Ifahamu Kozi ya Sayansi Afya ya Mazingira(Environmental Health Sciences)

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
18,963
35,577
Habari JF members.
Natumai nyote mu wazima wa afya,Mimi si mwandishi mzuri sana ila nitajitahidi kuelezea kile nachokifahamu.
Hivyo nipende kwenda moja kwa moja kuelezea kuhusiana na moja ya kozi muhimu katika masuala ya afya.

Kozi hii imeanza miaka mingi sehemu mbalimbali Duniani.
Na hapa Tanzania ilianza kwa lengo maalumu la kuthibiti magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na uchafu wa mazingira husika ya mahali..mfano ugonjwa wa kipindupindu kutokana na uchafuzi wa maji n.k

Mwanzoni hii kozi ilitolewa kwa ngazi ya cheti na stashahada na miongoni mwa vyuo vilivyotoa kozi hii ni Ngudu,Kagemu,Mpwapwa,Muheza,Muhimbili na Tanga ambapo mpaka leo hii vyuo hivyo bado vinaendelea kutoa kozi hii.Ni kozi ya miaka mitatu kwa ngazi ya stashahada na miaka miwili kwa ngazi ya astashahada.

Kwa ngazi ya shahada kozi hii inatolewa katika vyuo vikuu vya MUHAS,SUZA na RUCU.Vyuo hivi ndivyo vinavyotoa kozi hii kwa hapa nchini,ni kozi ya miaka mitatu kwa upande wa shahada ya kwanza.

Muhitimu wa kozi hii anafahamika kama Afisa afya Mazingira au kama lilivyo jina kongwe na linalofahamika anaitwa Bwana au Bibi afya..hawa hufanya kazi mbalimbali kuanzia ngazi ya mtaa/kitongoji hadi taifa(Wizara) na taasisi mbalimbali za umma ama sekta binafsi.

Kazi kuu yao kuu ni kulinda jamii dhidi ya magonjwa yote ya kuambukiza na yasiyo yakuambukiza..yatokanayo na hali chafu au mazingira mabovu ambayo husababisha madhara ya kiafya kwa mtu mmoja ama jamii kwa ujumla.

Hutekeleza dhima hiyo kuu kwa kuhamasiha usafi..ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo ya vyakula,ujenzi wa vyoo bora,usimamizi wa chanjo,utunzaji wa vyanzo vya maji,utunzaji wa mazingira na mengine mengi kulingana na eneo husika.

Maafisa afya husimamia na kutekeleza sheria ya Afya ya jamii ya mwaka 2009 (PHA2009).

Upande wa ajira kozi ina mpa nafasi mhitimu kujiajiri na kuajiriwa katika sekta mbalimbali ya umma na za binafsi.

Karibuni kwa nyongeza,ushauri au maswali..ili kuwasaidia vijana wetu katika kuchagua kozi nzuri hasa kipindi hiki wakijiandaa na elimu ya juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa upande wa masters hiyo course naweza ipata nimesoma geography University au lazima uweumesoma science.asante
Kwa vyuo vikuu Tanzania hakuna vyuo vinavyotoa masters ya EHS ila kwa vyuo vya nje unaweza ipata.
Wahitimu wengi wa BSCEHS huwa wanasoma MPH,Msc Occupational health and safety na zinginezo kulingana na hitaji la mtu.

Kimsingi hata Environmental health Sciences inakupa uwanda mpana sana wa kusoma kozi nyingi katika levo ya masters.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari JF members.
Natumai nyote mu wazima wa afya,Mimi si mwandishi mzuri sana ila nitajitahidi kuelezea kile nachokifahamu.
Hivyo nipende kwenda moja kwa moja kuelezea kuhusiana na moja ya kozi muhimu katika masuala ya afya.

Kozi hii imeanza miaka mingi sehemu mbalimbali Duniani.
Na hapa Tanzania ilianza kwa lengo maalumu la kuthibiti magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na uchafu wa mazingira husika ya mahali..mfano ugonjwa wa kipindupindu kutokana na uchafuzi wa maji n.k

Mwanzoni hii kozi ilitolewa kwa ngazi ya cheti na stashahada na miongoni mwa vyuo vilivyotoa kozi hii ni Ngudu,Kagemu,Mpwapwa,Muheza,Muhimbili na Tanga ambapo mpaka leo hii vyuo hivyo bado vinaendelea kutoa kozi hii.Ni kozi ya miaka mitatu kwa ngazi ya stashahada na miaka miwili kwa ngazi ya astashahada.

Kwa ngazi ya shahada kozi hii inatolewa katika vyuo vikuu vya MUHAS,SUZA na RUCU.Vyuo hivi ndivyo vinavyotoa kozi hii kwa hapa nchini,ni kozi ya miaka mitatu kwa upande wa shahada ya kwanza.

Muhitimu wa kozi hii anafahamika kama Afisa afya Mazingira au kama lilivyo jina kongwe na linalofahamika anaitwa Bwana au Bibi afya..hawa hufanya kazi mbalimbali kuanzia ngazi ya mtaa/kitongoji hadi taifa(Wizara) na taasisi mbalimbali za umma ama sekta binafsi.

Kazi kuu yao kuu ni kulinda jamii dhidi ya magonjwa yote ya kuambukiza na yasiyo yakuambukiza..yatokanayo na hali chafu au mazingira mabovu ambayo husababisha madhara ya kiafya kwa mtu mmoja ama jamii kwa ujumla.

Hutekeleza dhima hiyo kuu kwa kuhamasiha usafi..ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo ya vyakula,ujenzi wa vyoo bora,usimamizi wa chanjo,utunzaji wa vyanzo vya maji,utunzaji wa mazingira na mengine mengi kulingana na eneo husika.

Maafisa afya husimamia na kutekeleza sheria ya Afya ya jamii ya mwaka 2009 (PHA2009).

Upande wa ajira kozi ina mpa nafasi mhitimu kujiajiri na kuajiriwa katika sekta mbalimbali ya umma na za binafsi.

Karibuni kwa nyongeza,ushauri au maswali..ili kuwasaidia vijana wetu katika kuchagua kozi nzuri hasa kipindi hiki wakijiandaa na elimu ya juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hello!Hii kozi inautofauti gani na BSc. Environmental Science and management
 
Hii kozi imejikita zaidi upande wa afya..ni preventive medicine...utofauti wake hii imejikita zaidi katika ulizi wa afya kwa kuzuia na kulinda afya ya jamii dhidi ya magonjwa yatokanayo ama yasababishwayo na sababu za mazingira yanayomzunguka mtu ama jamii husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ESM ( Environmental science and management) inajikita zaidi ktk physical science, hii nyingine imejikita zaidi kwenye biological sciences

Lakini wanaweza fanyakazi pamoja Hawa wote, environmental officer sehem mbalimbali
Unaweza hama kada na ukahamia mazingira? Kwa halmashauri majukumu papi wanafanya watu wa mazingira?
 
Inawezekana sana bila shida,mana mwanafunzi wa ehs anasoma env polution and managment,env impact ass,env chemist& physcis,waste managment,indoor and outdoor air pollution.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom