Ifahamu milango minne ya kuingia katika mahusiano na sababu za kuvunjika au kufanikiwa kwa mahusiano hayo!

Heaven Seeker

JF-Expert Member
May 12, 2017
478
1,047
Amani kwenu Wakuu.

Elimu ya mahusiano ni kubwa na watu wengi wamekuwa wakielezea mambo kadha wa kadha, kwa upande wangu naomba kujikita katika muktadha tofauti kidogo kwa namna yake japo kwa ujumla wake mambo yanaweza kuwa yaleyale kama ambavyo huelezwa na watu wengine.

Bila shaka utakubaliana nami kuwa masuala ya mahusiano ni miongoni mwa mambo yanayochukuwa sehemu kubwa katika maisha yetu. Kwa mantiki hiyo, siku ya leo nimefanya uchambuzi mfupi wa milango mikuu minne inayotumika kwa kiasi kikubwa kuingia kwenye mahusiano, na sababu zinazoweza kupelekea mahuasiano hayo kuvunjika. Karibu ufuatane nami, hopefully utajifunza jambo.

1. Kijana akiwa katika hali ya kupevuka kimaumbile, lakini mdogo kifikra.

Huu ni wakati ambao kijana anakuwa katik aumri mdogo. Wakati huu ni pale ambapo kijana anaweza akawa bado katika safari ya masomo yake hasa hasa sekondari. Kutokana na mihemuko inayotokana na mabadiliko ya kimwili, wakati huu humpelekea kijana kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi. Ikiwa ni kijana wa kike inaweza kupeleka kuwa mjaumzito bila kujiandaa kuwa katika hali hiyo. Kutokana na influence za familia ama jamii inayomzunguka, vijana hawa wanaweza kuanza mahusiano ya ndoa moja kwa moja. Ndoa hii ina asilimia kubwa ya kuvunjika kwa hapo baadae kwakuwa matokeo ya mahusiano hayo hayakuwa katika hali ya kuridhia moja kwa moja tangia mwanzo. Hata hivyo, mahuasiano haya yanaweza kuwa endelevu endapo wenza hawa watafanya bidii za kupata elimu ya mahusiano ya ndoa na maisha kwa ujumla.

2. Mahusiano wakati wa maisha kijana anapokuwa chuoni.
Hiki ni kipindi ambacho vijana wengi hasa wanaokuwa katika mazingira ya vyuoni hukutana na kuanzisha mahusiano. Pamoja na sababu nyingine, sababu kuu zinazoweza kupelekea kuanzishwa kwa mahusiano kipindi hiki ni influence ya mazingira anayokuwa nayo ´kijana, hali ya uhuru wa kujitegemea kimaisha, starehe na kupata kampani (companionship). Uchunguzi wangu usio rasmi unaonesha kuwa angalau katika mahusiano ya watu 10 ambayo huanzishwa kipindi hiki, ni wastani wa mtu mmoja pekee katika hao 10 huweza kuwa na mahusiano yaliyo endelevu hapo baadae. Hii inatokana na kuwa sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa mahisiano hayo hazikuwa genuine, bali ilikuwa ni influence ya hali flani aliyokuwa nayo mtu. Kukitokea dhoruba za maisha hapo baadae mahusiano haya huwa ni rahisi kuvunjika.

3. Mahusiano baada ya maisha ya vyuoni kabla ya ajira ama shughuli ya kujiingizia kipato.
Hiki ni kipindi ambacho msichana ama mvulana anakuwa katika hali ya kutafuta ajira ama mtaji ili apate kazi yoyote itakayomuingizia kipato. Kutokana na sababu za ukata na kutamani maisha mazuri, kipindi hiki kijana anaweza kushawishika kirahisi kuanzisha mahusiano ili aweze kukidhi mahitaji yake ya msingi na yale ya ziada. Mahuaisno mengi ya kipindi hiki hayawezi kuendelea kwa sababu, sababu zilizopelekea kuanzishwa kwake hazikuwa genuine pia, bali ni ushawishi wa kutaka unafuu kimaisha.

4. Mahusiano wakati wa ajira ama kijana akiwa ameanza kujipatia kipato chake kwa kujiajiri.
Kwa kiasi kikubwa, kipindi hiki vijana wengi huanzisha mahusiano kwa nia ya dhati ili mtu aweze kumpata mwenza wake katika maisha. Mahusiano ya kipindi hiki yana chance kubwa ya kufanikiwa maana kila mtu anakuwa amekomaa kifikra na kujifunza mambo mengi kuhusu maisha. Japo kuwa hakuna guarantee ya mahusiano haya kuwa ni lazima yafanikiwe, ila uwezekano wa kudumu kwa mahusiano hayo kwa kipindi hiki ni kwa kiasi kinachoweza kuwa kikubwa zaidi.

Hivyo basi, ni jukumu la kila kijana kujifanyia tathmini na kujiuliza ni mlango upi katika milango hiyo hapo juu ulitumika kwake kuingia katika mahusiano aliyonayo. Kama unadhani mlango ulioutumia ama uliopo una chance ndogo kwa mahusiano hayo kuwa endelevu, unayo nafasi ya kuchukuwa hatua za maksudi ili kufanya maamuzi sahihi. Japokuwa maisha hayana kanuni moja pekee iliyo sahihi siku zote, ila uhalisia utabaki kuwa uhalisia.

Kwakuwa watu wengi hawapendi kusoma maelezo marefu, naomba kuishia hapa kwa leo na naweza kuendelea kuandika kulingana na mjadala utakavyokuwa ukiendelea. Ni matumaini yangu kuwa umepata jambo la kujifunza.
 
sawa tumekupata vyema mkuu
 
Back
Top Bottom