Ifahamu Familia ya Said Salim Bakhresa

Drop shipping Tanzania

Senior Member
Jun 15, 2020
132
250
Familia ya Said Salim Bakhresa

Said Salimu Awadh Bakhresa ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na uzoefu wa zaidi ya miaka 30 wa kusimamia kundi la kampuni za biashara. Yeye ni mwasisi na mwenyekiti wa Bakhresa Group of Companies. Alizaliwa mwaka 1949 na kukulia Zanzibar.

Bakhresa Group ni mkusanyiko wa kampuni mbalimbali zilizosajiliwa zinazofanya uchakataji wa mazao ya kilimo, vyakula na vinywaji baridi, usafiri wa majini, ufungashaji, usafirishaji, urejelezi wa plastiki na vyombo vya habari. Pia anaendesha hoteli huki Zanzibar inayoitwa Hotel Verde.

Mwanaviwanda maarufu anayefahamika Afrika Amshariki na Kati yote, Bakhresa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuwa muuzaji wa urojo, kabla ya kujishughulisha kama mwendesha mkahawa katika miaka ya 1970. Kutokana na kuanza bila ya makuu aliunda himaya ya biashara ndani ya kipindi cha miongo mitatu tu. amemuoa Fathiya Bakhresa na wana watoto saba: Mohamed Said Salim Bakhresa, Abubakar Said Salim Bakhresa, Omar Said Salim Bakhresa , Yusuph Said Salim Bakhresa, Khalid Said Salim Bakhresa (amefariki 2007), Mariam Said Salim Bakhresa. Bakhresa Group ni biashara ya familia. Watoto wake wote ni Wakurugenzi Watendaji wa Salim bakhresa & Co Ltd yenye hisa nyingi katika Azam Media Limited. Watoto wake pia wana nyadhifa zifuatazo:

Yusuph Said Salim Bakhresa:
Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Limited na Mkurugenzi wa Group Companies. Anashiriki kila siku kwenye shughuli za Bakhresa Food Products Ltd.

Abubakar Said Salim Bakhresa:
Anasimamia Bakhresa Malawi Limited, Bakhresa Grain Milling (Rwanda), Bakhresa Grain Milling Limitada (Msumbiji) na Bakhresa South Africa (Pty) Limited. Ana shahada ya kwanza ya Sayansi katika Usimamizi wa Biashara, somo kuu likiwa Fedha kutoka Chuo kikuu cha George Town, Washington D.C USA. Anajihusisha zaidi na biashara za usindikaji ngano katika Group na anasimamia ununuzi wa ngano kwa ajili ya Group.

Mohamed Said Salim Bakhresa:
Ni mkurugenzi Mtendaji wa Bakhresa Grain Milling (Uganda) Limited, kiwanda kikubwa zaidi cha kusindika ngano nchini Uganda. Amehitimu katika fedha,Sheria na utunzaji fedha kutoka chuo kikuu cha Southbank, United Kingdom.

Salim Ali Salim Bakhresa:
Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Verde Hotel. Hoteli Bora ya viwango vya 5 star iliyopo Zanzibar.
Pia amehitimu shahada ya Uzamili kwenye chuo cha Salford University huko United Kingdom.

Toa maoni yako hapo chini;-
 
mtongwe

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
477
1,000
Enzi zake bakhress akiuza Biriani/pilau. View attachment 1490667
Umenikumbusha mbali sana mkuu,hilo eneo mpaka leo lipo na bado analimiliki.....maana kwenye mtaa huo pale mkununguni na Swahili ilipo bank ya watu wa Zanzibar ndo kulikuwa ice cream centre na kwa mbele pale Mkunguni just opp na al Uruba hotel ndo kulikuwa na hiyo Restaurant ambapo kwa sasa amejenga ghorofa kuubwa lenye L shape
Na sababu ya kujenga ilo jengo la L shape ni baada ya mwenye jengo lilopo mtaa wa mkunguni na sikukuu kukataa katakata kumuuzia
 
mtongwe

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
477
1,000
Kwangu mimi Bakheresa ni Kati ya bad example Enterprenuer. Hakuna anayejua ukweli wa mafanikio ya Said Bakheresa wapo wanao sema ameanzia ktk kuhuza ice cream Kariakoo, wengine wanasema alipewa mitambo ya NMC na Serikali ya Tanzania.
Kwangu mimi Bakheresa ni mfanyabiashara mwenye roho ya tamaa anayetaka kufanya kila aina ya biashara anayoiona mbele yake kuwahina mafanikio na ndiyo maana biashara zake zote ameweka ndugu au watoto wake ndiyo waziendeleze.
Nilitegemea kwa umri na mafanikio aliyopata angekuwa na hata kitabu kimoja au biography yake kuinspire vijana wa Tanzania kuiga mfano wake hili waweze kupata mafanikio kama yake lakini matokeo yake history ya mafaniko yake anaigawa kwa familia yake tu.
Hatukatai kuwa anasiadia sana jamii lakini tulitegemea kuona kuwa mtu wa mfano kama REGINARD MENGI ( Mungu amrehemu) , tulitegemea tumuone Bakheresa anazunguka na kutoa speech za mafanikio yake hili azarishe mamilionea kama yeye ktk Africa kama anavyofanya DANGOTE, WARREN BUFFET, BILLGATES, ALIBABA etc.
Kinyume Chake Mzee huyu anatamaa ya kukuza utajiri wa yeye na familia yake peke yake. Hakuna anayejua mafanikio yake yemetokana na nini.
Kila biashara anata kufanya yeye na familia yake.Bakheresa ni BAD EXAMPLE SUCCESSFUL MAN IN AFRICA.
Nahisi kama chuki imetawala ktk uandishi wako
 
Chiwaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
5,473
2,000
Familia ya Said Salim Bakhresa

Said Salimu Awadh Bakhresa ni mfanyabiashara mwenye mafanikio na uzoefu wa zaidi ya miaka 30 wa kusimamia kundi la kampuni za biashara. Yeye ni mwasisi na mwenyekiti wa Bakhresa Group of Companies. Alizaliwa mwaka 1949 na kukulia Zanzibar.

Bakhresa Group ni mkusanyiko wa kampuni mbalimbali zilizosajiliwa zinazofanya uchakataji wa mazao ya kilimo, vyakula na vinywaji baridi, usafiri wa majini, ufungashaji, usafirishaji, urejelezi wa plastiki na vyombo vya habari. Pia anaendesha hoteli huki Zanzibar inayoitwa Hotel Verde.

Mwanaviwanda maarufu anayefahamika Afrika Amshariki na Kati yote, Bakhresa aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuwa muuzaji wa urojo, kabla ya kujishughulisha kama mwendesha mkahawa katika miaka ya 1970. Kutokana na kuanza bila ya makuu aliunda himaya ya biashara ndani ya kipindi cha miongo mitatu tu. amemuoa Fathiya Bakhresa na wana watoto saba: Mohamed Said Salim Bakhresa, Abubakar Said Salim Bakhresa, Omar Said Salim Bakhresa , Yusuph Said Salim Bakhresa, Khalid Said Salim Bakhresa (amefariki 2007), Mariam Said Salim Bakhresa. Bakhresa Group ni biashara ya familia. Watoto wake wote ni Wakurugenzi Watendaji wa Salim bakhresa & Co Ltd yenye hisa nyingi katika Azam Media Limited. Watoto wake pia wana nyadhifa zifuatazo:

Yusuph Said Salim Bakhresa:
Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Limited na Mkurugenzi wa Group Companies. Anashiriki kila siku kwenye shughuli za Bakhresa Food Products Ltd.

Abubakar Said Salim Bakhresa:
Anasimamia Bakhresa Malawi Limited, Bakhresa Grain Milling (Rwanda), Bakhresa Grain Milling Limitada (Msumbiji) na Bakhresa South Africa (Pty) Limited. Ana shahada ya kwanza ya Sayansi katika Usimamizi wa Biashara, somo kuu likiwa Fedha kutoka Chuo kikuu cha George Town, Washington D.C USA. Anajihusisha zaidi na biashara za usindikaji ngano katika Group na anasimamia ununuzi wa ngano kwa ajili ya Group.

Mohamed Said Salim Bakhresa:
Ni mkurugenzi Mtendaji wa Bakhresa Grain Milling (Uganda) Limited, kiwanda kikubwa zaidi cha kusindika ngano nchini Uganda. Amehitimu katika fedha,Sheria na utunzaji fedha kutoka chuo kikuu cha Southbank, United Kingdom.

Salim Ali Salim Bakhresa:
Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Verde Hotel. Hoteli Bora ya viwango vya 5 star iliyopo Zanzibar.
Pia amehitimu shahada ya Uzamili kwenye chuo cha Salford University huko United Kingdom.

Toa maoni yako hapo chini;-
Azam Marine yupo nani?
 
SIERA

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,866
2,000
Said Salim Bahresa sio tajiri kivile, mali zake nyingi za kuwezeshwa, lakini wenye hizo mali ni wengine. (YAANI hidden hand au web master au web spider) bahresa anatumika kama Vehicle tu, au tunaita the Gofer.
Huyu ni elite kama alivyo Bill gates na wakina Jeff Bezos au Mark Zuckerberg au Jack Ma..mali zao ni kama wamepewa wasimamie tu mali sio zao, ni ngumu sana eti kuuza kahawa ndani ya miaka 30 uwe tajiri namba hiyo, tena kwenye uchumi mdogo wa Zanzibar na Dsm.
Hawa ni waabudu shetani angalia logo za kampuni yao utaelewa. Ndo maana product zao za vyakula zina viambata visivyo sahihi kama Fortification nk kwenye maji na juice na ngano watu wanaumwa kwa kula vyakula vyao. Sio Azam tu hata Mo ni satanist.
Unamatatizo ya akili si bure
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
12,671
2,000
Umeona eeh. Watoto shule ipo na wamesomea dedha na uchumi
Kwa hii collabo, Bakhresa Group haiwezi kufa, na badala yake itaendelea kwa miongo mingine kadhaa kama tunavyoona biashara za wenzetu kwenye mabara mengine!! Na hiki ndicho kinatushinda ngozi nyeusi, na usikute kampuni kama IPP au Infotech hivi sasa zimeshaanza kutetereka kwa sababu tu waasisi wake wamefariki!
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
9,990
2,000
Umeona eeh. Watoto shule ipo na wamesomea dedha na uchumi
Nimemkubali sana Mzee Bakhresa hasa nikizingatia mwenyewe hana shule. Nadhani aliona effects za kutokuwa na shule mapema sana, na kwahiyo akaamua jambo kama hilo lisitokee kwa wanawe.
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
12,671
2,000
Nimemkubali sana Mzee Bakhresa hasa nikizingatia mwenyewe hana shule. Nadhani aliona effects za kutokuwa na shule mapema sana, na kwahiyo akaamua jambo kama hilo lisitokee kwa wanawe.
Kabisa mkuu. Ka invest sana kwa wanae, yaani almost wote kawasomesha nje. Ndio sababu haishangazi kuona kampuni zao zinakua na kusambaa kila nchi hapa mashariki na kati. Wako vizuri sana hawa jamaa.
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,109
2,000
Alishindwa kuwaonyesha vision yake,so sad
Amekufa watoto wana vision tofauti kwaio ni ngumu kuendeleza.
Pia naona watu weusi ndugu hatupendani kuna kitu kinatusambaratisha jinsi tunavyo kua taratibu nashindwa kukiwasilisha vizuri lakini chanzo kikuu ni wazazi ndio wanafanya makosa kila mtu anakua akiangalia maisha yake na si family legacy
Labda iko kwenye damu yetu
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,109
2,000
Usafirishaji ni Omar Bakhresa na Mohamed Bakhresa (Mombasa)japo yusuf ana Malori yake binafsi sio ya family lakini asilimia kubwa ni hao wawili

Mpira ni yusuf pia , boat ni yusuf pia
Nionavyo ni kampuni nyingi ambazo kila mtoto ana yake ili kusaidia brand
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,109
2,000
Kwangu mimi Bakheresa ni Kati ya bad example Enterprenuer. Hakuna anayejua ukweli wa mafanikio ya Said Bakheresa wapo wanao sema ameanzia ktk kuhuza ice cream Kariakoo, wengine wanasema alipewa mitambo ya NMC na Serikali ya Tanzania.
Kwangu mimi Bakheresa ni mfanyabiashara mwenye roho ya tamaa anayetaka kufanya kila aina ya biashara anayoiona mbele yake kuwahina mafanikio na ndiyo maana biashara zake zote ameweka ndugu au watoto wake ndiyo waziendeleze.
Nilitegemea kwa umri na mafanikio aliyopata angekuwa na hata kitabu kimoja au biography yake kuinspire vijana wa Tanzania kuiga mfano wake hili waweze kupata mafanikio kama yake lakini matokeo yake history ya mafaniko yake anaigawa kwa familia yake tu.
Hatukatai kuwa anasiadia sana jamii lakini tulitegemea kuona kuwa mtu wa mfano kama REGINARD MENGI ( Mungu amrehemu) , tulitegemea tumuone Bakheresa anazunguka na kutoa speech za mafanikio yake hili azarishe mamilionea kama yeye ktk Africa kama anavyofanya DANGOTE, WARREN BUFFET, BILLGATES, ALIBABA etc.
Kinyume Chake Mzee huyu anatamaa ya kukuza utajiri wa yeye na familia yake peke yake. Hakuna anayejua mafanikio yake yemetokana na nini.
Kila biashara anata kufanya yeye na familia yake.Bakheresa ni BAD EXAMPLE SUCCESSFUL MAN IN AFRICA.
Maajabu. Sasa ulitaka akugawie.
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,109
2,000
Said Salim Bahresa sio tajiri kivile, mali zake nyingi za kuwezeshwa, lakini wenye hizo mali ni wengine. (YAANI hidden hand au web master au web spider) bahresa anatumika kama Vehicle tu, au tunaita the Gofer.
Huyu ni elite kama alivyo Bill gates na wakina Jeff Bezos au Mark Zuckerberg au Jack Ma..mali zao ni kama wamepewa wasimamie tu mali sio zao, ni ngumu sana eti kuuza kahawa ndani ya miaka 30 uwe tajiri namba hiyo, tena kwenye uchumi mdogo wa Zanzibar na Dsm.
Hawa ni waabudu shetani angalia logo za kampuni yao utaelewa. Ndo maana product zao za vyakula zina viambata visivyo sahihi kama Fortification nk kwenye maji na juice na ngano watu wanaumwa kwa kula vyakula vyao. Sio Azam tu hata Mo ni satanist.
Ndio mnvayodanganywa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom