Ifahamu Parole ni nini? Wengi hamjui faida zake

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
8,397
2,000
Magufuli katekeleza ahadi yake “Nitafanya kazi na wana CCM, Nitafanya kazi na wapinzani” Katika uteuzi wake juzi, Kamteuwa Ndg. AUGUSTIONO LYATONGA MREMA-TLP kuwa mkuregenzi mpya wa Bodi ya PAROLE, ni bodi iliyo chini ya wizara ya mambo ya ndani kitengo cha MAGEREZA.

PAROLE NI NINI?

Parole ni utaratibu wa kisheria unaompa fursa mfungwa aliyehukumiwa kutumikia kifungo gerezani cha miaka minne na kuendelea, kutumikia sehemu ya kifungo chake katika jamii kwa masharti maalum baada ya kukidhi vigezo vifuatavyo

i). Awe ametumikia theluthi (1/3) ya kifungo chake na kuonesha mwenendo wa kurekebika kurudi katika jamii kumalizia sehemu ya kifungo chake kwa masharti maalum. Masharti hayo ni:
• Kuwa chini ya uangalizi maalum kuhakikisha kuwa hatendi kosa lolote mpaka atakapomaliza kifungo chake.
• Kuzingatia masharti ya Parole anayopewa kikamilifu
• Kuwa raia mwema na kuishi kwa kujipatia kipato halali katika jamii.
ii). Awe ameonesha kujutia kosa, kurekebika tabia na kuonesha mwenendo mzuri gerezani.
iii). Mamlaka husika kujiridhisha kuwa hatahatarisha usalama wa jamii.

Malengo ya kuanzishwa kwa Parole:
Madhumuni ya kuanzishwa kwa utaratibu wa Parole Nchini hayatofautiani na madhumuni ya kuanzishwa kwa utaratibu huu kwenye nchi nyingine duniani zikiwepo nchi za Afrika kama vile: Afrika kusini, Zambia na Namibia. Mfumo wa Parole ulioainishwa hapa nchini unatokana na uzoefu wa Parole unaotumika nchini Canada. Sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa Parole hapa Nchini ni:-
i. Kuhusisha jamii katika suala zima la urekebishaji wa wafungwa badala ya kutegemea serikali peke yake kwani chanzo cha uhalifu ni mazingira yanayotokana na jamii yenyewe.

ii. Kuwepo na kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wafungwa wenye vifungo virefu magerezani ambao kutokana na urefu wa vifungo vyao hawawezi kufaidika na programu zilizopo za urekebishaji kwa sababu ama watatoka magerezani wakiwa wazee wasiojiweza, watakutana na mabadiliko makubwa kijamii, kiuchumi na kisera wasiyoweza kuyamudu haraka/ipasavyo kwenda na wakati au watafia gerezani. Wafungwa wa aina hii hukata tamaa kwani hawaoni sababu ya kuwa na nidhamu wawapo gerezani, hivyo kusababisha usalama magerezani kuwa mashakani. Parole ilikusudiwa kuwarejeshea matumaini ya kurejea katika jamii na kuishi maisha ya kawaida na kupunguza tishio la kiusalama magerezani na katika jamii kwa ujumla

MUUNDO WA BODI ZA PAROLE
Kwa mujibu wa Sheria ya Bodi za Parole (Cap 400 R.E 2002) kifungu cha 3(2)(a-d) na 3(4-9) Bodi zifuatazo ziliundwa ili kuhakikisha kuwa Sheria ya Parole inatekelezeka hapa nchini.

Bodi ya Taifa ya Parole:

Bodi hii inaundwa na Wajumbe wafuatao:-
a) Mwenyekiti wa Bodi ambaye huteuliwa na Mheshimiwa Rais.

b) Wajumbe wawili ambao huteuliwa na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

c) Wajumbe sita ambao huingia kwenye Bodi kutokana na nyadhifa zao.

Wajumbe hao ni:-
i). Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) au Mwakilishi wake
ii). Mganga Mkuu wa Serikali
iii). Kamishna wa Ustawi wa Jamii
iv). Afisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais
v). Mkuu wa Jeshi la Polisi au mwakilishi wake
vi). Mkuu wa Jeshi la Magereza ambaye ndiye Katibu wa Bodi

Bodi za Parole za Mikoa
Bodi za Parole za Mikoa zinaundwa na Wajumbe wafuatao:-
a) Mwenyekiti wa Bodi ambaye huteuliwa na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

b) Wajumbe wanne ambao huteuliwa na Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

c) Wajumbe sita wanaoingia kwenye Bodi moja kwa moja kutokana na nyadhifa zao.
Wajumbe hao ni:-
i). Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Kanda au mwakilishi wake
ii). Mganga Mkuu wa Mkoa
iii). Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa
iv). Ofisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
v). Mkuu wa Polisi wa Mkoa (RPC) au mwakilishi wake
vi). Mkuu wa Magereza wa Mkoa (RPO) ambaye ndiye Katibu wa Bodi
Bodi hizi hudumu kwa kipindi cha miaka mitatu, baada ya hapo uteuzi mpya hufanyika.

SIFA ZA MFUNGWA WA PAROLE
Sheria ya Bodi za Parole Sura 400 ya mwaka 2002 na Kanuni zake za mwaka 1997 inaainisha kuwa mfungwa anayetumikia kifungo cha kuanzia miaka minne (4) na kuendelea anastahili kunufaika na mpango wa Parole kama atakuwa na sifa zifuatazo:-
i. Asiwe amehukumiwa kifungo cha maisha

ii. Asiwe ni mfungwa anayetumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, madawa ya kulevya na makosa yanayohusiana na kujamiiana.

iii. Asiwe ni mfungwa ambaye kifungo chake kimebatilishwa kutoka kwenye kifungo cha kunyongwa.

iv. Awe anatumikia kifungo kisichopungua miaka minne (4) au zaidi na awe ametumikia 1/3 ya kifungo chake.

v. Awe ameonesha tabia na mwenendo mzuri kwa muda wote aliokaa gerezani.

vi. Asiwe na pingamizi la kimahakama la kukataliwa kunufaika na utaratibu wa Parole chini ya Kifungu cha 67 cha Sheria ya makosa ya Jinai.

JE;MFUNGWA WA PAROLE ANAWEZA RUDISHWA GEREZANI?

NDIYO, Mfungwa wa Parole wakati wote wa Parole anatakiwa kufuata masharti aliyopewa na kutii Sheria za nchi na kuishi kwa amani wakati wote kama Sheria ya Bodi za Parole na Kanuni. Masharti hayo yameainishwa sehemu ya 3 kanuni ya 5(5) (a-h). Inapotokea akivunja masharti ya Parole au kufanya uhalifu taarifa hupelekwa kituo cha Polisi na mfungwa hujulishwa kuhusu kusudio la kutengua Parole yake na ikithibitika tuhuma zilizotolewa dhidi yake ni za kweli hurudishwa gerezani na kufunguliwa mashtaka mapya na kupelekwa mahakamani, ikithibitika kweli amevunja masharti Mahakama ndiyo yenye uwezo wa kutengua Parole baada ya kumsikiliza kwa mujibu wa Kanuni ya Sheria ya Bodi za Parole za mwaka 1997 sehemu ya 5, 9(a-d) na Kanuni ya 10 (1-2). Aidha Mahakama inayo uwezo kutengua Parole kwa mfungwa yeyote na kuamuru arudishwe gerezani kama ikithibitika kwamba:-

i. Amevunja sharti lolote la Parole

ii. Baada ya kupata maombi kwa maandishi toka kwa Mhe. Waziri kwa maslahi ya Taifa kwa mujibu wa Kanuni ya Sheria ya Bodi za Parole sehemu ya 5, 10(3) (a-c).

iii. Kama mfungwa husika atafanya uhalifu akiwa kwenye Parole.

JE; NI HATUA GANI HUFUATWA ILI MFUNGWA AWE PAROLE?

Kimsingi mfungwa anapoingia gerezani kwa mara ya kwanza hujulishwa kuhusu haki zake ikiwemo haki ya kuingizwa kwenye mpango wa Parole kama ana sifa kulingana na kosa lake na muda wa kifungo chake gerezani. Mfungwa mwenye sifa ya kuingizwa kwenye mchakato wa Parole anapotimiza 1/3 ya kifungo chake, Afisa Parole hukusanya taarifa mbalimbali zinazomuwezesha kujadiliwa katika Bodi za Parole; Taarifa hizo ni maoni kutoka kwa wazazi/ndugu zake, maoni ya mwathirika wa uhalifu, nakala ya hukumu, hati ya kifungo, maoni kutoka uongozi wa kijiji anachotarajia kwenda kuishi na maoni/taarifa kutoka kituo cha polisi kilichomkamata na pia matokeo ya uchunguzi wa alama zake za vidole kuhusu kumbukumbu zake za uhalifu. Taarifa hizi zote huwa ni kwa ajili ya kudumisha usalama wa jamii na wa mfungwa mwenyewe anufaikapo kwa Parole.

