Ifahamu Sayari Ambayo kila mtu and Uwezo wa kwenda bila gharama yeyote.

streat Anthem

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
395
474
Habari za wakati huu? Lengo la huu uzi ni kuwafahamisha KuhusuYa uwepo wa sayari ambayo kila mtu ana uwezo wa kwenda bila gharama yeyote.

Kwanza Kabisa nisifu uwezo na juhudi za wanasayansi na wataalamu wa mambo Ya anga ambao kila kukicha wanagundua sayari na nyota mbalimbali katika anga. Juhudi zao zimechangia kukua kwa maendeleo ya mwanadamu kwa kiasi kikubwa Sana. Pia niyapongeze mataifa kama Marekani, urusi na mengineyo kutoa mchango mkubwa sana katika kuwezesha wanasayansi, na pia kuwa mataifa ya kwanza kufanikisha binadamu kwenda anga za juu.

Juhudi za wanasayansi na mataifa makubwa katika kugundua sayari na nyota mbalimbali katika anga zimekua chachu ya kila nchi zinazoendelea kupambana na kuhakikisha na wao wanakua na Uwezo huo.

Lakini ugunduzi huo haujaleta matumaini kwenye Maisha Ya mwanadamu, haujatatua matatizo makubwa yanayomkabili mwanadamu kama magonjwa,njaa,umasikini, vita na kifo,.

Hatua hii imekuwa sababu ya mataifa yaliyoendelea kiuchumi kuzinyonya na kuzigandamiza nchi zinazoendelea.


Lakini kuna tumaini jipya la mwanadamu ambalo ndio suluhisho la matatizo yote yanayomkabili mwanadamu.
Sayari hii sio ngeni masikioni mwa wengi lakini itakua mpya machoni Pa wengi.
Ni sayari ambayo hakuna vita, njaa, umasikini, kifo, hofu, magonjwa na kila aina ya uovu.
Ni sayari ambayo inakupa tumaini jipya na furaha ya milele, hutochoka kuishi ndani ya sayari hii kwa Maana ina kila kitu ambacho kinaipendeza roho ya mwanadamu.

Ni sayari ambayo hautatumia gharama yeyote kusafiri au kwenda huko kama wamarekani wanavyotumia mabilioni ya dola kwenda anga za juu au mwezini .
Ni sayari ambayo inatumia muda mchache kufika tofauti na Urusi wanavyotumia miezi na miaka kufika huko.
Ni Sayari ambayo haihitaji roketi na mandege makubwa na ya gharama.

Sayari hii inahitaji kukubali kubadili fikra zako, matendo na mienendo yako pamoja na moyo wako
Inahitaji uishi vyema na umpendeze Mungu kwa matendo yaliyotukuka.
Chombo cha usafiri kwenda kwenye Sayari hii ni maisha yetu na tiketi ni matendo yetu mema

Na Sayari hii ni UPENDO kwa Maana Mungu ni Pendo na kila kitu kwake kinawezekana.

Tukiishi ndani ya sayari ya Upendo njaa,umasikini,vita,dhiki,uoga,hofu,mateso,uovu,kifo,utumwa na kila aina ya baya litakua halina nafasi.

Nina amini kama mataifa tajiri yangewezesha binadamu tusafiri na kwenda kuishi katika Safari hii hakuna hata mmoja amabaye angerudi huku.
Je unapenda kwenda na kuishi ndani Ya sayari hii? Basi mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe, mpende Mungu wako kwa moyo,nguvu na akili zako zote na upende mazingira yanayokuzunguka.

Nawatakia Safari njema wapendwa mi mtanikuta tayari nimeshatangulia.
 
Wale wavuta bangi na watumiaji wa madawa ya kulevya na wenyewe huwa wanaenda sayari gani?

Nafikiri kwenda kwenye hii sayari unayoisema itakugharimu kifo, baada ya kutekeleza yote uliyoyapendekeza.
Hii sayari haikugharimu kitu chochote zaidi ya kufanya maamuzi yaliyo sahihi

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom