Ifahamu Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo

Rubondo
Ni vizuri kuzitangaza sehemu zote katika nchi yetu ambazo ni za utalii
Nchi inatakiwa ijulikane yote na sio baadhi tu
Mimi siijui Rubondo na wengi wetu pia
Sasa mtalii bila kumsifia ataijuaje?
Tena ingekuwa kwenye packaging kabisa kuwa watapelekwa siku 2 kisiwani
 
Pamoja na kukipamba sana bado hakistahili kubebwa na Boeing 787 Dreamliner. Dreamliner ilipaswa ibebe kitu unique na kikubwa kwa sababu ni ndege ya masafa marefu. Rubondo ingekuwa kwenye Bombardier ingekuwa sawa kabisa.

Watanzania bado tuna tatizo kwenye branding and promotion. Ninachikiona ni kufanya matangazo ya kumridhisha Rais kwa vile anatoka kanda hiyo.

Hakuna mtalii atakayetoka India au Guangzhou kwa ajili ya kwenda Rubondo kuja kuviona hivyo vitu ulivyo vitaja mtoa mada.

Tuendelee kupaza sauti ya kuitangaza Kilimanjaro, Ngorongoro na Serengeti. Ni kweli Kilimanjaro nalo limeandikwa, ila badala ya Rubondo basi tungeendelea kuandika vilele vya Mawenzi au Kibo.

Ushauri; ATCL ihusishe Wizara ya Utalii au taasisi zilizo chini yake kama TTB au TANAPA kwenye branding.
Mkuu umepiga penyewe, hukutaka unafki ktk hili.
 
Zipo ndege tatu mpya zitakazowasili mwakani ambazo zitabeba majina hayo mengine.... Ngorongoro ipo au hujaosoma
Hata kama ipo still tuna vivutio vikubwa by hierarchy vingi kuliko Rubondo. Think about Mikumi, Ruaha, Gombe, Seronera etc.

Hiyo Rubondo hata Mtanzania wa kawaida hajui kama siyo mwenyeji wa lake zone ndiyo maana nimependekeza kuwa Bombardier ndiyo ingehusika kuwatangazia Wa Tanzania kwanza kwa vile yenyewe trip zake ni za humu humu Tanzania.
 
Stupid question. Usimjibu mpumbavu kadri ya upumbavu wake usije kuwa sawa na yeye... Mithali 26:4
Tusi hili ndilo lililokuelewesha kwamba tanapa hawakuhusika kuchagua jina..wapumbav wanna shida sana..wanapenda kudandia Mambo kwa mbele, ndivyo walivyo..vitu vinafanyika vya maendeleo ndio wanaibuka ku dictate terms na how to go about..miaka yote wapumbaff nyie mlikuwa wapi..mbona hata hizo ndege hamkuwa Wala mkiziwazia..Na naomba Allah Mwenyezi Mungu akawanyamazishe midomo yenu milele. Hatutaki ujinga..mmefilisika Sera kichwani shwaaiinnnn
 
Pamoja na kukipamba sana bado hakistahili kubebwa na Boeing 787 Dreamliner. Dreamliner ilipaswa ibebe kitu unique na kikubwa kwa sababu ni ndege ya masafa marefu. Rubondo ingekuwa kwenye Bombardier ingekuwa sawa kabisa.

Watanzania bado tuna tatizo kwenye branding and promotion. Ninachikiona ni kufanya matangazo ya kumridhisha Rais kwa vile anatoka kanda hiyo.

Hakuna mtalii atakayetoka India au Guangzhou kwa ajili ya kwenda Rubondo kuja kuviona hivyo vitu ulivyo vitaja mtoa mada.

Tuendelee kupaza sauti ya kuitangaza Kilimanjaro, Ngorongoro na Serengeti. Ni kweli Kilimanjaro nalo limeandikwa, ila badala ya Rubondo basi tungeendelea kuandika vilele vya Mawenzi au Kibo.

Ushauri; ATCL ihusishe Wizara ya Utalii au taasisi zilizo chini yake kama TTB au TANAPA kwenye branding.
Yaani tuendelee kutangaza vilele vya mlima wakati kuna maeneo hayajatangazwa kabisa? Mlima umeshatangazwa, Ngorongoro nayo imetangazwa kwenye ndege na kwa sehemu nyingi hadi timu ya ngorongoro heroes, timu ya taifa bila zenji, inaitwa Kmajaro stars(heroes), serengeti nayo vile vile. Acheni rigidity na wivu.
 
Ndege yetu mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakayowasili mchana wa leo imepewa jina la kisiwa cha Rubondo 'Rubondo Island'. Hii ni ndege ya nane mpya katika ya 11 zilizonunuliwa na serikali ya CCM inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe MAGUFULI kwa lengo la kuimarisha shirika letu na ndege (ATCL).

Nimeona nikufahamishe kidogo juu ya kisiwa hiki kilichopewa hadhi ya hifadhi ya Taifa. Moja ya faida ya kumiliki shirika imara la ndege ni pamoja na kuutangaza utalii wetu ili watalii wengi zaidi waje nchini. Kuzipa ndege majina ya vivutio vyenu vya utalii ni njia moja wapo ya kuutangaza utalii wenu.

Sasa fahamu machache juu ya kisiwa hiki cha Rubondo:-

1. Kisiwa hiki waliishi wakazi waliojulikana kama Banyarubondo hadi kati ya mwaka 1964-1965 serikali ilipolazimika kuwaondoa kwa kuwalipa fidia na kisiwa hiki kutangazwa pori la akiba mnamo mwaka 1966 na baadae kupandishwa daraja kuwa hifadhi ya Taifa mwaka 1977. Kisiwa cha Rubondo kipo kusini magharibi mwa ziwa Victoria.

2. Kisiwa cha hifadhi ya Taifa Rubondo kina ukubwa wa kilomita za mraba 457 ambazo kati yake 237 ni nchi kavu na 220 ni maji. Hifadhi hii ipo jirani na visiwa 11 vya makazi ambavyo ni Mizo, Nyamitundu, Chitende, Katera, Iroba, Chambuzi, Munyila, Makosi na Izilambula.

3. Kisiwa cha hifadhi ya Taifa Rubondo ndio pekee hapa nchini na Afrika vinavyopatikana katika makazi ya maji ya ziwa.

4. Rubondo ina wanyama wa asili na waliopandikizwa. Mnyama wa asili ni nzohe ambaye anapatikana katika hifadhi hii pekee. Wapo vile vile tembo, sokwe mtu, pongo, mamba, viboko, fisi maji, ngedere, kenge, ndezi, vicheche, nguchiro, ndege aina 400, samaki aina 13, misitu minene mikubwa ya asili ya Kongo, fukwe zilizojaa rasilimali za uoto wa asili wenye harufu nzuri ya kipekee na eneo zuri la kulala watalii.

wafanyakazi wengi wa migodi mikubwa na viwanda vikubwa kanda ya ziwa, raia wa kigeni wanaokuja kufanya tafiti pia hupendelea kwenda kupumzika katika kisiwa hiki kwani kinavutia na kinautulivu wa hali ya juu. Panga kukitembelea.

#TanzaniaUnforgettable
#MabadilikoBora #MabadilikoYaKweli #MabadilikoTuliyoyataka #ChaguaCCMKaziIendelee

View attachment 1245023View attachment 1245024View attachment 1245025View attachment 1245026
Kuna kitu cha msingi sana umesahau,sport fishing, ni eneo maalum sana kiasi kwamba kuna waswiss huwa wanakuja kila mwaka kwa ajili ya hiyo kitu.

Vile vile kuna luxury camp moja,kama aijaongezwa nyingine na tanapa wana camp site yao ambayo ni raisi sana waweza lala kwa buku tano tu kwa usiku,kwa kweli rubondo ni amazing place.
 
Tusi hili ndilo lililokuelewesha kwamba tanapa hawakuhusika kuchagua jina..wapumbav wanna shida sana..wanapenda kudandia Mambo kwa mbele, ndivyo walivyo..vitu vinafanyika vya maendeleo ndio wanaibuka ku dictate terms na how to go about..miaka yote wapumbaff nyie mlikuwa wapi..mbona hata hizo ndege hamkuwa Wala mkiziwazia..Na naomba Allah Mwenyezi Mungu akawanyamazishe midomo yenu milele. Hatutaki ujinga..mmefilisika Sera kichwani shwaaiinnnn
Hujui kuwa hujui, nao ni ulemavu na hauna tiba.
 
Back
Top Bottom