Ifahamu siku ya uapisho wa Rais nchini Tanzania na maana ya ishara zinazoambatana na matukio wakati wa uapisho

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,781
898
IFAHAMU SIKU YA UAPISHO WA RAIS.

MATUKIO YANAYOFANYIKA.


Katika hafla ya uapisho kunakuwa na matukio mbalimbali kama ifuatavyo;
✍🏽Kupigwa kwa mizinga 21.
✍🏽Ukaguzi wa gwaride.
✍🏽Salaamu kutoka katika vikosi vya kijeshi.
✍🏽Burudani.

KULA KIAPO.

Katika hafla ya uapisho tukio la Rais kula kiapo ndio tukio kuu.

Kwenye tukio la uapisho huambatana na maandamano ya majaji na Rais mteule kuelekea jukwaa la uapisho.

Rais mteule anakula viapo vitatu ambavyo ni kama vifuatavyo:

Kiapo cha kwanza; Rais anaapa kuwa atakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wake wote, ataihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kiapo cha pili; Rais anaapa kuwa atawatendea haki watu wote kwa mujibu wa sheria, mila na desturi za Tanzania bila woga, upendeleo, huba wala chuki.

Kiapo cha tatu; Rais mteule anakula kiapo cha kudumisha Muungano, kwamba atautetea na kuudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
.
.
KATIBA, MKUKI NA NGAO.

Baada ya kula kiapo Rais atapewa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kama kitendea kazi chake.

Aidha, atatakiwa kukaa kwenye kigoda cha jadi na kukabidhiwa Mkuki na Ngao kama ishara ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
.
.
BAADHI YA SEHEMU YA HOTUBA YA MH. RAIS. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI BAADA YA KULA KIAPO CHA KUWA RAIS.

🇹🇿 "Bado tunayakumbuka tuliyoahidi katika ilani yetu ya uchaguzi ya CCM yaliyoandikwa katika kurasa 303."- Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Tutaendelea kudhibiti rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za umma. Niwakumbushe tuu kuwa mwisho wa uchaguzi huu ndio mwanzo wa uchaguzi ujao"- Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Niwapongeze wabunge wote waliochaguliwa, na bahati nzuri mwaka huu wabunge wengi ni kutoka Chama Cha Mapinduzi."- Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Kwa kipekee kabisa pia nimpongeze Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mwinyi. Pia nikishukuru sana Chama Changu Cha Mapinduzi kwa ushindi wa kishindo Bara na visiwani"- Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Tulianza na uzinduzi wa kampeni Dodoma na tumemaliza Dodoma. Ni dhahiri kuwa ushindi tulioupata wanaccm umetokana na baraka zenu wana Dodoma, ahsanteni sana."- Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Tofauti ni kwamba mwaka 2015, niliapa nikiwa Dar es Salam Ila Leo naapa nikiwa Dodoma. Namshukuru Sana MUNGU kwa Jambo hili." - Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Kwa moyo wa unyenyekevu mkubwa nipende kumshukuru MUNGU kwa kutupa afya ya kuiona siku hii ya leo." - Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Niwashukuru viongozi wa tume ya Uchaguzi pamoja na vyombo vya ulinzi kwa kusimamia vizuri zoezi la Uchaguzi wa mwaka huu." - Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Niwashukuru sana watanzania kwa hali ya utulivu mkubwa katika kipindi chote cha uchaguzi. Hii inaonyesha uchaguzi ulikuwa huru na wa haki." - Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Nipende pia kuwashukuru pia viongozi wa mataifa mbalimbali kuungana nasi kwenye hafla hii." - Dkt. Magufuli

🇹🇿 "Napenda pia kuwaeleza watanzania wote kuwa uchaguzi sasa umekwisha, narudia tena uchaguzi sasa umekwisha. Jukumu lililopo mbele yetu ni kuweka jitihada katika kuleta maendeleo ya Taifa letu." - Dkt. Magufuli
IMG-20201106-WA0098.jpg
IMG-20201106-WA0102.jpg
IMG-20201106-WA0100.jpg
IMG-20201106-WA0101.jpg
IMG-20201106-WA0082.jpg
 
Ujanjaujanja Tu!!😁😂😀😀😄😄😄😄
Shukrani Sana Mleta Mada
Wabunge Nao Wanakula Kiapo Cha Kugonga Meza 😏🙄😀😀😁
 
Alafu katiba nayo huwa ni maneno,kiapo cha kwanza na pili ameshavisahau

na hicho cha 3 huenda Ismael Jussa akawa na jibu sahihi.
 
Kakwepa nitaihifadhi kuilinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maana yake?
 
Ujanjaujanja Tu!!😁😂😀😀😄😄😄😄
Shukrani Sana Mleta Mada
Wabunge Nao Wanakula Kiapo Cha Kugonga Meza 😏🙄😀😀😁
Hahahaah...au wanakula kiapo cha kula poshooo (joke).

Wabunge wanakula kiapo cha kuwatumikia wananchi (real)
 
1604775178305.png

Huu mkuki una uzito gani? Je kwenye ulimwengu huu wa teknolojia, mikuki ina kazi gani?
Wale Wakulungwa wakulabilangwa 900 kutoka Gamboshi Bado wako kwenye payroll?
 
Mbona sijaona shukrani kwa wapiga kura,shukrani zimeenda kwa NEC na vikosi vya ulinzi.
 
Tunakoelekea miaka ijayo ma Rais wajao wapewe Smg na Radar.
Hivyo ndo watoto wetu wanasoma shuleni,mikuki na ngao,hata kwenye katuni hawaioni sikuizi.,wakendelea kuwapa marais hivyo vitu watoto na wajukuu wetu watakuja kutusumbua kwa maswali wakiuliza hivyo ni vitu gsni.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom