Ifahamu misingi ya utoaji haki

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1611224273325.png
Kwa kuzingatia utawala bora vyombo vinavyohusika na kutoa haki kama vile mahakama, mabaraza yenye asili ya mahakama, kamati za nidhamu na vyombo vingine vinavyofanya kazi zenye asili ya kimahakama vinapaswa kufuata misingi ya kutoa haki kama vile:-

• Kuzingatia Katiba na sheria za nchi;

• Kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii au
kiuchumi;

• Kutochelewesha haki bila sababu ya msingi;

• Kutoa fidia stahiki kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa
ya watu wengine;

• Kukuza na kuendeleza usuluhishi baina ya wanaohusika katika
migogoro;

• Kutenda haki bila kufungwa kupita kiasi na masharti ya kiufundi
yanayoweza kukwamisha haki kutendeka; na

• Kuzingatia kanuni za haki ya asili (natural justice).
 
Naombeni msaada niende kulalamikia wapi?
Nimepanga nyumba leo ni miaka 15
Nalipa kodi vizuri tu hatuna deni
Leo mwenye nyumba anasema nakupa siku tatu uhame. Hakuna notisi wala nini hivi ni haki kweli
Nyumba yenyewe nimeiremba kweli
 
Naombeni msaada niende kulalamikia wapi?
Nimepanga nyumba leo ni miaka 15
Nalipa kodi vizuri tu hatuna deni
Leo mwenye nyumba anasema nakupa siku tatu uhame. Hakuna notisi wala nini hivi ni haki kweli
Nyumba yenyewe nimeiremba kweli

Unalemba nyumba utafikiri yako mwenye nyumba kashakwambia uhame unataka ukashitaki kwa sababu gani? Au unataka umpole mali yake kwa nguvu? Lemba mali yako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom