Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Ukipata cream jamii ya allylamines kwenye pharmacy kubwa itakufaa sana.

Ukioga hakikisha umejikausha kabisa na taulo

Usishirikiane taulo na mtu mwingine na ufue kila wiki na kulianika juani.

Paka dawa mara mbili au tatu kwa siku, asubuhi ukiamka, lunch time na kabla hujalala.

Vaa boxers za cotton.
hizi cream ndio kama Clotrimazole ,Nizoral,Ketoconazole ama ni tofauti ???
naomba kujua
 
Nimepona....nitaweka tips nilizotumia
Oh, nafurahi kuwa ulipona na tatizo lako la fungus…japo nimekuta umepona, nakupa pole kwa mateso yaliyokupata!
tatizo ulilokuwa nalo ni kweli kabisa ni fungus, nilipokuwa sekondari niliwaji kupata na iilisababishwa na kuvaa chupi bila ya kujifuta maji mara baada ya kuoga au kujitawaza! Pia kurudia kuvaa chupi bila kufua…kwa kifupi ni uchafu na unyevunyevu ndio haswa ndio visababishi vya kuwafanya kuvu (fungus) hao kuota na kukua.
dalili ni hizohizo kujikuna sana hata kujichubua ngozi na kusababisha majeraha ambayo hutoa majimaji na baadaye kuweka tabaka gumu ambalo pia huwasha sana. Ukioga maji ya baridi utapata maumivu siyo ya dunia hii na hivyo unashauriwa kuoga maji ya vuguvugu! Mara unapooga zingatia kujifuta vizuri na upake antifungal powder na siyo dawa yoyote ya cream au majimaji. lengo ni kutengeneza mazingira makavu ktk maeneo ya sehemu za siri. na kumbuka kupiga pasi taulo ili kuua kuvu wanaojishikisha kwenye taulo. Pia ukumbuke kuvaa chupi safi na kamwe usurudie kuvaa chupi chafu.
Dawa kama mycota powder ni kiboko kwa aina ya kuvu hawa na ukianza kuitumia matokea ni ndani ya masaa 24 hali inadarikia na unapomaliza wk unakuwa na dalili za kupona kabisa. Lakini hata hivyo unapaswa uendelee na matibabu kwa takribani wiki mbili baada ya dalili zote kupotea.
Niseme tena pole sana kwa maswahibu yaliyokukuta na samahani kwa kuwa sikutembelea janvini kwa kipindi kirufu sana.
enzi hizo mimi niliubatiza ugonjwa huo wa fungus kama 'pumbu erosion' yaani 'mmomonyoko wa korodani/mapumbu!
 
Pumbu erosion ni ugonjwa wa kuvu(fungus) unaowapata watu wenye kwenye mikunjo ya ngozi sehemu ya siri zenge joto na unyevunyevu…hasa kwenye mapumbu/korodani

Nilipokuwa sekondari niliwaji kupata na iilisababishwa na kuvaa chupi bila ya kujifuta maji mara baada ya kuoga au kujitawaza! Pia kurudia kuvaa chupi bila kufua. Kwa kifupi ni uchafu na unyevunyevu ndio haswa ndio visababishi vya kuwafanya kuvu (fungus) hao kuota na kukua.

Dalili ni hizo hizo kujikuna sana hata kujichubua ngozi na kusababisha majeraha ambayo hutoa majimaji na baadaye kuweka tabaka gumu ambalo pia huwasha sana.

Ukioga maji ya baridi utapata maumivu siyo ya dunia hii na hivyo unashauriwa kuoga maji ya vuguvugu! Mara unapooga zingatia kujifuta vizuri na upake antifungal powder na siyo dawa yoyote ya cream au majimaji.

Lengo ni kutengeneza mazingira makavu ktk maeneo ya sehemu za siri. Na kumbuka kupiga pasi taulo ili kuua kuvu wanaojishikisha kwenye taulo. Pia ukumbuke kuvaa chupi safi na kamwe usirudie kuvaa chupi chafu.

Dawa kama mycota powder ni kiboko kwa aina ya kuvu hawa na ukianza kuitumia matokea ni ndani ya masaa 24 hali inabadirikia na unapomaliza wiki unakuwa na dalili za kupona kabisa. Lakini hata hivyo unapaswa uendelee na matibabu kwa takribani wiki mbili baada ya dalili zote kupotea.

Nawasilisha!
 
Husababishwa na uchafu
Mimi pia nilisoma boarding na sikua najifuta huko nikitoka kuoga ila sikuwahi kuupata
Unatakiwa uwe unaoga mara kwa mara na uwe na boxer nyingi, nilikua nazo zaidi ya 5 na nilikua naanika juani, huu ugonjwa niliusikilizia tu kwa watu, na mpaka leo naeza kuoga nisijifute na taulo ila sijawahi kuumwa
 
Huo ufala ulinipata nikiwa form 3 aisee acha kabisa.

Chanzo nilinunua boxer za mpira Ubungo pale. Zile boxer zilinisababishia hayo matatizo kende zikawa na rangi ya kungu flani na wingu jeusi jeusi usipime hayo maumivu yake. Ilikuwa class sikai halafu kipindi cha joto yanawasha kinoma

Likizo nilikuja nikapata cream na nikabadili boxers na kununua za cotton nikapona. Tangu na hapo sijawahi kulipata tena hilo gonjwa.
 
Hata kama huna pumbu erosion unashauliwa kunyoa vzr sehemu hizo na upake limau kwaajili ya kupaweka Safi kabisa bila harufu wala chochote.Hata kwapa paka limao baada ya kunyoa.

Wadada kamulia limao kwny kikombe cha kuogea then dailute na maji then safisha dyudyu Kwa nje hasa mara tu baada ya bleeding.Ba hata ukinyoa pia.Hakika ukifanya hivi unabaki msafiii hata uvinza mtu anakuendea bila wasiwasi.
 
ukinipata mwezi wa 3 tu hapo....

Me nkaupotezea, usiku napiga gitaa hadi ngozi yote inatoka korodani znabak na ngo nyekundu kama inataka kutoa damu hivi... Nliacha tu maana hujaga na kupona wenyewe,

Kilichonikuta sasa kilinikimbiz pharamcy kununua cream ya kupaka.. Ilikua hivia bwana..

Nilienda bafun kuog sasa kila nkitafuta sabuni siioni, na nina haraka sana, nkatafta tafuta wapi, nkaona isiwe shida acha niogee ya unga...

Dk 2 mbele naanza kuhisi kama nachanwa chanwa na viwembe katika korodani, maumivu yake hakika ni kama zmekatwa na kunyofolewa kabisa..

Sio raggae sio kiduku vyote nilicheza... Ilipopoa chaap nko pgamacy siamini kama mzima
 
Huo ufala ulinipata nikiwa form 3 aisee acha kabisa.

Chanzo nilinunua boxer za mpira Ubungo pale. Zile boxer zilinisababishia hayo matatizo kende zikawa na rangi ya kungu flani na wingu jeusi jeusi usipime hayo maumivu yake. Ilikuwa class sikai halafu kipindi cha joto yanawasha kinoma

Likizo nilikuja nikapata cream na nikabadili boxers na kununua za cotton nikapona. Tangu na hapo sijawahi kulipata tena hilo gonjwa.
poleee
 
kwa wale wa "MATEMA BEACH HIGH SCHOOL" form six class of 201* hii kitu kwao sio ngeni kabisa, ase unanikumbusha ugonjwa huu ulisumbua Sana watu kitambo hiyo na sababu kuu ya huu ugonjwa mm nuliona unasababishwa na maji yaliyokuwa yakitumika

Ase asikwambie mtu bob kile kipindi shule inakaribia kufungwa vile uko na kipururu and at the some time uko na pumbu erosion lina kuwa jambo la aibu Sana kwa mchumba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom