Ifahamu Familia ya Said Salim Bakhresa

Kwa hii collabo, Bakhresa Group haiwezi kufa, na badala yake itaendelea kwa miongo mingine kadhaa kama tunavyoona biashara za wenzetu kwenye mabara mengine!! Na hiki ndicho kinatushinda ngozi nyeusi... na usikute kampuni kama IPP au Infotech hivi sasa zimeshaanza kutetereka kwa sababu tu waasisi wake wamefariki!!
Kampuni zetu ni Kama makanisa ya upako akifa mmiliki nayo ufa
 
Una miaka kuanzia 20 na kuendelea na bado unategemea wazazi kwa asilimia 100 jitafakari sana wewe bila hivyo utaishia pabaya.

Nimesema asilimia 100 wapo wanaopambana wanategemea asilimia kadhaa tu na asilimia kadhaa wanajimudu hawa wana muelekeo nzuri.

Wapo wanaojimudu 100% kila kitu hawa ndo wanaoelekea pazuri.

Lakini una miaka kuanzia 20 mpk 35 unategemea kwenu nenda ukaombewe na ni aibu na kinyaa kukuta mtu nzima kijana una nguvu lakini unakula kwenu bure, kulala bure, kila kitu kwenu na huzalishi hata hamsini ujitafakari sana maana utaishia pabaya sana na maisha yako yatakua ya shida tu.

Kujitegemea kuanzia miaka 20 ni lazima kwa kila kijana hususan vijana kiume.
SIsi ngozi nyeusi akili zetu imegotea hapo.
 
Familia ya Said Salim Bakhresa

Said Salimu Awadh Bakhresa ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na uzoefu wa zaidi ya miaka 30 wa kusimamia kundi la kampuni za biashara. Yeye ni mwasisi na mwenyekiti wa Bakhresa Group of Companies. Alizaliwa mwaka 1949 na kukulia Zanzibar.

Bakhresa Group ni mkusanyiko wa kampuni mbalimbali zilizosajiliwa zinazofanya uchakataji wa mazao ya kilimo, vyakula na vinywaji baridi, usafiri wa majini, ufungashaji, usafirishaji, urejelezi wa plastiki na vyombo vya habari. Pia anaendesha hoteli huki Zanzibar inayoitwa Hotel Verde.

Mwanaviwanda maarufu anayefahamika Afrika Amshariki na Kati yote, Bakhresa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuwa muuzaji wa urojo, kabla ya kujishughulisha kama mwendesha mkahawa katika miaka ya 1970. Kutokana na kuanza bila ya makuu aliunda himaya ya biashara ndani ya kipindi cha miongo mitatu tu. amemuoa Fathiya Bakhresa na wana watoto saba: Mohamed Said Salim Bakhresa, Abubakar Said Salim Bakhresa, Omar Said Salim Bakhresa , Yusuph Said Salim Bakhresa, Khalid Said Salim Bakhresa (amefariki 2007), Mariam Said Salim Bakhresa. Bakhresa Group ni biashara ya familia. Watoto wake wote ni Wakurugenzi Watendaji wa Salim bakhresa & Co Ltd yenye hisa nyingi katika Azam Media Limited. Watoto wake pia wana nyadhifa zifuatazo:

Yusuph Said Salim Bakhresa:

Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Limited na Mkurugenzi wa Group Companies. Anashiriki kila siku kwenye shughuli za Bakhresa Food Products Ltd.

Abubakar Said Salim Bakhresa:

Anasimamia Bakhresa Malawi Limited, Bakhresa Grain Milling (Rwanda), Bakhresa Grain Milling Limitada (Msumbiji) na Bakhresa South Africa (Pty) Limited. Ana shahada ya kwanza ya Sayansi katika Usimamizi wa Biashara, somo kuu likiwa Fedha kutoka Chuo kikuu cha George Town, Washington D.C USA. Anajihusisha zaidi na biashara za usindikaji ngano katika Group na anasimamia ununuzi wa ngano kwa ajili ya Group.

Mohamed Said Salim Bakhresa:

Ni mkurugenzi Mtendaji wa Bakhresa Grain Milling (Uganda) Limited, kiwanda kikubwa zaidi cha kusindika ngano nchini Uganda. Amehitimu katika fedha,Sheria na utunzaji fedha kutoka chuo kikuu cha Southbank, United Kingdom.

Salim Ali Salim Bakhresa :

Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Verde Hotel. Hoteli Bora ya viwango vya 5 star iliyopo Zanzibar.
Pia amehitimu shahada ya Udhamili kwenye chuo cha Salford University huko United Kingdom.

Toa maoni yako hapo chini;-
Ushamili=uzamili
 
Aisee sio Mchezo yaani SSB wanae wote kawapa MASHAVU kwenye kampuni zake.
 
Mfumo Dume wa Kiislam umembana

Mfumo Dume wa Kiislam umembana

Kwa nini midomo yenu huwa wazi kama vyoo vya kienyeji kuusingizia uongo UISLAM? Wewe UISLAM Unaufahamu? Ni wapi uislam ulipo kataza au kuzuia mtoto wa kike kusomeshwa na kumiliki mali? Acha ujinga wewe.

Kwa taarifa yako na wengine kama wewe elewa kuwa Mke wa kwanza kabisa Wa Bwana Mtume s.a.w bi Khadija alikuwa mwanamke tajiri sana miongoni mwa matajiri wa Maka na alikuwa na msururu wa wafanyakazi Wanaume wakisambaza bidhaa zake sehemu mbalimbali za Shamu na uarabuni.
 
Back
Top Bottom