Ifahamu Ndege ya Pan american iliyopotea na kuonekana baada ya miaka 37 Abiria wake wakiwa hai

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
8,684
2,000
Moderator Hebu ondoeni hii kitu imekuwa kero sasa, watu hawafanyi searching now haina maana ya hicho kisehemu cha kutafuta aka searching.

Wengine tukiweka uzi unaofanana on spot mnauondoa haraka sana How?
 
Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
35,047
2,000
Haya maajabu nataman yangetokea hapa dege linaloenda china na Magufuli likapatE tokea kupotea hewan..alafu lirudi miaka 40 ijayo..kizaz chetu UJINGA kitakuwa kimeisha isha labda
 
Himidt Lengo

JF-Expert Member
Jan 4, 2018
244
250
Mungu anathibitisha ujiniazi Wa Prof.Albert Einstein (He lives on √ co R.I.P X) Wa kugundua Theory of relativity. Nadhani Mungu ataendelea kuthibitisha physics kwa kufanya Hiyo ndege itue tena kwa miaka ijayo abiria wake wakiwa na umri uleule hata km imepita miaka 50.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madame B

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
28,876
2,000
UZUSHI WA NDEGE YA PAN AMERICAN “FLIGHT” 914

Nimepata maswali mengi kuhusu ndege hii ya PAN AMERICAN 914 na nimeona kujibu mmoja mmoja ni ngumu ni bora nijibu kwa wote hata na wengine walioshindwa kuniuliza na wamesikia hili suala waweze nao kufaidika.

Kwanza naanza kwa kusema hii story ni ya uongo wa kiwango cha lami, mimi ni mpenzi sana wa story zenye utata na maajabu ndani yake na niliwahi zamani kidogo kukutana na hiki kisa cha kusadikika ambacho wengi wa waandishi wanaendelea kukisambaza kwa kutojua wanasambaza uongo uliotukuka.

Kabla sijaelezea uongo wa hiki kisa tuangalie story yenyewe ya kusadikika ilivyotengenezwa,

Mnamo mwaka 1992 mwezi mei tarehe 21 katika bara la AMERIKA KUSINI nchini VENEZUELA kulionekana ndege isiyotambulika baada ya mnara wa waongozeaji ndege kuinasa kupitia rada.

Hapo ilikuwa ni uwanja wa ndege wa CARACAS ila tu pale muungozaji wa ndege uwanjani hapo alipoanza kuwasiliana na rubani mkuu wa ndege ya PAN AMERICAN 914 ndege hiyo ikawa haionekani tena kwenye rada.

Muuongozaji wa ndege alishtuka kutoiona tena ndege hiyo ila bado rubani wake bado yuko hewani na wakaanza kuwasiliana,

MUONGOZAJI NDEGE: hapa ni VENEZUELA, wewe umetokea wapi?
RUBANI: Mungu! sisi ni shirika la ndege la PAN AMERICAN 914 tunatokea NEW YORK kwenda MIAMI, FLORIDA
MUONGOZAJI NDEGE: Imekuwaje mmekosea hivyo kwa kufika umbali wa zaidi ya kilomita 2000. “muongozaji ndege akaamua kuangalia kwenye diary ya ratiba zote za ndege na kuja kukuta hiyo ndege ya PAN AMERICAN 914 iliyokuwa ikitoka NEW YORK kwenda MIAMI iliruka tarehe 22 julai 1955.

Ina maana hapo ni zaidi ya miaka 37 imepita toka ndege hiyo iruke na muungozaji wa ndege alishtuka sana na kumjibu rubani wa ndege kuwa “ sidhani kama ni nyie ambao mnaniambia kuwa ndo nyie”.

Hapo hapo muongozaji ndege akawasiliana na mamlaka za usafiri wa anga NEW YORK na FLORIDA kuhusu ndege hiyo na wakaambiwa kweli ndege hiyo ilipaa tarehe 22 julai 1955 na haikufanikiwa kufika MIAMI.

Baada ya uchunguzi wa muda mrefu haikuonekana na kuhisi labda ilianguka baharini na kuzama, mungozaji wa ndege akarudi kwenye mawasiliano na rubani halafu akakuta ndege inaonekana tena kwenye rada na kuiruhusu itue uwanjani hapo

Ndege hii ilikuwa na abiria 50 ambao wote walikuwa hai pamoja na wafanyakazi wa ndege sasa cha kushangaza ni pale watu wote waliokuwemo ndani ya ndege wako vile vile yani hawajazeeka wakati ndugu zao waliowaacha wamezeeka [wamekuua].

Tusichanganye kitu, hapa Kuna aina mbili za story Kuna wengine wanasema ilitua na kutoweka tena Ila tuendelee na aina hii ambayo ndo imesambaa zaidi na iko kwenye chanzo halisi cha story hii.

Ndege yenyewe ni hii hapa
20190315_205336.jpg

TUENDELEE,

MAREKANI wakafanya taratibu za kuwarudisha nyumbani watu wake hao kutoka VENEZUELA na kubaki maswali magumu vichwani mwa wanasayansi kuwa iliwezakan vipi kuishi miaka 37 ndani ya ndege bila kula wala kunywa, ndege kupaa kwa miaka 37 bila mafuta, watu kutozeeka kubaki vilevile n.k

Na maswali hayo mpaka leo hii yameshindikana kujibiwa…??? Mwisho wa siku kisa hiki kinaangukia kwenye zile makala za ajabu na zilzoshindikana kutatuliwa [mystery unsolved cases].

Sawa tumeshaona kisa chenyewe, twende kwenye kujua uongo wa kisa hicho. CHA KWANZA ; kwa wasiojua chapisho la kwanza kuchapishwa kisa hiki lilikuwa gazeti maarufu la udaku na story za kusadikika liitwalo WEEKLY WORLD NEWS ni gazeti maarufu sana nchini MAREKANI kwa story za udaku na uongo.

Tuone kwa ufupi sana historia ya gazeti hili, WEEKLY WORLD NEWS ni gazeti la udaku na story za kufikirika lililoanzishwa mwaka 1974 na kuja kufa mwaka 2007, miaka yote hiyo ya kazi machapisho yake yote ni vituko vitupu tena vinakuwa ndo viko mbele ya gazeti.

Kuchapisha kwake vituko ila huwaambia kitu WAMAREKANI ni wanalipenda kuliko kawaida yani lilikuwa linauza balaa kama njugu kwasababu ya kuandika vitu vya kijinga ambavyo watu wanavifurahi kwa kuhisi ndo ukweli wenyewe

Sasa gazeti hili lilichapisha kisa hiki mara mbili tofauti, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1992 na mara ya pili ilikuwa mwaka 1993 katika machapisho haya kila kitu kimeandikwa vilevile ila tofauti ni huyu shuhuda wa hili tukio ambaye ndo yule muongozaji wa ndege wa CARACAS.

Kuna picha hapo chini zinaonesha gazeti hilo la WEEKLY WORLD NEWS kwa machapisho yake ya mwaka 1992 na 1993 na unaweza kuona picha ndogo katikati hapo ndo za hao mashuhuda wa kisa hiki kwa ya mwaka 1992 kuonekana picha ya shuhuda mwingie na ya mwaka 1993 picha nyingine kabisa.

Haya ndo madhaifu ya magazeti ya udaku kusahau vitu vidogo kama picha hizo na kwa kuwa tofauti kabisa, sasa fikiria gazeti la aina hii linalochapisha vituko ndo liliibua habari hii naamini waandishi wengi hawajui chanzo halisi cha kisa hichi ni wamekikuta mtandaoni na kukileta kwa jamii bila kukifanyia utafiti wa kutosha .

CHA PILI; turudi tarehe 22 mpaka 26 julai 1955 kuangalia magazeti ya kuaminika nchini MAREKANI na nimejaribu kuangalia magazeti makubwa na maarufu sana yanayosomwa zaidi Ambayo ni THE NEW YORK TIMES, THE WALL STREET JOURNAL, THE WASHINGTON POST na DAILY NEWS yenyewe hayana habari yoyote inayosema kuna ndege imepotea nchini MAREKANI ya kampuni ya PAN AMERICAN 914.

Nimeangalia magazeti haya kwa hizo siku tano [22 mpaka 26] mfululizo ili kama taarifa za kupotea kwa ndege hiyo zilichelewa kuwafikia vyombo vya habari basi nizione ila hakuna na yote hiyo ni kutaka kujihakikishia.

Twende tarehe iliyotajwa kuwa ndege hiyo ndo ilikuja kuonekana baada ya miaka 37 nchini VENEZUELA na nikarudi tena kwenye magazeti hayo maarufu nchini MAREIKANI na safari hii nikaliongeza na gazeti la USA TODAY kwasababu mwanzoni mwaka 1955 lilikuwa bado halijaanzishwa.

Nako katika magazeti haya hakuna habari hiyo kuwa kuna ndege ilipotea na kurudi baada ya miaka 37 na kwa ukubwa wa habari hii iliyojaa maajabu ya MUSA lazima ingeandikwa hata mwaka mzima sababu sio kitu cha kawaida kabisa ila gazeti letu pendwa la WEEKLY WORLD NEWS lenyewe habari hii unaikuta na ndo gazeti pekee lilioandika habari hii duniani.

CHA TATU: nikaenda kupitia tovuti rasmi na za kuaminika zinazoongelea masuala ya usafiri wa anga na baadhi ya hizo tovuti ni hizi, AVIATIONSAFETY,NET:1955, AVIATIONSAFETY.NET:1990, PANAMAIR.ORG-ACCIDENTS. ASN RECORDS OVER 80 AIRCRAFT MISSING SINCE 1948, PAN AMERICAN ACCIDENTS na zote haziongelei kabisa kuwa kuna ndege ya shirika la PAN AMERICAN 914 ilipotea mwaka 1955.

Ukifanikiwa kupitia vyanzo hivi vimeanisha ajali zote za ndege zilizowahi kutokea hata kama hizo ndege hazikupatikana mpaka leo hii na inaonesha idadi ya ndege zilizopata ajali mwaka huo [1955] ni ndege tisa tu duniani kati ya hizo ni mbili tu za taifa la MAREKANI na hakuna ndege ya PAN AMERICAN 914.

CHA NNE; nikaenda kwenye tovuti ya rasmi ya shirika la ndege la PAN AMERICAN inasema kuwa kampuni hii ya ndege ilianzishwa mwaka 1927 na kufilisika mwaka 1991 kwa samani zake kuuzwa kwa kampuni ya ndege ya DELTA.

Katika historia ya uendeshaji biashara ya ndege imeshawahi kupoteza ndege zake kwa ajali ila kwa mwaka 1955 hawakuwa na ndege yoyote ya kampuni yao iliyopata ajali ila miaka mwili mbele [1957] ndege yao moja ilipata ajali.

Ikabidi kwenye tovuti hiyo nitafute ndege aina ya PAN AMERICAN FLIGHT 914 ila hakuna ndege aina hiyo katika kampuni hii mpaka inakuja kufilisika na story hii imekuja baada ya kampuni hii kufilisika mwaka 1991.

Ina maana ndege PAN AMERICAN 914 ni ndege ya kufikirika na wenye kampuni hawaitambui nao wanaona mazingaombwe kwa kumilikishwa ndege wasiyoijua kuwa ni ya kwao.

CHA TANO; hakuna picha wala video iliyopigwa au kurekodiwa kuhusu ndege hiyo ilipoondoka mwaka 1955 au kuonekana tena nchini VENEZUELA nafikiri wote tunaifahamu kampuni ya GETTY IMAGE ambayo inahusika na uhifadhiziji wa picha na hawa hakuna picha ambayo hawana duniani kila picha wanayo ila ukienda kwenye tovuti yao ukataka picha za tukio hili hawana nao labda wewe ndo uwape na sijui utaitolea wapi.

Pia hakuna mahojiano yoyote yaliyorekodiwa duniani kuhusu hili tukio si kampuni ya PAN AMERICAN, marubai, wafanyakazi wa ndege wala abiria hakuna kabisa nafikiri kwa ukubwa wa hili tukio lazima mahojiano yangekuwepo ila hakuna

Hizo ni facts kuu tano amabazo nimekuandaliwa kujibu hilo swali kuhusu hicho kisa na zinaonesha kuwa story hii ni ya uongo wa kiwango cha lami na wala hakuna haja ya kujiuliza cjui hao watu walikula nini, walishiji ndani ya ndege, ndege iliwezaji kukaa huko ilipokuwepo bila mafuta, kwanini hao watu hawakuzeeka n.k

Ulikuwa ni uzushi toka kwenye gazeti ukaingia mtandaoni na kwa mujibu wa GOOGLE uzushi huu ulianza kusambaa mitandaoni (duniani) kuanzia mwaka 2008.

Kwa matazamo wangu nafikiri dhumuni kuu la uongo huu kuzushwa ni kutaka kuelezea jambo moja liitwalo “TIME TRAVEL” muda kusafiri maana hili suala limekuwa na mvutano baina ya wanasayansi kuwa “TIME TRAVEL” ipo au laa na wanasayansi kama ALBERT EINSTEN na NIKOLA TESLA wanaamini suala la “TIME TRAVEL”.

Nafikiri ni muda kwa waandishi kusoma vyanzo vingi kabla ya kuaandaa makala na inapohitajika kulipia kupata vyanzo vya uhakika kama vitabu ni kulipia tu ili kujiridhisha na wanachokiandika.

20190315_205731.jpg

Hizo picha hapo juu ndo matoleo ya magazeti ya mwaka 1992 na 1993 na unaweza kuona picha mbili tofauti katika magazeti hayo na kushindwa kujua yupi ndo JUAN DE LA CORTE maana kwenye machapisho yote limetumika hilo jina moja kwa picha mbili tofauti na ndo shuhuda mwenyewe ambaye ni muogozaji wa ndege kwa mujibu wa gazeti letu la udaku

Hizi picha zote chini ni front cover za magazeti ya WEEKLY WORLD NEWS unaweza kuona vituko vinavyopostiwa...!!!!
Picha zenyewe hizi hapa chini
20190315_204513.jpg
20190315_204459.jpg
20190315_204449.jpg
20190315_204422.jpg
20190315_204409.jpg
20190315_204358.jpg
20190315_204347.jpg
20190315_204337.jpg
20190315_204327.jpg
20190315_204316.jpg
20190315_204306.jpg
20190315_204255.jpg
20190315_204245.jpg
20190315_204232.jpg

20190315_210221.jpgImeandaliwa na COMRADE SABOUR.
INSTAGRAM :mad:ijuehistoria.
NO: 0679 95 93 08.
 
cabo

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
3,445
2,000
View attachment 1044618

Bado simanzi imetanda kufuatia ajali mbaya ya ndege ya Ethiopia Airlines, Flight ET302 iliyokuwa ikitoka Addis Ababa, Ethiopia kuelekea Nairobi, Kenya, kupata ajali na kusababisha vifo vya watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Ajali hiyo ya ndege, imewakumbusha wengi kuhusu majanga mbalimbali yaliyowahi kutokea kwenye usafiri wa anga yakizihusisha ndege mbalimbali, miongoni mwa matukio hayo, lipo tukio ambalo mpaka leo limeacha kitendawili kilichokosa majibu.

Ni tukio la ndege ya Shirika la Pan American, Flight 914 lililotokea mwaka 1955. Ndege hii, ilikuwa katika safari zake za kawaida, ikitokea New York, kwenda Miami, Florida nchini Marekani huku ndani yake ikiwa na abiria 57, wafanyakazi wanne na rubani.

Katika hali isiyo ya kawaida, ndege hiyo ilitoweka kwenye rada, muda mfupi baada ya kupaa angani. Juhudi za kuitafuta zilianza kufanyika mara moja lakini hakukuwa na taarifa zozote zilizopatikana ambazo zingesaidia kupatikana kwa ndege hiyo. View attachment 1044619

Saa zilikatika, zikawa siku, ikawa miezi na hatimaye ikawa miaka! Ndege ya Pan American haikupatikana, hakukuwa na mabaki wala kisanduku cheusi, wala hakukuwa na taarifa zozote zinazowahusu abiria waliokuwa ndani yake. Kwa lugha nyepesi, ‘iliyeyuka’!

Mei 21, 1992, ikiwa imepita miaka 37 tangu kupotea kwa ndege hiyo, wakati shughuli za kawaida zikiendelea katika Uwanja wa Ndege wa Caracas nchini Venezuela, jambo lisilo la kawaida lilitokea kwenye uwanja huo.

Kwanza, kulitokea mwingiliano wa mawimbi ya sauti katika chumba cha kuongozea ndege, mwongoza ndege Juan de la Corte anasimulia kwamba walipotazama vizuri, waligundua kwamba kuna ndege ilikuwa ikijiandaa kutua.

Haikuwa imeonekana kwenye rada za uwanjani hapo na mwingiliano wa sauti uliotokea, kumbe ilikuwa ni rubani wa ndege hiyo, akiwasiliana na chumba cha kuongozea ndege uwanjani hapo.

“Ndege ilikuwa imechakaa sana, rubani akawa anataka kutua bila hata kupata idhini ya kufanya hivyo, wakati tukiendelea kumdadisi ametoka wapi na ndege hiyo kwa sababu haikuwa kwenye ratiba, alitueleza kwamba anatoka New York na alikuwa akielekea Miami.

Kumbuka kwamba hapo ndege ilikuwa imefika Caracas, Venezuela, ikiwa imeenda umbali wa takribani kilometa 1,800 kutoka mahali alikotakiwa kutua. Kila mtu uwanjani hapo alipigwa na butwaa. View attachment 1044621

“Ilibidi tumsaidie kutua lakini ndani ya chumba cha marubani, kulisikika kama mabishano hivi, wakiwa wanaujadili uwanja kwamba umebadilika, siyo ule waliouzoea,” anasema Corte.

Kwa bahati nzuri, mahojiano hayo kati ya rubani akiwa ndani ya ndege na muongozaji wa ndege, yalirekodiwa, vinginevyo pengine ubishi ungekuwa mkubwa sana leo hii. Baada ya kutua, kwa mujibu wa mashuhuda, waliweza kumtambua rubani huyo kuwa ni yule aliyepotea na ndege angani! Abiria pia walikuwa ni walewale walioripotiwa kupotea na ndege hiyo.

Cha ajabu sasa, eti walikuwa wanaonekana vilevile baada ya miaka 37. Hakuna aliyezeeka au kubadilika chochote baada ya kipindi chote hicho. Ndani ya muda mfupi tu, watu wengi walikuwa wamekusanyika uwanjani hapo, kushuhudia maajabu hayo ya karne.

Baada ya kuona watu wanajaa, rubani aligeuka na kuwa mbogo, akawa anawataka watu wasiwasogelee kwani abiria wake walikuwa wamechoka na wanahitaji kupumzika, lakini watu walizidi kujaa, jambo lililomfanya aamue tena kuirusha ndege hiyo, akaondoka na abiria wake huku akiangusha kalenda ya mwaka 1955 uwanjani hapo na hawajapatikana tena mpaka leo.

Maswali yanayoendelea kusumbua vichwa vya wengi mpaka leo, ndege hiyo ilikuwa wapi kwa miaka yote hiyo? Ilikuwa ikiongeza wapi mafuta ya kuifanya iendelee kuwa angani? Zipo nadharia nyingi ambazo pia ni ngumu kuzithibisha kisayansi.

Wapo wanaoamini kwamba ndege hiyo ilitekwa na viumbe wa sayari nyingine na kutokomea nayo, wapo wanaoamini kwamba ndege hiyo iliingia kwenye mkondo uitwao ‘time elapse’ ambao inaaminika kwamba ndani ya mkondo huo, hakuna majira, kila kitu kinabaki jinsi kilivyo kwa miaka nenda rudi.

Hashpower7113
Aiseee hiii ni nzuri hii ya elapse time ningepata wa saa ningeendaga uko kabisa nikaishigi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
rip faza_nelly

JF-Expert Member
Feb 19, 2018
4,286
2,000
UZUSHI WA NDEGE YA PAN AMERICAN “FLIGHT” 914

Nimepata maswali mengi kuhusu ndege hii ya PAN AMERICAN 914 na nimeona kujibu mmoja mmoja ni ngumu ni bora nijibu kwa wote hata na wengine walioshindwa kuniuliza na wamesikia hili suala waweze nao kufaidika.

Kwanza naanza kwa kusema hii story ni ya uongo wa kiwango cha lami, mimi ni mpenzi sana wa story zenye utata na maajabu ndani yake na niliwahi zamani kidogo kukutana na hiki kisa cha kusadikika ambacho wengi wa waandishi wanaendelea kukisambaza kwa kutojua wanasambaza uongo uliotukuka.

Kabla sijaelezea uongo wa hiki kisa tuangalie story yenyewe ya kusadikika ilivyotengenezwa,

Mnamo mwaka 1992 mwezi mei tarehe 21 katika bara la AMERIKA KUSINI nchini VENEZUELA kulionekana ndege isiyotambulika baada ya mnara wa waongozeaji ndege kuinasa kupitia rada.

Hapo ilikuwa ni uwanja wa ndege wa CARACAS ila tu pale muungozaji wa ndege uwanjani hapo alipoanza kuwasiliana na rubani mkuu wa ndege ya PAN AMERICAN 914 ndege hiyo ikawa haionekani tena kwenye rada.

Muuongozaji wa ndege alishtuka kutoiona tena ndege hiyo ila bado rubani wake bado yuko hewani na wakaanza kuwasiliana,

MUONGOZAJI NDEGE: hapa ni VENEZUELA, wewe umetokea wapi?
RUBANI: Mungu! sisi ni shirika la ndege la PAN AMERICAN 914 tunatokea NEW YORK kwenda MIAMI, FLORIDA
MUONGOZAJI NDEGE: Imekuwaje mmekosea hivyo kwa kufika umbali wa zaidi ya kilomita 2000. “muongozaji ndege akaamua kuangalia kwenye diary ya ratiba zote za ndege na kuja kukuta hiyo ndege ya PAN AMERICAN 914 iliyokuwa ikitoka NEW YORK kwenda MIAMI iliruka tarehe 22 julai 1955.

Ina maana hapo ni zaidi ya miaka 37 imepita toka ndege hiyo iruke na muungozaji wa ndege alishtuka sana na kumjibu rubani wa ndege kuwa “ sidhani kama ni nyie ambao mnaniambia kuwa ndo nyie”.

Hapo hapo muongozaji ndege akawasiliana na mamlaka za usafiri wa anga NEW YORK na FLORIDA kuhusu ndege hiyo na wakaambiwa kweli ndege hiyo ilipaa tarehe 22 julai 1955 na haikufanikiwa kufika MIAMI.

Baada ya uchunguzi wa muda mrefu haikuonekana na kuhisi labda ilianguka baharini na kuzama, mungozaji wa ndege akarudi kwenye mawasiliano na rubani halafu akakuta ndege inaonekana tena kwenye rada na kuiruhusu itue uwanjani hapo

Ndege hii ilikuwa na abiria 50 ambao wote walikuwa hai pamoja na wafanyakazi wa ndege sasa cha kushangaza ni pale watu wote waliokuwemo ndani ya ndege wako vile vile yani hawajazeeka wakati ndugu zao waliowaacha wamezeeka [wamekuua].

Tusichanganye kitu, hapa Kuna aina mbili za story Kuna wengine wanasema ilitua na kutoweka tena Ila tuendelee na aina hii ambayo ndo imesambaa zaidi na iko kwenye chanzo halisi cha story hii.

Ndege yenyewe ni hii hapa
View attachment 1046409

TUENDELEE,

MAREKANI wakafanya taratibu za kuwarudisha nyumbani watu wake hao kutoka VENEZUELA na kubaki maswali magumu vichwani mwa wanasayansi kuwa iliwezakan vipi kuishi miaka 37 ndani ya ndege bila kula wala kunywa, ndege kupaa kwa miaka 37 bila mafuta, watu kutozeeka kubaki vilevile n.k

Na maswali hayo mpaka leo hii yameshindikana kujibiwa…??? Mwisho wa siku kisa hiki kinaangukia kwenye zile makala za ajabu na zilzoshindikana kutatuliwa [mystery unsolved cases].

Sawa tumeshaona kisa chenyewe, twende kwenye kujua uongo wa kisa hicho. CHA KWANZA ; kwa wasiojua chapisho la kwanza kuchapishwa kisa hiki lilikuwa gazeti maarufu la udaku na story za kusadikika liitwalo WEEKLY WORLD NEWS ni gazeti maarufu sana nchini MAREKANI kwa story za udaku na uongo.

Tuone kwa ufupi sana historia ya gazeti hili, WEEKLY WORLD NEWS ni gazeti la udaku na story za kufikirika lililoanzishwa mwaka 1974 na kuja kufa mwaka 2007, miaka yote hiyo ya kazi machapisho yake yote ni vituko vitupu tena vinakuwa ndo viko mbele ya gazeti.

Kuchapisha kwake vituko ila huwaambia kitu WAMAREKANI ni wanalipenda kuliko kawaida yani lilikuwa linauza balaa kama njugu kwasababu ya kuandika vitu vya kijinga ambavyo watu wanavifurahi kwa kuhisi ndo ukweli wenyewe

Sasa gazeti hili lilichapisha kisa hiki mara mbili tofauti, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1992 na mara ya pili ilikuwa mwaka 1993 katika machapisho haya kila kitu kimeandikwa vilevile ila tofauti ni huyu shuhuda wa hili tukio ambaye ndo yule muongozaji wa ndege wa CARACAS.

Kuna picha hapo chini zinaonesha gazeti hilo la WEEKLY WORLD NEWS kwa machapisho yake ya mwaka 1992 na 1993 na unaweza kuona picha ndogo katikati hapo ndo za hao mashuhuda wa kisa hiki kwa ya mwaka 1992 kuonekana picha ya shuhuda mwingie na ya mwaka 1993 picha nyingine kabisa.

Haya ndo madhaifu ya magazeti ya udaku kusahau vitu vidogo kama picha hizo na kwa kuwa tofauti kabisa, sasa fikiria gazeti la aina hii linalochapisha vituko ndo liliibua habari hii naamini waandishi wengi hawajui chanzo halisi cha kisa hichi ni wamekikuta mtandaoni na kukileta kwa jamii bila kukifanyia utafiti wa kutosha .

CHA PILI; turudi tarehe 22 mpaka 26 julai 1955 kuangalia magazeti ya kuaminika nchini MAREKANI na nimejaribu kuangalia magazeti makubwa na maarufu sana yanayosomwa zaidi Ambayo ni THE NEW YORK TIMES, THE WALL STREET JOURNAL, THE WASHINGTON POST na DAILY NEWS yenyewe hayana habari yoyote inayosema kuna ndege imepotea nchini MAREKANI ya kampuni ya PAN AMERICAN 914.

Nimeangalia magazeti haya kwa hizo siku tano [22 mpaka 26] mfululizo ili kama taarifa za kupotea kwa ndege hiyo zilichelewa kuwafikia vyombo vya habari basi nizione ila hakuna na yote hiyo ni kutaka kujihakikishia.

Twende tarehe iliyotajwa kuwa ndege hiyo ndo ilikuja kuonekana baada ya miaka 37 nchini VENEZUELA na nikarudi tena kwenye magazeti hayo maarufu nchini MAREIKANI na safari hii nikaliongeza na gazeti la USA TODAY kwasababu mwanzoni mwaka 1955 lilikuwa bado halijaanzishwa.

Nako katika magazeti haya hakuna habari hiyo kuwa kuna ndege ilipotea na kurudi baada ya miaka 37 na kwa ukubwa wa habari hii iliyojaa maajabu ya MUSA lazima ingeandikwa hata mwaka mzima sababu sio kitu cha kawaida kabisa ila gazeti letu pendwa la WEEKLY WORLD NEWS lenyewe habari hii unaikuta na ndo gazeti pekee lilioandika habari hii duniani.

CHA TATU: nikaenda kupitia tovuti rasmi na za kuaminika zinazoongelea masuala ya usafiri wa anga na baadhi ya hizo tovuti ni hizi, AVIATIONSAFETY,NET:1955, AVIATIONSAFETY.NET:1990, PANAMAIR.ORG-ACCIDENTS. ASN RECORDS OVER 80 AIRCRAFT MISSING SINCE 1948, PAN AMERICAN ACCIDENTS na zote haziongelei kabisa kuwa kuna ndege ya shirika la PAN AMERICAN 914 ilipotea mwaka 1955.

Ukifanikiwa kupitia vyanzo hivi vimeanisha ajali zote za ndege zilizowahi kutokea hata kama hizo ndege hazikupatikana mpaka leo hii na inaonesha idadi ya ndege zilizopata ajali mwaka huo [1955] ni ndege tisa tu duniani kati ya hizo ni mbili tu za taifa la MAREKANI na hakuna ndege ya PAN AMERICAN 914.

CHA NNE; nikaenda kwenye tovuti ya rasmi ya shirika la ndege la PAN AMERICAN inasema kuwa kampuni hii ya ndege ilianzishwa mwaka 1927 na kufilisika mwaka 1991 kwa samani zake kuuzwa kwa kampuni ya ndege ya DELTA.

Katika historia ya uendeshaji biashara ya ndege imeshawahi kupoteza ndege zake kwa ajali ila kwa mwaka 1955 hawakuwa na ndege yoyote ya kampuni yao iliyopata ajali ila miaka mwili mbele [1957] ndege yao moja ilipata ajali.

Ikabidi kwenye tovuti hiyo nitafute ndege aina ya PAN AMERICAN FLIGHT 914 ila hakuna ndege aina hiyo katika kampuni hii mpaka inakuja kufilisika na story hii imekuja baada ya kampuni hii kufilisika mwaka 1991.

Ina maana ndege PAN AMERICAN 914 ni ndege ya kufikirika na wenye kampuni hawaitambui nao wanaona mazingaombwe kwa kumilikishwa ndege wasiyoijua kuwa ni ya kwao.

CHA TANO; hakuna picha wala video iliyopigwa au kurekodiwa kuhusu ndege hiyo ilipoondoka mwaka 1955 au kuonekana tena nchini VENEZUELA nafikiri wote tunaifahamu kampuni ya GETTY IMAGE ambayo inahusika na uhifadhiziji wa picha na hawa hakuna picha ambayo hawana duniani kila picha wanayo ila ukienda kwenye tovuti yao ukataka picha za tukio hili hawana nao labda wewe ndo uwape na sijui utaitolea wapi.

Pia hakuna mahojiano yoyote yaliyorekodiwa duniani kuhusu hili tukio si kampuni ya PAN AMERICAN, marubai, wafanyakazi wa ndege wala abiria hakuna kabisa nafikiri kwa ukubwa wa hili tukio lazima mahojiano yangekuwepo ila hakuna

Hizo ni facts kuu tano amabazo nimekuandaliwa kujibu hilo swali kuhusu hicho kisa na zinaonesha kuwa story hii ni ya uongo wa kiwango cha lami na wala hakuna haja ya kujiuliza cjui hao watu walikula nini, walishiji ndani ya ndege, ndege iliwezaji kukaa huko ilipokuwepo bila mafuta, kwanini hao watu hawakuzeeka n.k

Ulikuwa ni uzushi toka kwenye gazeti ukaingia mtandaoni na kwa mujibu wa GOOGLE uzushi huu ulianza kusambaa mitandaoni (duniani) kuanzia mwaka 2008.

Kwa matazamo wangu nafikiri dhumuni kuu la uongo huu kuzushwa ni kutaka kuelezea jambo moja liitwalo “TIME TRAVEL” muda kusafiri maana hili suala limekuwa na mvutano baina ya wanasayansi kuwa “TIME TRAVEL” ipo au laa na wanasayansi kama ALBERT EINSTEN na NIKOLA TESLA wanaamini suala la “TIME TRAVEL”.

Nafikiri ni muda kwa waandishi kusoma vyanzo vingi kabla ya kuaandaa makala na inapohitajika kulipia kupata vyanzo vya uhakika kama vitabu ni kulipia tu ili kujiridhisha na wanachokiandika.

View attachment 1046412
Hizo picha hapo juu ndo matoleo ya magazeti ya mwaka 1992 na 1993 na unaweza kuona picha mbili tofauti katika magazeti hayo na kushindwa kujua yupi ndo JUAN DE LA CORTE maana kwenye machapisho yote limetumika hilo jina moja kwa picha mbili tofauti na ndo shuhuda mwenyewe ambaye ni muogozaji wa ndege kwa mujibu wa gazeti letu la udaku

Hizi picha zote chini ni front cover za magazeti ya WEEKLY WORLD NEWS unaweza kuona vituko vinavyopostiwa...!!!!
Picha zenyewe hizi hapa chini View attachment 1046387 View attachment 1046388 View attachment 1046390 View attachment 1046391 View attachment 1046392 View attachment 1046393 View attachment 1046394 View attachment 1046395 View attachment 1046396 View attachment 1046398 View attachment 1046400 View attachment 1046401 View attachment 1046403 View attachment 1046404

View attachment 1046413

Imeandaliwa na COMRADE SABOUR.
INSTAGRAM :mad:ijuehistoria.
NO: 0679 95 93 08.
Mkuu ielezee na 'PHILADELPHIA EXPERIMENT' nadhani habari zake utakuwa nazo...tujue kama na yenyew ni kweli au story tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom