Ifahamu AirBus-H225, Helicopter ya kijeshi iliyoubeba mwili wa Mzee Mkapa kuelekea Lupaso, Mtwara

Mr pianoman

JF-Expert Member
May 22, 2019
2,549
6,097
'Airbus H225' maarufu Super Puma kwa sasa Cougar ni helicopter inayoundwa na kampuni ya Airbus {#Eurocopter} barani Ulaya.
Imeanza kuundwa rasmi miaka ya 2000 ikiwa ni muendelezo wa maboresho ya hali ya juu katika kizazi cha 'Helicopter' ya awali aina ya Eurocopter #As332.

'Helicopter' hii ina matoleo mawili, ya kawaida H225 na ya kijeshi H225M. Imeundwa maalum kwa ajili ya usafirishaji abiria na mizigo kwenda umbali mrefu katika hali ya hewa zote kwa kutunia mafuta kidogo.

Pia mahususi zaidi kwa kazi za uokoaji {#search & #rescue}, Zimamoto, usafirishaji watu mashuhuri {#VIP}, usafirishaji katika vituo vya uchimbaji mafuta {#offshore_Oil_transport}, ulinzi na usalama katika bahari {#coastguard} n.k

Ni Helicopter yenye teknolojia ya kisasa ikiwemo #autopilot na nguvu kubwa inayozalishwa na injini mbili aina ya 'Turbomeca Makila.

Ina uwezo wa kubeba mzigo unaoning'inia nje {#slingload} tani 4.7 na kawaida tani 5.4

Kwa matoleo ya kijeshi #H225M au #EC725 uboreshaji na ufanisi ni mkubwa zaidi kutoka kwenye ubebaji mizigo #CargoHelicopter {#CH} na kuwa #UtilityHelicopter {#UH} kufanya kazi zote {#Multirole} kwa kupachikwa silaha {#Combat_SAR} na kusonga katika uwanja wa vita pasipo shaka.

Uwezo:
Kasi ya juu: hadi 315km/h
Umbali: km 984
Kimo: futi 19,000
Panga: 5 juu, 04 mkiani
Injini: 02 #Safran #Turbomeca #Makila2A1
Mafuta: 684 lbs
Abiria: 19 kawaida, 28 mkao wa kijeshi.
Bei/Mtandaoni: U$d Mil.28

Katika jambo kubwa ambalo #Amir_jeshi mkuu/Jeshi la wananchi #Tanzania {#jwtz/#tpdf/#tafc} limeonesha ubavu ni kuwa na Helicopter hizi mbili.
Hizi ni helicopter zinazotumiwa na mataifa makubwa kama:
#England
#Spain
#Japan
#France
#Denmark
#Norway
#Ukraine
#China
#Argentina
#Vietnam,
#Mexico n.k

Taarifa kutoka,
Airbus na wikipedia.View attachment 1519945
FB_IMG_1595964662862.jpg
 
Siyo ndogo lakini kwa kitu kinachopaa hewani ilipaswa isilingane na treni zinazotembea ardhini hasa ikizingatiwa ni ya kijeshi
Kwa helicopter hizo ndo speed zake ...............Helicopter hazijaundwa kwa ajili ya speed ndo maana hata ikiwa angani unaweza ukai control vizuri kuliko vyombo vingine vinavyotembea angani........helicopter angani kitu kikubwa ni "stability" na "maneuverability".........na ndo maana haitumiki sana kwa ishu za kusafirisha abiria na inaweza kufika
na kutumika sehemu ambazo vyombo vingine vya anga inakua ngumu kufika.....................
.................hio chini ndo helicopter inayoshikiria rekodi ya kasi zaidi duniani .....hapo imepishana speed kiasi gani na hii ya mleta mada??..........kwa comparison yako hujaitendea haki Helicopter...............ishu ni kwamba kila chombo kinakuaga na kazi yake maalum, kwa helicopter speed sio priority kubwa
Screenshot_20200729-000029.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom