Ifahamu Dhahabu ya Kijani (GREEN GOLD) Itakayokuza Uchumi wa Wakulima wa Tanzania

Wazo Kuu

Member
Oct 21, 2018
47
150
Dhahabu ya Kijani (Green Gold) ni zao linalostawi vizuri katika maeneo yenye milima zenye mvua nyingi angalau nusu mwaka. Afrika mashariki linastawi vizuri katika nchi za Tanzania, Uganda Burundi na Rwanda zina utajiri mkubwa kutokana na ardhi yake kukubali kustawi kwa wingi Matunda ya Maparachichi.

Parachichi la Tanzania linatajwa kuwa bora Zaidi na linalopendwa Zaidi katika masoko ya Ulaya.

Green Gold ya Tanzania ni zao ambalo litaifanya Tanzania kumaliza kabisa tatizo la umasikini kutokana na uhitaji Mkubwa katika soko la Ulaya kwa sasa.

Ukitoa Kenya kuwa msafirishaji Mkubwa wa Maparachichi yanayozalishwa Tanzania, lakini pia Nchi ya Nigeria na Uganda kwa uwekezaji zinatarajiwa Miaka 10 baadaye zitakuwa moja ya Mataifa makubwa yanayozalisha kwa wingi Maparachichi na kusafirisha nje ya nchi.

Kwa hali ya sasa Kilimo cha Parachichi ni cha uhakika na chenye faida kubwa, ambapo kwa nchi kama Marekani peke yake matumizi ya Parachichi kwa kila raia wake imeongezeka kwa asilimia 406 kuanzia 1990 hadi 2017.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa Parachichi Duniani, nchi ya Uganda imedhamiria kuwahamasisha Wakulima Wadogo kuwa wazalisha wakubwa wa zao la Parachichi waweze kufikia asilimia 75, huku Wakulima wa Mashamba makubwa wenyewe wazalishe kwa asilimia 25 na lengo ni kuhakikisha wananchi wa hali ya chini nchini Uganda wanajiingiza kwenye Kilimo hicho ili kukuza uchumi wa wananchi kuuza bidhaa zao nje ya nchi.

Tanzania ni moja ya eneo bora katika mikoa ya Mbeya, Iringa, njombe, Ruvuma, rukwa , Katavi, Arusha ,Kilimanjaro, Tanga, Kagera, Mara na Morogoro yamebarikiwa ardhi yenye rutuba likatostawi zao la Parachichi.

Watanzania hawana budi kuitumia fursa hii ya kwa kulima Dhahabu ya Kijani (Maparachichi), kutokana na uhitaji wake kwa sasa katika nchi za Asia, Ualaya na Marekani

Bila kusahau Rais waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anahamaisha sana uwekezaji na Kilimo chenye tija, na moja ya maeneo ambayo ameyatazama sana na kuyapa kipaumbele ni Kilimo cha Miti ya Matunda ambayo yatakuwa yanasafirishwa nje ya nchi.

PARACHICHI 2.png
 

DE FULE

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
1,179
2,000
Barikiwa sana Wazo Kuu kwa bandiko hili.

Tunasubiri na wadau wengine waje wajazie nyama!
 

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
1,874
2,000
Mfumo wa udhibiti wa soko ndiyo changamoto.Ingekuwa ni Uhakika kama tungekuwa tunayaprocess hapa hapa bongo,lakini mimi sijawahi kuamini katika kilimo ambacho mazao yake tunayauza huko nje kama raw materials.Tena huwa siwashauri sana watu kuwekeza nguvu zao zote kwa zao ambalo linakwenda kuwa processes nje ya nchi,kwa sababu soko la hivyo ni delicate sana sana.
 

Lucky Star

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,249
2,000
Zamani nilijua Dhahabu ya kijani kwa mkulima ni Korosho.
Hata salamu yao ilikuwa:-
Korosho Korosho.....(kiitikio) Dhahabu ya kijani kwa mkulima.

Anyway, ni zao zuri kwa biashara.
Lakini kutokana na changamoto zake za uhifadhi na usafirishaji, basi elimu zaidi inatakiwa kutolewa.
Ni zao lisilo na magonjwa mengi, na huzaa vizuri kama mbegu zilizopandwa ni bora.

Shelf life yake baada ya kukomaa na kuiva ni ndogo kwa matunda.

Soko la ndani ni lile la kimazoea, yaani siku zote marketing strategies na thamani ya zao havibadiliki sana.

*Elimu ya uhifadhi itolewe ili kulinda ubora, kwani parachichi hata kwa kulitazama ni 'the most perishable crop'.
*Hatua sahihi ya ukomavu kwa ajili ya uvunaji sidhani kama inajitosheleza.
*Channel za masoko yanayolipa zinafahamika kwa wachache, mamlaka husika zisaidie kutafuta soko la uhakika ikiwa ni pamoja na kuweka masuala ya kisheria yanayomlinda mzalishaji badala ya kuwahimiza kuzalisha au kuwasifia wachache waliofanikiwa.

Ngoja nifuturu kwanza.
 

Kong Chi

Member
Mar 15, 2021
29
45
Kuna kijana nilimwona youtube huko kusini nafikiri mtwara anafanya kilimo cha parachichi na anatengeneza millions na hata waziri mkuu alimtembelea niliona, sijui anayauza vipi na wapi mnaweza kujifunza kwake
 

DASM

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,789
2,000
Katika maeneo uliyoyataja nafikiri Njombe na Rungwe ndio sehemu yenye conducive environment wa kulima parachichi Kwa Tanzania. Ila Njombe itakuja kuwa leading producer in future
 

DASM

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,789
2,000
Mfumo wa udhibiti wa soko ndiyo changamoto.Ingekuwa ni Uhakika kama tungekuwa tunayaprocess hapa hapa bongo,lakini mimi sijawahi kuamini katika kilimo ambacho mazao yake tunayauza huko nje kama raw materials.Tena huwa siwashauri sana watu kuwekeza nguvu zao zote kwa zao ambalo linakwenda kuwa processes nje ya nchi,kwa sababu soko la hivyo ni delicate sana sana.
Parachichi inatumika as food kwahiyo ni chakula. Processing yake ni kusafisha na Grading kwenye maboksi . Kule zinauzwa at least 2 us dollar or 2.5 usdollar per parachichi. Kwahiyo small proportion ndio inaenda kutengeneza juice , mafuta and other cosmetic s. Parachichi inapanda bei kutokana na nutritional components zilizomo ndani yake
 

Lucky Star

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,249
2,000
Katika maeneo uliyoyataja nafikiri Njombe na Rungwe ndio sehemu yenye conducive environment wa kulima parachichi Kwa Tanzania. Ila Njombe itakuja kuwa leading producer in future
Ongeza Kagera, Kigoma na baadhi ya maeneo ya mikoa ya kaskazini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom