Online Pastor
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 1,948
- 1,515
Mji wa kwanza kutekwa na Waisraeli baada ya kuuvuka mto Yordani ulikuwa Yeriko.
Na Mungu aliwaagiza kuwa kila watakapouvamia mji wa Kaanani ni sharti waangamize vyote watakavyovikuta kwenye miji isipokuwa vito vya thamani ambavyo sharti ilibidi viwekwe kwenye hema ya kukutania.
Kwa kutii agizo hili mji wa Yeriko ulianguka na Waisraeli kushinda kirahisi.
Mji uliofuata kuvamia ulikuwa ni mji mdogo wa Ai.
Yoshua akiamini kuwa atashinda kirahisi alituma jeshi dogo la Waisraeli 2000 ambao waliishia kutwangwa na kupepetwa na Waisraeli 36 kufariki hapohapo.
Ilipopitishwa sensa ya kubaini chanzo cha kushindwa vita,ikaonekana kuwa kuna mtu aliiba vito mjini Yeriko.Mtu huyo alikuwa Akani,ambaye ilibidi auwawe yeye na familia yake.
TUNAJIFUNZA NINI?
Kuna mikosi,laana,na shida ambavyo vinatukabili leo kutokana na dhambi za ndugu,jamaa na marafiki zetu.Hivyo tujifunze kumuuliza roho mtakatifu kila tunaposhindwa kufanikiwa ili tujue kama chanzo ni siye,Mungu,Shetani au ndugu zetu
REFFERENCES
YOSHUA 7