MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Burigi ni moja kati ya Hifadhi tano zilizopo Mkoani Kagera ambazo ni Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika yaliyotangazwa hivi Karibuni kuwa hifadhi za Taifa ambapo mapori hayo yalikuwa chini ya Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na sasa tayari Mapori hayo yanasimamiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
>>>>>>>>https://www.ippmedia.com/sw/makala/utalii-wapiga-hodi-kagera [Fuatilia taarifa hii kutoka IPP media ya August 26, 2018]Hebu tueleze hiyo hifadhi ukubwa wake, na historia yake kwanza. Je inaweza kuhifadhi wanyama wa aina gani.
Wanyamapori kuhamishiwa katika Hifadhi Taifa Burigi ni mbinu ya na utalaam wa "ecology" lengo likiwa ni kuwaepusha baadhi ya wanyama kupata madhara ya kimazingira katika maeneo waliokuwepo na pia lengo lingine ni kupandikiza aina mbalimbali nyingine za wanyama katika Hifadhi ili kuongeza vivutio ambavyo ni muhimu kwa Watalii wa ndani na nje kuja katika Hifadhi hizo kuona.
Aidha, TANAPA wanaendelea na mikakati ya kuzitangaza Hifadhi mpya zilizoko Mkoani Kagera ili wawekezaji wa ndani nje waweze kuwekeza Kagera.
Hifadhi hiyo haipo katika Wilaya ya Chato kama ilivyoelezwa bali ipo katika Mkoa wa Kagera.
Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera .
Wito unatolewa kwa vijana Mkoani Kagera kuanza kuchangamkia fursa kwa kuanza kujiandaa katika masomo ya utalii ambapo watapata ajira za kuongozA Watalii, kujiandaa kusomea uhotelia ili kufanya kazi katika Hoteli za Kitalii zitakazojengwa katika Hifadhi hizo za Taifa Mkoani Kagera, hayo ni pamoja na kusomea lugha mbalimbali ili kupata fursa nzuri ya kuongoza Watalii kutoka nchi mbalimbali na kuelezea vizuri juu ya maliasili katika hifadhi hizo.