If you had a chance, What will you do to Change Tanzania?

meku

New Member
Apr 29, 2008
2
0
Wadau ningependa kusikia maoni yenu.... nauliza hiviii.... kama ungepata nafasi ya kuibadili Tanzania ya leo ungefanya nini?...
 
Wadau ningependa kusikia maoni yenu.... nauliza hiviii.... kama ungepata nafasi ya kuibadili Tanzania ya leo ungefanya nini?...

Mkuu,

Unapoibuka ghafla na swali kama hili bila hata kuwa na utangulizi, unakuwapo unakosea.

Wewe anza kwa kutuambia kwamba una mawazo kuhusu kuibadili Tanzania ya leo halafu sisi tutafuatia.

Ila kwa kuendelea kukukaribisha, mimi nina maoni yafuatayo:

1. Ntaitisha kura ya maoni ya kuibadili katiba ya Tanzania, iendane na zama za sasa zenye mambo kama kuwa na wagombea ambao wameishi nje ya nchi kwa miaka kadhaa, wenye umri usiozidi miaka 50 na si chini ya miaka 35, kupewa nafasi ya kuleta ujuzi na uzoefu katika ardhi ya nchi yao.

2. Ntabadili mfumo wa serikali ili kuwa na serikali za mitaa zenye kubuni na kupanga mipango yake bila kuingiliwa na serikali kuu isipokuwa kwa masuala ya kuchagua madiwani na meya ambapo itabidi pawepo na wagombea binafsi na pia meya kuchaguliwa na wananchi badala ya baraza la madiwani.

Hii inatoa nafasi kwa wananchi wote kuwa na nafasi ya kuchaguliwa kuongoza mkoa au wilaya.

3. Ntazifanzia mabadiliko sekta za Elimu, Afya, Jamii, Uhamiaji kwa kuwapa kazi hio wataalamu waliosomea mambo hayo ambao wapo tu wanasoma magazeti kila siku asubuhi maofisini. Ntataka waje na mawazo yao ingawa na mimi ntakuwa na mawazo yangu ambayo ni kama ifuatavo:

(a) Katika elimu ntapenda nione kila mtoto wa kitanzania anaefikisha umri wa mwaka mmoja, anaanza shule ya awali na walimu wanakuwa wapo wameandaliwa. Pia kila mtoto ambae amefikisha umri wa kuanza darasa la kwanza anafanza hivo na ntataka mtoto yoyote akifikisha umri wa miaka 14 tayari anajua kila kitu kuanzia kusoma,kuandika na ntatilia mkazo katika hisabati na Kiingereza.

Ikumbukwe kuwa baadhi ya watoto wanapomaliza shule ya msingi bado wanakuwa ni mambumbumbu. Kwa hio kuanzia umri wa miaka 14 hadi 19 mtoto yoyote yule tayari anakuwa amekwishajulikana ana kipaji gani na ni namna gani ya kumuendeleza iwe katika sayansi, ufundi na mengine kwa hio inabaki kumpa nafasi ya kuwa mtaalam katika fani yake kupitia vyuo na shule maalum.

(b) Katika sekta ya Afya ntahakikisha kwamba madaktari wote waliosoma nje ya nchi wanapokuja nyumbani likizo basi tunahitaji msaada wao wa kitaaluma hasa katika maeneo ambayo kumuona daktari ni taabu. Kwa mfano daktari anaishi na kufanza kazi Ujerumani lakini kazaliwa Kisiju Pwani, basi hata kama ana nyumba mbezi tutampa kiwanja ajenge Kisiju Pwani ili awe karibu na wananchi wenzie. Pia wale ambao wamestaafu basi serikali itaingia mkataba nao ili kusadia jamii za watanzania.

(c) Sekta ya jamii, hili ni tatizo mahala popote duniani na hata Marekani ambako wameendelea ni kwamba kama hukuweka akiba ulipokuwa unafanza kazi basi utakuwa na matatizo pale utapohitaji msaada (nafikiri umetazama movie ya John Q).

Kwa hio ntahakikisha kila mtu ambae amejiajiri anachangia mfuko wa pensheni ili fwedha zile zimsaidie pale anapopata dharura na anapostaafu kufanza kazi. Kwa maana moja au ingine ntajitahidi kubuni njia mbalimbali za kuwawezesha watu kufanza kazi na kupata revenue kupitia kodi mbalimbali.

(d)Kuhusu sekta ya uhamiaji ntahakikisha kwamba kila mtoto anaezaliwa katika ardhi ya Tanzania anajulikana kwa kuweka kumbukumbu ambayo itasaidia ku-balance allocation ya resources kama elimu na afya kwa mtoto huyo (nafikiri unanifahamu hapo). hapa ntakuwa najaribu kuzuia raia wasio watanzania kufaidi mambo ambayo ni kwa watanzania tu isipokuwa kama baba na mama au mmoja wao ana uraia wa Tanzania.

Hapa namaanisha kwamba watu wote wasio raia wa Tanzania wanakuwa "second" kwa watanzania katika kupata "resources" kama elimu, ajira, makazi na kadhalika.

Hayo ni baadhi ya maeneo ambayo ninaona yahahitaji mabadiliko ya haraka ingawa kuna maeneo mengine kama biashara na viwanda, usafiri na usafirishaji ambayo ningeyatia katika awamu ingine tuchukulie ninapewa awamu mbili.

Ntaelezea namna ya kubadili maeneo haya kadiri tunavoendela kujadiliana.

NB:

Mimi sio mwanasiasa lakini napenda mabadiliko yawe ya kisayansi zaidi.

Ahsante.
 
in short, mimi nitaanzia kwny kuadopt kiasi sera ya chadema ya majimbo,
Huko gavana/mbunge au mtu wa aliepigiwakura nao ndio atakuwa mwisho wa mambo yote atakuwa kwa kifupi rais, kama rais wa zanzibar,
huko majimboni, wataamua kuwa na dizaini yoyote ya muundo, ilimradi kwa kupiga kura.
% ya pato itapelekwa serikali kuu.
Hapo rais wa nchi ndio ataamua abajeti vipi pato hilo yeye na mawaziri wake wa kuteuliwa nae, kama kusaidia majimbo masikini au kusafiri poa tu.
jimbo litaendeleza elimu, mila, priorities kutegemea na uamuzi wao.
**
Elimu kwa watoto wadogo (1.5 yrs - 5yrs) ni muhimu sana ndio ya kuipa kipaumbele, walimu wake wawe wataalamu kweli na shule zijulikane na zihakikiwe zote, sio watoto kupoteza miaka yao muhimu wakikaririshwa tu goodmorning teacher, mwalimu ni house girl wa mwenye shule, kasoma short course miezi mitatu baada ya kupika miaka 7.
 
..........kama ungepata nafasi ya kuibadili Tanzania ya leo ungefanya nini?...[/QUOTE]

Swali gumu hilo!
Ila la linatia hamasa kujibu kwani nadhani kwa walio wengi humu JF nia kubwa ni kubadili hari halisi ilivyo katika Tanzania yetu ya leo,Kiuchumi,Siasa na Kijamii.
Lakini swali lako liko so vague kwani halina base(do not get me wrong here),kwa maana Tanzania yaleo kila kitu katika nyanja hizo tatu haziko sawa.

Ila kama swali lilivyo ndivyo basi KWA HAKIKA KABISA NINGEKATAA HIYO NAFASI labda uliweke hilo swali vizuri zaidi.
Na kama ningelazimishwa kwa hiyo nafasi basi,KUTOKA na hali halisi ya Elimu na kukua kwa UFAHAMU WA WATANZANIA(kuhusu nchi yao na neema zote zilizomo na plus hizo nyanja tatu hapo juu) nchii hii ningeibadili kwa kufata Mlengo wa KINYERERE (siasa za ujamaa na kujitegemea)labda nahizo kwa wakati huu tunaweza kufika mahara tukawa nchi iliyo endelea.
 
Meku ni swali gumu lakini zuri
Nianze kwa kurejea Ze Comedy iliyorushwa jana.Kwenye session ya burudani waliimba wimbo mmoja wa dini usemao "natamani nchi mpya".

Mantiki ya wimbo ule ni paradiso kwa maana ya maisha mapya baada YA KIFO.Hata hivyo maelezo ya mzee wa "bonyee" kabla ya wimbo kuimbwa yalinigusa sana.

Alisema kuwa yeye binafsi anatamani sana kuiona nchi ya tofauti na tanzania ya leo.Nchi ambayo vijiji vyake vina barabara nzuri,hospitali,umeme n.k.Tena akaendelea kusema angetamani kuiona nchi isiyokuwa na mafisadi,yenye viongozi wenye kuwathamini wananchi wao...

Nimenukuu maelezo hayo kuonesha uhalisia na umuhimu wa swali lako kwa kila mtanzania.Kila mtu anatamani kuiona tanzania mpya,tofauti na hii tuliyonayo yenye harufu ya ufisadi,njaa,umasikini na kukata tamaa.

Mimi kama raia mwema mwenye uchungu na tanzania siku zote nimetumia nafasi yangu na bado nitaendelea kutumia nafasi yangu kuitendea Tanzania yafuatayo:
a)Kuwa mstari wa mbele kuikataa rushwa kwa nguvu zangu zote
b)Kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa uvivu ni adui wa maendeleo popote.
c)Kuonesha njia kwa wengine pale nilipo kwa kukemea maovu.

Hata hivyo haya yote yamefanywa na yanafanywa lakini matatizo yako palepale.Kama kila raia wa nchi hii akiweka maslahi ya taifa mbele hakika tutafika tunakotaka kwenda.

Hebu fikiria kama leo akitokea kiongozi wa ngazi ya juu ambaye hatawaonea aibu mafisadi na kuwafyekelea mbali bila kujali mahusiano yao,na maofisini nako kila mtu akawa adui wa rushwa,uvivu na uzembe.Yaani kil mtu akawajibika kwa nafasi yake,kuanzia kiongozi mpaka mwanafunzi wa chekechea.

Hatutaiona Tanzania ya leo baada ya miaka michache.barabara mbaya ambazo leo zipo mpaka katikati ya miji kama posta(dar)hazitakuwepo,hospitali na zahanati zitajengwa kila kona,umeme hautakuwa anasa tena,elimu yetu itakuwa ya kiwango cha juu,tutafaidi rasilimali zetu kamaMungu alivyokusudia.

Hii ndiyo Tanzania ninayoiota kila uchwao,ninajitahidi kuijenga kila siku lakini tuu wachache wenye kuliona hilo na kuliwazia hilo.
 
(1) sheria mpya ya vyombo vya habari na uhuru wa kusema
(2) ningefuta usalama wa taifa maana hawana kazi kwa sasa bali ni hasara na kula rushwa tu
(3) katiba mpya
(4) adhabu ya ufisadi itakua ni kunyanga
 
Back
Top Bottom