Ifahamu 'Competence Based Curriculum' (CBC) ambayo haitamuacha nyuma mtoto yeyote

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
669
Elimu ya sasa wanafunzi huandaliwa kufaulu mitihani bila kukuza uwezo binafsi walionao hali inayoua vipaji vya wengi na kutokomeza ndoto za watoto kadhaa waliopo nchini. Mfumo unaotumika kwa sasa ni mfumo wa 7-4-2-3 ukiangalia miaka ambayo mtu anaitumia kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.

Hata hivyo kwa kuzingatia utofauti wa uwezo wa watoto, ni kitu kisichoendana na akili watu kutumia mtihani mmoja kupima uwezo wa kila mtoto ambaye ana uelewa na vipaji tofauti.

Misingi ya Competence Based
Tofauti na kutilia mkazo kwenye mitihani, competence based inatilia mkazo kwenye matokeo ya kukuza ujuzi husika (Outcome oriented), pia ni 'learner centered' yaani inamuangalia mwanafunzi kama individual na kumkuza kama yeye na sio kuangalia kundi la wanafunzi kama ilivyo hivi sasa.

Utofauti, kwa sasa wanafunzi wanatakiwa kuwa na ufahamu na uelewa sawa, wakati mtaala wa kupima uwezo utakuza utofauti ili kuwa na upekee wa kimawazo.

Namna ya kuwapima wanafunzi kwenye Competence Based Curriculum.
Namna hii ya ufundishaji inaanza na Diagnostic ambayo inatafuta kufahamu gap lililopo ili kutambua uhitaji.

Formative. Ambapo inakuwa na nia ya kujenga ujuzi kwa mwanafunzi. Hii ikiwa ni pamoja na kupima uwezo wa mwanafunzi kuelewa knowledge anazojifunza.

Summative assessments Ambapo ni upimaji wa jumla wa ujifunzaji kwa mwanafunzi.

Competence based inalenga kwenye kukuja ujuzi, ufahamu na maadili ambayo yatatumika katika maisha ya kila siku. Inakuza uwezo wa mwanafunzi kutegemea na vipaji vyake. Inalenga kumkuza mtu ili kuja kuwa mzalishajii bora ndani ya jamii.

Wakati mtaala ulliopo unajikita kwenye kufaulu, competence based inafanya mtu ajifunze kujifunza, yaani elimu haaishi baada ya mtu kuhitimu, kuwa na uwezo wa kutatua mambo magumu kwa kujiamini. Na uwezo wa kutumia vifaa vya kidigitali.

Kiauhalisia mtaala ulipo umeshindwa mambo mengi sana hali inayopelekea wadau kuhitaji competence based curriculum ili kuwa na watoto wanaojielewa na kufahamu vitu wanafanya.
 
Ni kweli shule inaweza msaidia mtu kukuza alichonacho ila kwetu shule zimeua vipawa vya watoto wengi Sana na Bado zinaendelea kuuwa.
Na walio kwenye nafasi wako bize kusifia wenzetu ila kufanya kitu kwaajili ya Taifa lao wanajiweka back benches.
 
Ni kweli shule inaweza msaidia mtu kukuza alichonacho ila kwetu shule zimeua vipawa vya watoto wengi Sana na Bado zinaendelea kuuwa.
Na walio kwenye nafasi wako bize kusifia wenzetu ila kufanya kitu kwaajili ya Taifa lao wanajiweka back benches.
Uwekezaji wetu kwenye elimu ndiyo chanzo cha mauaji hayo.

Shule ya msingi yenye darasa la kwanza hadi la saba, ina walimu 5 January to December for seven years.

Kila mara nawaza, wale walimu wa private schools, tukiwa chuoni, darasani nilikuwa bora kuliko wao. Ila leo wanatoa matokeo mazuri kuliko mimi.

Jibu ni uwekezaji duni katika shule za umma.

Shule za umma siasa inatawala. Kiongozi wa taasisi akipiga sana kelele kumbana mwalimu awajibike, jiandae kwa figisu. Utaambiwa ananitaka kimapenzi au amenibaka. Na kitakachofuata ni dhahama kwa kiongozi.

Kwa ujumla, shule za umma ni kijiwe cha kupumzika waajiri kwenye sekta ya elimu.
 
Back
Top Bottom