IFAHAMU NDOA KWA UNDANI ( Uvumilivu ni silaha kubwa) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IFAHAMU NDOA KWA UNDANI ( Uvumilivu ni silaha kubwa)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Aug 23, 2012.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Naona haya maswali ya ndoa ni too much Wana JF wenzangu, ambao mpo kwenye ndoa, kila ndoa ina matatizo yake kikubwa ni uvumilivu tu, hebu jaribu kufanya zoezi hili

  Tafadhari chukua glass ya maji mkononi, usisome tu naomba kama unaweza chukua glass jaza maji na ishike mkononi.
  Swali ambalo naweza kukuuliza ukisha ichukua mkononi ni je, glass ya maji ni nzito kiasi gani?
  Naamini jibu ni kwamba haina uzito wowote.
  ... Upo sahihi na umebarikiwa kwa jibu zuri.
  Hata hivyo ukweli ni kwamba hata kama uzito wa glass yenye maji si lolote, kama ukiishika kwa zaidi ya saa moja utaanza kusikia uzito wake, unavyozidi kuishika kwa muda mrefu ndivyo utajisikia uzito unaongezeka zaidi ingawa uzito wa glass ya maji ni ule ule.
  Utajisikia mkono kuanza kuuma na kulemewa na uzito kama vile umeshika bonge zito la tofali la sementi.

  Ndivyo mahusiano ya ndoa yanavyofanya kazi wakati mwingine.
  Kuishi wawili ni sharing ya mambo mbalimbali na kuna wakati mwenzako anaweza kukwaza, kukuumiza, kukusema vibaya, kufanya vibaya, kukutukana, kukudanganya nk na kila kitu unafanya kwake au wewe unafanyiwa kina uzito mkubwa au mdogo sana moyoni kwa partner wako.
  Hata hivyo unavyozidi kutunza vitu vidogovidogo vinavyokuumiza moyo bila kuviweka wazi kwa mwenzako ili muongee na kuyamaliza. Siku zinavyoongezeka na kwenda itafika siku mkusanyiko ya hayo mambo moyoni mwako utaanza kuwa mzito na kujisikia vibaya kwa mwenzako.

  Inawezekana chanzo cha hasira zako au uchungu ulionao au maumivu uliyonayo nk ni matokeo ya vitu ambavyo uliweka moyoni mwako miaka 5 au 10 au 25 iliyopita katika ndoa yako.
  Kubwa zaidi hukufanya juhudi yoyote kuhakikisha unaongea bayana na wazi kwa mke wako au mume wako na kutokana na hiyo tabia leo umefika hapa baada ya hayo mambo kujijenga kwenye moyo wako kwa miaka zaidi ya 5 nk.
  Huku mwenzi wako akiwa amesahau hayo mambo, wewe umeendelea kuyashika ndani ya moyo wako na ni wewe unayeumia kwani mwenzio hajui kama bado yapo moyoni mwako.
  Hata ukimwambia leo anaweza kuwa shocked kusikia kwamba bado ulikuwa umeweka jambo au mambo kama hayo moyoni.
  Kwa kuwa umeshindwa kuachilia imefika mahali umeona ndoa haina maana kwako, haikupi furaha na unaanza kufikiria mlango wa kutokea (anyway ndoa haina exit, ni deadend).
  Unajisikia humpendi tena mume wako au mke wako.
  Badala ya kidonda kupona sasa inazidi kuwa fresh.
  Na kidonda kinazidi kuliwa na wadudu na damu kutoka bila wewe kujua.
  Jifunze kuwa wazi na kuongea kwa mpenzi wako kama amekukosea mwambie na msahemeane na kusahau yaliyopita.

  AMEN.......!!!!
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Amen ni somo zuri kwa walio kwenye ndoa...maana tafiti nyingi zinaonyesha wenye ndoa 85% husema hawataki tena kuoa/kuolewa na mwenza wake baada ya miaka 5 ya kwanza tu!!
   
 3. kirumonjeta

  kirumonjeta JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 3,095
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Nani kasema NDOA haina exit????????weeeeeeeeeeeeeh wewe tu
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Maneno yaliyomo kwenye vitabu vitakatifu ndiyo yamesema......!!!!
   
 5. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Nyce lesson
   
 6. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,204
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  God be with you pamoja sana.
   
 7. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Ushauri wako si mzuri, wanandoa wengi ni wazinzi, hasa sisi wanaume, je, mkeo akikuambia kama karuka ukuta na watu watatu tofauti utamsamehe? Pia uvumilivu unakipimo chake, kikizidi ukaendelea kuvumilia unageuka kuwa mpumbavu. Ushauri wako ni wa miaka ya '85 kurudi nyuma. Ndoa za Sasa hivi watu hawana uvumilivu au mapenzi ya kweli wanataka maslai tu. Pia huo msemo wa hakuna ndoa isiyo na matatizo ni imani potofu ya kuwasihi watu (hasa wanawake) waendelee kuishi ktk ndoa kwa kunyanyasika. Koti likikubana unalivua na dawa ya jino ni kuling'oa.
   
 8. c

  christmas JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,608
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  i like it, big up mtoa mada
   
 9. Mc Tilly Chizenga

  Mc Tilly Chizenga JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 3,719
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  kimbweka leo umetembelewa na roho mtakatifu?umetoa mada ya ukweli

  ni kweli kusema hukuweka huru,lakini kwa tafakari yangu huwa naona ni kuhamisha mzigo wa maumivu kwa mwenzako.wewe msemaji unakuwa huru uliyemuambia anakufa ndani kwa ndani

  kwa akina mama tangu mwanzo mwa kuumbwa dunia hawakai na vitu,husema lakini hili limekuwa jambo moja kubwa linalochangia wanaume ktk ndoa kufa kabla ya wake zao kwa asilimia nyingi tu!

  wanaume tukianza leo kila jambo kulitoa tu kinywani wake zetu watakufa ktk miaka mi5 ya kwanza ya ndoa!maneno ni sumu kali inayoua taratibu.

  my conclusion:Mimi kama mimi kama kuna jambo litakuwa linanikwaza na nikilizungumza litamtoa machozi mke wangu,nipo tayari "liniue" kuliko niliseme "likamuue" mke wangu. Kwangu mimi kupona kwake mke wangu ni bora kuliko uzima wangu!nimemaliza!
   
 10. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Nimependa mfano wako wa 'glass ya maji'....ila sijui kama ndio unau'relate' na uvumilivu? Kama ndivyo, basi ina maana uvumilivu lazima uwe na kikomo (threshold) ambayo ikivukwa...uvumilivu hauwezekani. Ni sawa kama uwezo wako wa ku'hold' glass hiyo ya maji kwa saa 1 au 2, zikipita hizo ni lazima uweke chini hiyo glass au la utaidondosha uivunje kabisaa!

  Na pia kabla hujafikia hiyo 'threshold' ya kushindwa kuhold hiyo glass, kuna changes zitatokea kucompensate kuchoka kwa huo mkono, mfano kuchezesha chezesha mkono au vidole, kama mkono ulikuwa umeinuka basi utaanza kushuka chini taratiibu mpka ufikie pointi ambapo hata hizo compensatory mechanism hazisaidii tena!

  ndio vivyo hivyo kwa ndoa/mahusiano ya kimapenzi....utavumilia, lakini unachokivumilia kikiendelea..utadevelop compensatory mechanism...na bado kikiendelea, utatua mzigo au kuutupa kabisa! Sasa kwa nini tuone ile 'act' ya kutua/kutupa mzigo ndio mbaya na haionyeshi uvumilivu (kidini na kijamii inaonekana hivyo)? na tatizo ni kuwa, ni wewe tu mhusika ndio utakaebeba hiyo glass ya maji, no one will help you...hata kama umebeba glass kwa mkono wa kulia, wa kushoto hautakusaidia...kwa nini iwe 'issue' basi ukitua mzigo?

  Kuna watu wengi wako kwenye ndoa/mahusiano yasiyobebeka kwa kigezo tu cha dini yangu inasemaje kuhusu hili? Familia itasemaje? Jamii itanionaeje? ooooh sijui natakiwa kuvumilia...unavumilia nini? Ulioa/olewa ili uvumilie? Uvumilivu ndio umekuwa ndio msingi wa ndoa/mahusiano siku hizi? sio tena upendo wa dhati? ambao kama haupo hata kuvumilia kwenyewe hakuna maana yeyote...unavumilia nini sasa hapo? ili iweje?

  To be honest....mimi sio mfuasi wa uvumilivu kwenye ndoa/mahusiano...I believe in 'walking away', 'moving on' from a bad unhealthy relationship! Uvumilivu has never been healthy....
   
 11. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Umezungumza vizuri sana Kimbweka, sina cha kuongeza!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. l

  lasix JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  thank u Riwa unaonyesha ulikua kichwa kweli darasani.
   
Loading...