Sep 25, 2018
27
20
Moja ya matunda yaliyoonekana ni ya kiswahili na tumekuwa nayo na kuishi nayo katika jamii yetu ni matunda haya mawili kutoka katika miti tajwa hapo juu.

Japo inatokea katika familia moja ya Annonacea ila kwa kiiingereza hili kundi la miti jamii hii huitwa Custard Apple trees.

Tuchambue pamoja kuanzia na topetope kisha stafeli.

1.TOPETOPE
Ni tunda linalotokana na mti wa mtopetope au mtomoko, kibotani (elimu ya mimea) linaitwa Annona squamosa, katika ngazi ya familia ya mimea jamii ya Annonaceae na ni moja ya familia kubwa ya miti iliyopo katika nchi za kitropiki kwa hii yenye matunda inakuwa na tunda lenye mbegu zilizotawanyika katika tunda moja wapo mfano topetope na hii munaoufahamu mutanikubalia. Kwa lugha ya malkia linaitwa Sweetsop. Moja ya matunda na miti maarufu katika nchi za kitropiki (Nchi zinazozunguka ikweta au almaarufu kwa kuwa ni nchi zinazopigwa na jua moja kwa moja)


UNATOFAUTISHAJE TOPETOPE NA STAFELI?
Kuna wengi wameshindwa na wanashindwa kutofautisha hapa kuanzia tunda,majani na mti;

A) TUNDA
Topetope lina tunda dogo size ya ngumi la binadamu na kama litazidi hapo ni aina tu hasa haya ya kigeni kutokea sehemu za ubaridi.

Ganda la tunda linakuwa na rangi ya kijani isiyoiva na linakuwa na miinukomiinuko kama makunyanzi na ndani ni jeupe a tofauti na stafeli halina muonekano huu.

B) MAJANI
Topetope huwa na majani madogo kwa muonekano na rangi ni kijani tu yenye mnga'o wa kati,malaini sana endapo utayagusa.

Sifa ya majani ya topetope ni kuwa na sumu kali kwa wadudu kama mbu

C) MITI
Mti wa mtopetope huwa na urefu wa Mita 3 mpaka 7 na shina lake ni jembamba.

2. STAFELI
Ni tunda linalotokana na mti wa msatafeli,kw kiingereza linaitwa ni Soursop,familia yake ni Annonaceae kama ilivyo kwa topetope tu.Licha ya kufanana na topetope ni nini utofauti wake?

A) TUNDA
Tunda lake ni kubwa kwa kufananisha na topetope,lina miiba miiba kwa nje na rangi yake ni kijani kabisa (deep colour).

Sifa ya tunda lake ni kutooa juice nzuri sana na wengi wanafahamu bidhaa pasi kujua tunda lake na mti.

B) MAJANI
Majani yake ni ya kijani kabisa na ni mapana kwa ukubwa,mara nyingi sio rahisi kuona mistari ya kusafirishia chakula na maji kwa chini kama ilivyo kwa topetope kutokana na rangi ilivyoiva.

C) MITI
Miti yake ni mirefu kuanzia Mita 3 hadi 10 na ina kivuli kipana kuliko topetope.

KWANINI UPANDE HII MITI?

Suala la afya na matatizo la kiafya yamekuwa ni ujumbe wa kila dakika katika stations za radio na Televisions. Kwa kuwa wengi wametoka katika njia kuu na kuingia njia yenye majuto kwa kuacha kutumia vitu vya asilia.

Hapa chini ni faida ya miti, majani na matunda yake kwa kila mti wa tunda

a)Topetope, miti yake ni mizuri katika kuhifadhi mazingira hasa maeneo ya karibu na majumbani na kikubwa kutokana na ukubwa wa mti wenyewe (Mita 3 hadi 7) pia inaweza kuwa miti ya kuzuia upepo katika maeneo ya majumbani na hata kuzunguka mashamba yetu pia.

Majani yake ni sumu ya kufukuzia Mbu na inawaua hasa katika hatua ya viluwiluwi.

Mizizi na magome yake ni dawa ya magonjwa mbalimbali nadhani hapa wengi tutatofautiana kutokana namaeneo na malezi pia.

Tunda lake ni zuri kwa kuwa linatoa juice yenye ladha tamu yenye kubeba nguvu za tiba kwa kuwa ndani yake kuna;

- 56.3mg ya Vitamin C nadhani wengi wameilewa Vitamin C kutokana na kipindi hiki tulichonacho cha Covid-19

- Fiber content au nyuzinyuzi kwa 6.8g ambayo ni 18% ya kambakamba anazohitaji mtu nzima katika afya ya mwili,fiber zinasaidia kudhibiti cholestrol mwilini na kiwango cha sukari mwilini.

- Nishati kwa kuwa kuna 25g za Carbohydrate au wanga katika tunda hili hivyo ni chanzo kizuri cha nguvu mwilini.

- Antioxidant kwa hivyo inatibu na inalinda mwili kutokana na changamoto mbalimbali.

- Utabibu kwa jamii za watu wa mataifa mengi hasa India wanatumia kwa vidonda vya tumbo na kumeng'enya vyakula kwa wenye matatizo.

Mbegu zake zina sumu kali na inashauriwa kabla haujatumia zipitie hatua kadhaa za kiutabibu,nazo zinatoa mafuta mazuri ya kupikia na pia zinatumika kutengenezea manukato mbalimbali (Perfumes)

b) Stafeli kutokana na umbo la mti wake unaweza kutumika kama kivuli, windbreak na kitunza mazingira kwa maeneo ya mijini.

Mizizi na magome yanatumika kutibu vidonda na pia magonjwa ya tumbo.

Tunda lake linatoa juice nzuri na yenye kuvutia ila yenye kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali ya kisukali na pressure.

WAPI NAWEZA PANDA MITI HII TANZANIA?

Sehemu kubwa ya nchi yetu unaweza kupanda aidha kibiashara au matumizi ya nyumbani.

1.Udongo
Udongo ambao hautuhamishi maji, usio na chumvichumvi japo inavumilia sana. Udongo kichanga, tifutifu, tifutifu kichanga na tifutifu mfinyanzi unafaa sana kwa kulima miti hii, hali ya udongo (pH) yake ni 5.6 hadi 7.3 inafanya vizuri tu.

2.Mwinuko toka usawa wa bahari
Kuanzia Mita 0 hadi 2100 miti hii inafanya vizuri pasipo kubagua wala kuleta madhara katika ukuaji wake wala uvunaji wake.

3.Joto
Hapa kuna uwanda mpana kuanzia sentigredi 15 mpaka 27, chini ya joto la sentigredi 13 ukuaji hudumaa na kudumaza mti hivyo ukuaji wake utachukua muda mrefu,juu ya sentigredi 35 hatua ya maua inaweza kupunguzwa hii inaitwa ABORTION na hutokea kwa miti mingi inavyopambana na kujibu hali ya nje katika uchavushaji wake (POLLEN TRANSFER IN POLLINATION).

4.Maji na Mvua
Hapa maeneo yenye ukame wala hakuna shida linavumilia maana kwa maeneo yanayopokea mvua chini ya milimita 750 kwa mwaka yanastawi na kuvumilia nyakati kame. mwagiliaji unaweza kufanyika wa kumwagilia kwa ndoo (wastani wa ndoo ya liya 10 kila baada ya siku 2) au drip ni kutokana na kiwango cha uzalishaji unachokitaka wewe tu.

KWANINI WENGI HATUJAFIKIA KUZALISHA KIBIASHARA?
Jamii ya Tanzania tumekosa soko katika bidhaa za kilimo ila kingine ni uthubutu wa kuangalia mbadala. Maana shida sio kuuza tunda ila je,tumewahi kuthubutu kuuza kilichopo katika matunda au miti hii? wa sababu hii wenzetu kenya wameshakimbilia fursa ya kilimo cha matunda haya na wameshacheza na soko la kimataifa (EXPORTATION) sasa kazi kwetu na kuamua japo ni safari isiyohitaji wiki au mwezi ila kilimo chake ni kirahisi na kisichohitaji gharama sana.

CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA KILIMO HIKI NI ZIPI?
1. Wadudu wanyonyao sukari za kwenye matunda na majani (SUCKERS INSECTS) hasa nziweupe (Whiteflies), utitiri (mites), vidung'ata (mearlybugs),vidugamba weupe (scales) ambao huharibu ubora wa tunda na kushusha uzalishaji na hili ndilo tatizo la wazalishaji na wakulima wengi wa haya mazao,soko la matunda na bidhaa yake lipo wazi ni wewe na maamuzi yako.

Mwandishi anapatikana mkoani Morogoro, maeneo ya SUA, ni Mkulima na mshauri/mtaalamu wa masuala ya kilimo cha bustani, mifumo ya mashine na udhibiti wadudu waharibifu wa mazao.
t1.jpg
topetope 3.jpg
tope.jpg
STAFELI 2.jpg
STAFELI 3.jpg
STAFELI.jpg
 
Kuna tunda flani halina miiba lipo smooth nje, hilo ndio nalifahamu kama topetope.
Sijui nielezeje zaidi, kama umeelewa naomba unieleweshe zaidi mkuu.
 
Kuna tunda flani halina miiba lipo smooth nje, hilo ndio nalifahamu kama topetope.
Sijui nielezeje zaidi, kama umeelewa naomba unieleweshe zaidi mkuu.
Hata mimi nalifahamu hivyo, ngoja nitamwambia Dogo anipigie picha mti wake, majani yake na tunda lenyewe alafu nitalituma hapa tujue kuwa ni aina gani la topetope? Pia ni kubwa tofauti na hivyo vidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani hayo mastafeli nimeotesha mengi Ila yanashambuliwa Sana na wadudu na matunda yanaoza hovyo Sana sijui nitumie dawa gani ,binafisi nayapenda sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom