Ifikapo Januari 31, 2021 wafanyabiashara wasiotumia mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) hawataruhusiwa kuingiza bidhaa sokoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,376
2,000
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema ifikapo Januari 31, 2021 wafanyabiashara wasiotumia mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) ulioanza kutumika Novemba 1 mwaka huu hawataruhusiwa kuingiza bidhaa zao sokoni.

Taarifa iliyotolewa leo Desemba 30 na TRA imezitaja bidhaa hizo kuwa pamoja na juisi za matunda na mbogamboga, maji ya kunywa ya yaliyofungashwa kwenye chupa, na bidhaa za fllamu na muziki (yaani,CDNCDs/DVD/Kanda zilizorekodiwa).

“Hatua hii inafualia kukamilika na kuanza kwa matumizi ya mfumo huu kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili kwa bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia, na aina zote za vileo tangu Januari 15, 2019 na kwa bidhaa za vinywaji laini mnamo tangu Agosti 1, 2019 mtawalia,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imerejea kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, sura ya 399 R.E 2019 ikitahadharisha uzalishaji na uingizaji wa bidhaa hizo sokoni bila stempu hizo.

“Kuanzia mnamo Novemba 1, 2020 lazima bidhaa kama juisi, maji ya kunywa yaliyofungashwa kwenye chupa, kazi za filamu (kwa mfano, CDsNCDs/DVDs/Kanda zilizorekodiwa), zitakazozalishwa ama ndani ya nchi au kuingizwa kutoka nje ya nchi ziwe zimebandikwa Stempu za Kodl za Kielektroniki kama ilivyoelekezwa katika Kanuni ya 4 ya Kanuni,” imesema taarifa hiyo.

TRA imesema kwa kuwa bidhaa hizo hazikuwa zikibandikwa stempu hapo awali, hivyo basi, bidhaa zote zilizopo sokoni na kwenye maghala ya watengenezaji au waingizaji wa bidhaa hizo, ambazo hazijabandikwa stempu hizo zinaruhusiwa kuendelea kuuzwa kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu (3), yaani, ama kabla au hadikufikla mnamo tarehe 31Januari2021.

“Baada ya tarehe hiyo, bldhaa hizi zote hazitaruhuslwa kuwepo sokoni bila kubandikwa Stempu za Kodi za Kielekroniki.

TRA imewataka wazalishaji na waagizaji kutoa taarifa kwao juu ya idadiya bidhaa alizonazo ambazo hazijabandikwa stempu za kodi za kielektroniki kabla ya tarehe rasmiya kuanza matumizl ya mfumo huu kwa kujaza fomu maalum inayopatikana kwenye ofisi za TRA za kila Mkoa na katika tovuti ya Mamlaka hiyo (www.tra.go.tz).

“TRA inawakumbushwa wafanyabishara na wadau wote kuwasilisha taarifa kamili ya chapa zao (brands) na idadi ya stempu za ETS wanazokusudia kutumia kwa mwaka ujao iii waweze kusajillwa katlka Mfumo wa usimamiziwa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETSMS) na kuweza kuagiza stempu kupitia tovuti salama (https:l/taxstamp.tra.go.tzJ) lliyofungamanishwa ndani ya tovuti ya Mamlaka,” imesema taarifa hiyo.
 

Heisenberg

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
1,166
2,000
Ni njia nzuri ya kukusanya mapato. ila kama kawaida yetu sisi waTz utasikia bia hazipo sokoni kisa mashine ya TRA ya kuprint sticker imeharibia.
Mara utasikia mifumo inasumbua. Mara sijui mzabuni wa kuleta wino kafa, mara karatasi sijui zimeisha, Sijui tenda imetangazwa Nk.

Pia TRA iweke wazi namna ya Kuhakiki kama sticker husika ni Halali maana Muda si mrefu wanamchi watanunua printer zao binafsi
 

Kokolo

JF-Expert Member
Mar 20, 2008
933
1,000
Ni njia nzuri ya kukusanya mapato. ila kama kawaida yetu sisi waTz utasikia bia hazipo sokoni kisa mashine ya TRA ya kuprint sticker imeharibia.
Mara utasikia mifumo inasumbua. Mara sijui mzabuni wa kuleta wino kafa, mara karatasi sijui zimeisha, Sijui tenda imetangazwa Nk.

Pia TRA iweke wazi namna ya Kuhakiki kama sticker husika ni Halali maana Muda si mrefu wanamchi watanunua printer zao binafsi
Sticker bandia hiyo ni economic crimes, hapo ni jera miaka mingi sana, au penalty kubwa Sana, kosa la uhujumu uchumi, etc.
 

Guasa Amboni

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
8,251
2,000
Kama nawaona wauza gongo kimpumu mnazi mbege na kangara wakilifuatilia zoeI hill kwa umakini mkubwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom