Ifahamu kimchi kutokea South Korea

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Mara ya kwanza naonja Kimchi ilikuwa kwenye hafla fulani huko Jijini Dar es Salaam. Nillikuwa na shauku sana kuonja menu ambayo naiona tu kwenye series.

Of course nilijua kitakuwa ni chakula chenye ladha ya tofauti but sikutegemea kama itakuwa na ladha ya spicy kiasi kile. Lakini yeah nilienjoy!

Kimchi kwa wakorea ni kama Ugali kwa Watanzania, Burger au Hot dog kwa wamarekani yaaani ni chakula cha taifa na mara nyingi huliwa kama Side Dish pembeni kukiwa na wali au bokoboko, kama umeangalia Korean Dramas nyingi utakuwa umeshaelewa ninachokiongelea.

Wanahistoria wanasema kuwa Kimchi ilikuwepo tangu kipindi cha himaya ya Silla 57 BC - AD 935 na hata kipindi cha Goryeo Kimchi ilikuwepo pia maana kulikuwa na mashairi kama lile la Yi Yugbo yalikuwa yanaelezea pishi hilo.

. KIMCHI NI NINI?

Kimchi ni chakula maarufu sana huko South Korea na inategenezwa na kabichi pamoja na Raddish (sijui kiswahili chake) kisha baadaye huongezewa viungo mbalimbali ambavyo hunogesha pishi hilo.

Sasa hapo kwenye Cabbage achana na hizi cabbage za kibongo ambazo tunalia na ugali. Kimchi hutengenezwa na aina cabbage inayoitwa NAPA Cabbage ambayo ina utofauti na hizi cabbage za kawaida. Nitaweka picha hapo chini Ili uione ikoje.

Ukiachana na Cabbage pia Kimchi huwekwa Vitunguu maji , Tangawizi, Vitunguu swaumu pamoja na Chilli powder alafu huchachushwa (fermented) kwa muda ili kupata menu yenyewe.

Baada ya kupikwa Kimchi inaweza kufanyiwa "PACKAGING" vizuri na ikauzwa kwenye Supermarket kama bidhaa ya kawaida.

Kwa hapa Dar Kimchi inapatikana pale Atti Korean Restaurant na Goong Restaurant Slip way

Video ya jinsi ya kupika kimchi, Link yake hii hapa.




vegan-kimchi-recipe-12-of-14.jpg
kimchi-recipe.jpg
3d849a8c423a5e448d3ac94958564467.jpg
easy-kimchi-korean-fermented-cabbage-ft-1.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom