Ifahamu nchi ya Switzerland (Uswisi) japo kwa machache

Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,504
2,179
Nikiwa bado kwenye msoto mkali wa lockdown JamiiForums imekuwa sehemu mojawapo ya kuniondoa upweke, asikuambie mtu ni kazi ngumu sana kukaa ndani masaa yote kwa mtu mwenye akili timamu.

Leo na-share na nyie japo kwa machache kuhusu hii nchi ninayoishi kwa sasa (Uswisi) ili kama kuna mtu anataka kuja huku apate kuijua japo kidogo. Uswisi ni mojawapo ya nchi nzuri sana katika ukanda huu wa ulaya usalama wa raia ni wa uhakika kiufupi ni nchi salama na yenye kiwango kidogo cha uhalifu, ni nchi yenye milima mingi na maziwa lakini isiyo na bahari na iliyojengwa vizuri na kwa ubunifu wa kipekee na mandhari ya kuvutia na watu wengi wa huku ni wakrsito na wasio na dini

Kuishi hapa nchini ni gharama kubwa sana kulingana na ughali wa maisha uliopo uzuri ni kwamba kampuni, mashirika na serikali wanalipa mishahara mikubwa na walimu ndio wanaongoza kulipwa vizuri na watu wa hii nchi wanapenda sana hisabati na physics na Ina wataalamu wengi wa sayansi na pia ukifanya kazi nchini humu utakuwa na option ya kukaa ama kuwa na makazi rasmi Ufaransa, Ujerumani, Italia au Austria kwa miundombinu iliyopo ya usafiri, watu wengi wanaishi kwenye hizi nchi na wanafanya kazi hapa. Hata mimi binafsi kipindi naanza kazi huku niliishi na mpenzi wangu Germany na asubuhi tulikuwa tunapanda treni kuja kazini Uswisi mpaka tulipotofautiana yeye akaenda kupanga Apartment Ufaransa Mimi nikarudi Geneva.

Kama nilivoelezea hapo juu hii ni nchi yenye utamaduni wa kitajiri na ili uishi huku unatakiwa uwe na hela ya kutosha, Lugha rasmi za mawasiliano zinatumika ni 3 Kijerumani, Kifaransa na Kiitaliano kwa asilimia kubwa lugha ya Kijerumani ndio imepewa hadhi maalum na lahaja ya watu wa huku wanayozungumza ni ya kijerumani na kwa asilimia kubwa ya raia wa huku huzungumza kiingereza vizuri sana na kama unajua Kiingereza vizuri hutapata tabu au Swissdeutsch.

Ndani ya hii nchi hamna ubaguzi na watu wake ni wakarimu sana kwa wale mabaharia kama mimi kazi yako ni kuopoa tu umpendae. Kwa wale wanaokuja kusoma kuna vyuo vingi na vyenye hadhi ya juu sana duniani na pamoja nakuwa na Gharama kubwa za maisha hapa nchini ada za vyuo ziko chini ukilinganisha na vyuo vingine ulaya na Duniani huku vikitoa elimu bora kabisa ada huanzia mpaka Euro1100 kwa mwaka kwa hapa nchini chuo kilicho na watu weusi wengi ni "Swiss Tropical Institute" kipo katika jimbo la Basel na pia Basel ni mji wenye watu wengi weusi na ukizaa mtoto huku ni sheria huruhusiwi kumpa jina lisilo na maana nzuri mfano MATATIZO au SIKUJUA. Na kitu cha kushangaza huku mbwa analipiwa kodi; gharama za kodi zinatofautiana kulingana na ukubwa/uzito wake na pia huruhusiwi kufuga mfugo mmoja unatakiwa ufuge jike na dume.

Kwa wahamiaji hasa kutoka Africa maisha ya hapa na tamaduni za wenyeji yanaweza kuwawia ugumu kwa siku za mwanzoni, maisha ni ya utulivu sana na kelele ni kosa kisheria linaloweza kufanya upelekwe mahakamani na kwa mtaani maisha kwa wahamiaji ni rahisi kama utakuwa na kazi ya kukuingizia kipato na ni magumu Kama hutakuwa na kazi ya kueleweka, zipo kazi zisizohitaji ujuzi na zinazohitaji ujuzi japokuwa ni rahisi kwa wenye ujuzi kuweza kupata kazi kuliko asiye na ujuzi na hii haimaanishi asiye na ujuzi hawezi kupata kazi anaweza na inaweza kuwa rahisi kwake pia kutegemeana na watu wa uenyeji wake.

Ukiwa hapa Uswisi unahitaji angalau CFH 9000+ ili uweze kuishi maisha ya kawaida kulingana na ughali wa mahitaji Kama vyakula, nyumba,vinywaji na mengineyo ingawa Kuna watu wanaishi chini ya kiwango hicho cha fedha na miasha huwa ni magumu mno na ni vigumu kukuta mtu asiye na kazi rasmi akilipwa chini ya CFC 43 kwa saa ambayo ni Kama $44 kwa saa pia hulipwa pesa ya nyumba na usafiri malipo haya pia huhusisha wafanyakazi wa viwandani ambao ni vibarua wanaolipwa kwa siku, wafanyakazi wa mashambani japo kuna wanaolipwa zaidi ya hapo kwa vile suala la mishahara ni Open -Market kwa hapa nchini, wafanyakazi wanaofanya kwenye nyumba za kutunzia wazee na walemavu hulipwa vizuri zaidi.

Uswisi sio nchi nzuri kwa wale wanaoanza kutafuta maisha wasiokuwa na wenyeji ama pesa ya kujikimu kwa kipindi chote watakachokuwa wanatafuta uenyeji na kazi ya kuwaingizia kipato ili kuendesha maisha yao

Kwa expert mwenye ujuzi wanalipa vizuri sana, wanalipa mishahara minono mno na fani ambazo ziko in-demand katika soko la ajira hapa Uswisi ambazo kupata kazi ni rahisi ukiwa na utaalam wa kutosha ni.
IT and Telecommunication hawa soko lao ni kubwa sana kwa mtu aliye vizuri.
Fani zote za engineer
Technician walio skilled
Fani za afya (madaktari, famasia, nesi n.k) na
Wabunifu wa majengo kwa wageni walio na fani hizi na wamebahatika kupata kazi huku hawajutii kabisa.

Kwa wale wapenda starehe kama mimi na watu wa night-Club Zurich ndio baba lao kwa Night-life hapa nchini, hili jiji la Zurich limepakana kwa karibu sana na Ujerumani na ni jiji ghali kuliko majiji mengine na pia ndilo jiji kuu la kibiashara nchini Uswisi hapa utakutana na Clubs ambazo hujawahi kuziona ukanda wote wa Africa mashariki Kama Club Zurich humu ndani ya hii Club kila kitu ni VIP imepakana kwa karibu na Kaufleuten kuna Hive, Mascotte, Zukunft, Aura na Gonzo ambayo ni underground karibu na pwani ya ziwa ni bonge moja la Club chini ya ardhi ambayo hutojuta kuingia.

Lakini hiyo haimanishi majiji mengine hayana Club nzuri hapa GENEVA ninapoishi kuna The Baraque Club, Five Night Club, Java Club, Mambo Club na nyingine nyingi sana ni zaidi ya bata kwa wanaopenda kujiachia na huko jimbo la Basel nako kuna Sandoasa Club, Club59, 8bar, Barock Club, The Pub, The Lab, L39 na nyingine nyingi.

Kwa wanaowataka kufanya biashara uje ukijua mfuko wako uko vizuri kweli kweli pamoja na kwamba mabenki ya huku ni salama, yana faragha ya hali ya juu na nafuu sana.

Parabora
Geneva - Switzerland

Chukua hatua stahiki za kujilinda, Corona ipo na ni hatari
 
Chanel za kuja huko vipi
2. Fare kiasi gani mpaka huko
3. Kazi za kibaharia kama uhouse boy, kukata nyasi, kifua kupiga deli na kuogesha vizee vya kizungu zipo na zinapatiakana? Maana sisi wa Mwananyamala kwa Ally Maua na Manzese Midizini ndio kazi zetu.

4. Totoz za huko zinalipa? Kali au ndio kama wakorea tu wamepooza.

Jibu hayo kwanza ulete mwangaza kwa mabaharia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanel za kuja huko vipi
2. Fare kiasi gani mpaka huko
3. Kazi za kibaharia kama uhouse boy, kukata nyasi, kifua kupiga deli na kuogesha vizee vya kizungu zipo na zinapatiakana? Maana sisi wa Mwananyamala kwa Ally Maua na Manzese Midizini ndo kazi zetu.

4. Totoz za huko zinalipa? Kali au ndo kama wakorea tu wamepooza.

Jibu hayo kwanza ulete mwangaza kwa mabaharia.
Kama utaingia kihalali na documents zote kazi unaweza kupata, watoto wapo mkuu ni wakali lakini lazma ujue kwamba wana maisha ya utajiri kwa asilimia kubwa
 
Back
Top Bottom