali watu tuzidai haki zetu kwa vitendo

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,227
113,580
Haki ya Watanzania kuweza kukutana na kufanya mambo yao kwa amani ni haki ya msingi kabisa na ni haki iliyopo kikatiba. Mtu mmoja au kundi la watu wachache kwa nini tuwaachie waikiuke hiyo haki na sisi tunaishia tu kulalamika halafu muda si mrefu tunasahau!!

Katiba ya sasa inakiukwa waziwazi hadharani mchana kweupe kabisa na hatufanyi kitu. Tunaishia kulalamika na kudai katiba mpya! Hiyo katiba mpya nayo ikinajisiwa, tutafanya nini?

Huu ndo mmoja wa mfano wa mabadiliko ya kifikra ninayoyazungumzia. Laiti tungekuwa na watu wengi walio na mwamko juu ya haki zao za msingi, tungekuwa tuko mbali sana.

Kwingineko huko duniani huwezi kuwanyima watu haki yao ya msingi ya kuweza kukutana kwa amani na kufanya mambo yao. Watakuburuta toka huko Ikulu wakushikishe adabu.

Unapoinajisi katiba namna hiyo maana yake wewe upo juu ya hiyo katiba.

Sisi ni mazoba sana.
 
Back
Top Bottom