Baada ya Taarifa hizi zote kukamilika kila mfungwa anayependekezwa kunufaika na Parole hufunguliwa jalada (Prison Form 64) kwa ajili ya kutunza kumbukumbu zake pamoja na taarifa za tabia na mwenendo wa mfungwa. Mchakato wa kumjadili mfungwa huanzia katika Kamati za Urekebishaji ya Gereza. Kamati hiyo hupitia taarifa hizo na kutoa maoni na mapendekezo kwenda Bodi ya Parole ya Mkoa. Bodi ya Parole ya Mkoa hupitia maoni na mapendekezo hayo na baada ya uchambuzi wa kina, hutoa mapendekezo yake kwa Bodi ya Taifa ya Parole kupitia kwa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole.

Sekretarieti ya Taifa ya Parole ina jukumu la kuratibu shughuli za Bodi. Hivyo hupokea taarifa za wafungwa waliopendekezwa au kutopendekezwa kunufaika na Parole kutoka katika Bodi za mikoa. Huchambua taarifa hizo na kuandaa taarifa ya kila mfungwa kwa ajili kujadiliwa na Bodi ya Taifa ya Parole. Bodi hiyo kwa kutumia taaluma mbalimbali walizonazo wajumbe wake na nyadhifa zao hufanya uchambuzi wa kina wa mawasilisho hayo na kutoa uamuzi mfungwa anufaike au asinufaike na Parole. Uamuzi wa Bodi ya Taifa ya Parole huwasilishwa kwa Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa Kifungu cha 6(4) cha Sheria ya Bodi za Parole Na 25 ya mwaka 1994 (Sura ya 400 R. E 2002). Mheshimiwa Waziri hupitia taarifa za kila mfungwa na kutoa uamuzi wa mwisho wa kukubaliwa au kukataliwa kunufaika kwa mpango wa parole. Uamuzi huo huwasilishwa kwa Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza.
HITIMISHO
Hakuna mtu anayezaliwa na tabia ya uhalifu. Jamii ndiyo inayomjengea mazingira ya kujifunza tabia hiyo. Hivyo basi, jamii inawajibika kubadili mazingira yake ili naye aweze kubadili tabia na kuishi kama raia mwema.
 
Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,128
2,000
Asante kwa somo zuri sana kuhusu PAROLE. Nilikuwa siyajui haya, nakushukuru tena.

Sijajua tu ni katika muktadha upi Augustino Lyatonga Mrema ni mpinzani
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,589
2,000
Hebu tupieni picha ya Mrema Lyatonga aliyopiga hivi karibuni tumuone.
 
sheriff john brown

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
636
1,000
Tunashukuru kwa elimu ya palole, ila katika hiyo ahadi ya rais kuteua wapinzani kufanya nao kazi ungerekebisha kwa kuwa Mrema ni familia ya ccm na kampeni yakuhakikisha magufuli ana shinda alishiriki
 
ctc database

JF-Expert Member
Jul 6, 2016
201
250

Uchambuzi Wa nguvu. Hivi ndugu zangu kwa nn hawa wafungwa wasingekuwa wanasaidia ktk kazi za kijamii. Kma MTU anapewa muda Wa uangalizi lkn anakuwa anakuwa labda anasafisha masoko, barabara n.k. mi naona ingekuwa poa
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
50,054
2,000
Sikuwahi kujua kama Tanzania kuna kitu kama hiki.
Nilikua naona kwenye movie tu.
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,692
2,000
Uchambuzi Wa nguvu. Hivi ndugu zangu kwa nn hawa wafungwa wasingekuwa wanasaidia ktk kazi za kijamii. Kma MTU anapewa muda Wa uangalizi lkn anakuwa anakuwa labda anasafisha masoko, barabara n.k. mi naona ingekuwa poa

Miji yetu ni michafu sana hao wangetumika kuisafisha, mahakama ni chakavu, wafungwa wangetumika kuzijenga na kuziboresha, barabara nyingi mijini zina mashimo kadhalika wafungwa wangetumika kuziba mashimo, nakumbuka nyumba nyingi za JKT miaka ya nyuma zilijengwa kwa nguvu za askari wa mujibu wa sheria na fedha ilihitajika kwa ajili ya kununua mabati mbao cement nk
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom