Elections 2015 If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

Wanabodi,

John Pombe Magufuli ndiye Mahundi wa urais Tanzania kwa mwaka huu wa 2015-2025!, Kuna walioshindana naye, waliopingana nae, na waliopingana nae!. Kuna msemo usemao, "if you can't beat them, join them!".

Maria wito kwa wote walioshindana nae, kwanza kukubali matokeo, Pili kumpatia ushirikiano kwa ku join him.

Wakati wa mchaka to wa kumpata mgombea wa CCM nilipandisha uzi huu, kuhusu baadhi ya wagombea wa CCM wakipita wana hatari ya ku make the worst Dictators, John Pombe Magufuli was number 2 ya Rais who can make the worst dictator this country has ever had!.

Hoja kuwa Magufuli ni dictator haina mjadala, kitu cha muhimu ni kumuombea tuu kwa Mungu, angalau amfanye ni a benevolent one, vinginevyo tutajuta!.

Jakaya Kikwete ukiondoa mambo yake ya Kikwete ya uswahili Swahili, alikuja ni mtu mwenye huruma iliyooitiliza kiasi cha kutafsiriwa ni Rais dhaifu, hivyo CCM ya Kikwete ilikuwa ni CCM dhaifu!, CCM ya Magufuli itakuwa ni CCM sasa kazi tuu, ambayo ni hatari kwa waliozoea CCM lege lege, hivyo akijenga CCM imara sana, huu upinzani mwisho ni 2020!.

JK tumemchekea, tumemdhihaki, tumembeza, tumemkejeli, hadi kumchezea, yeye akicheka tuu na kuwaacha yapite. Kwa Magufuli, hakuna kucheka, wala hakuna mchezo, ni kazi tuu, hivyo hili ni angalizo muhimu sana na hata majaaliwa ya huu Uhuru tulionao humu jf mbele ya unpredictable dictator, ni mashaka matupu unless we join them!.

Thanks God, mimi ni mmoja wa wachache, wanaojua huyu Magufuli aliibukia wapi hadi yeye kuwa ndie mgombea wa CCM na sababu ni zipi!. Hivyo let's hope, only zile sababu, zilizopelekea kwa nini ni Magufuli, ndio the only ones zitakazo mcheck and balance him in between being a real dictator and a benevolent dictator, so to be on a safe side, if you can't beat them, just join them!.

Wana Chadema, Wana UKAWA na Watanzania wenzangu, najua wengi wetu tulimtaka Lowassa, tumemkosa!, tukapewa Magufuli, let's just take him!. If you can't get what you want, just take what you get!.

Sio tumjoin kwa sababu ndio tumemkubali, au kwa sababu ndio sasa tunampenda, no way, we have to join them because we have to!.

Pasco!.

Andika vizuri.
 
Aaagh unamuita kilaza aaagghh basi tumia usafiri wa anga maana barabara za kilaza zitakumeza.

Nyie ndio mnaoshinda mnakulwa rushwa kutumikia wananvhi sasa mnalo.

Kama vile hizo barabara hazimezi watu sasa hivi......

Unakumbuka ile ajali ya basi kutokana na shimo la barabarani, kwenye barabara 'mpya'?
 
Tusitishane hapa. Akiwa rais afanye kazi kwa mujibu wa katiba. Hii habari ya kunyenyekea binadamu mimi huwa sina & inanichefua sana. Kila mtu ataendelea na majukumu yake, tofauti ni kuwa wengine ni viongozi na sisi ni raia wa kawaida.
 
The prospect of CCM being in power for almost 60 years makes me sick to my stomach!

Not only that.

The fact that Magufuli is the least qualified of all past CCM presidential nominees and therefore the likely next president for the next 10 years is hard to bear and unforgivably cringeworthy!

You real make sense brother
 
Trust me! Ikiwa Magufuli atabahatika kushinda, basi ndiye atakayeifuta CCM kwenye ramani ya siasa za Tanzania! Kwa ufupi ni kilaza na wanaotarajia jipya kutoka kwake watavunjika moyo kupita kiasi!! Kazi ya urais siyo kukesha site kutafuta ujiko kwa makelele na kujipa ubora miongoni mwa wenzako!! Kumbuka kuwa urais ni kuongoza hivyo kila dosari unatupiwa wewe!! Sielewi na nasema tena sielewi imani ya watu kwa Magufuli ni yale makelele au kwenda kuchukua nyundo kugongagonga lami au kwenda kwenye mzani wa Kibaha au kutaja idadi na takwimu au kupiga makelele!

Ukijifanya mbabe kwenye urais wakati nchi yako ni masikini wakubwa watakubana tu! Ukiwa kilaza wa kushindwa kubuni mbinu za kuondoa umasikini imekula kwako!! Magufuli ana mbinu gani???

we pimbi kweli...!!!
 
The prospect of CCM being in power for almost 60 years makes me sick to my stomach!

Not only that.

The fact that Magufuli is the least qualified of all past CCM presidential nominees and therefore the likely next president for the next 10 years is hard to bear and unforgivably cringeworthy!

Sijui hizo takwimu umezitoa wapi, na sijui ina vigezo gani...

Lakini yawezekana kuwa ni hisia tu, hivyo sio fact!!
 
kama Nyerere na kina Kambona wangekua na mawazo hayo basi leo tungekua chini ya wakoloni....yaani wewe huna msimamo ni bendera fuata upepo...siku zote jasiri husimamia unachokiamini mfano mzuri ni Maalim Seif kwa miaka 20 bado anapigania haki za watu wake...
 
Mimi ndio nimekuuliza, ina takwimu/vigezo gani kuona kuwa mgombea wa ccm wa mwaka huu ni "least qualified"...

Sihitaji takwimu wala vigezo vyovyote vile kuona kuwa mgombea wa CCM wa mwaka huu ni bomu kwa sababu hayo ndiyo maoni [ninavyoona] yangu.

Halafu wala hukuuliza. Umetoa kauli tu.

Sasa nikuulize wewe: unajua tofauti ya kauli na swali?

Manake uliandika hivi: "Sijui hizo takwimu umezitoa wapi, na sijui ina vigezo gani..."

Unasema wewe ndiyo umeniuliza. Ulipouliza ni wapi hapo?

Unauliza swali kwa kuandika "Sijui hizo takwimu umezitoa wapi, na sijui ina vigezo gani..."?

Na kwa nini nihitaji takwimu kuona kwamba Magufuli ni bomu?

*Ona jinsi ambavyo maswali huulizwa.*
 
Hukusema kuwa ni maoni yako, rudi kwenye bango lako ujisome tena. Labda kwa vile kingereza changu sio kizuri, lakini kwa uelewa wangu ulifanya generalization, kitu ambacho sio kizuri(kwa maoni yangu).

Kuuliza sio lazima uweke alama(?), maelezo tu kama yangu yanaweza kutosha kuwa swali na likahitaji majibu.

Ili kuthibitisha kauli yako, ni vizuri kutoa vigezo/maelezo ili kulinda hoja yako, kwa nini Magufuli unamuona "least qualified"? Hilo umeshindwa/hutaki kunijibu.
 
Hukusema kuwa ni maoni yako, rudi kwenye bango lako ujisome tena. Labda kwa vile kingereza changu sio kizuri, lakini kwa uelewa wangu ulifanya generalization, kitu ambacho sio kizuri(kwa maoni yangu).

Kuuliza sio lazima uweke alama(?), maelezo tu kama yangu yanaweza kutosha kuwa swali na likahitaji majibu.

Anhaa...kama ambavyo kuuliza si lazima umalizie kwa kuweka alama ya kuuliza baada ya sentensi basi hata kutoa maoni yangu si lazima nianzie au kumalizia kwa kuandika 'haya ni maoni yangu'.

Ili kuthibitisha kauli yako, ni vizuri kutoa vigezo/maelezo ili kulinda hoja yako,

Sihitaji kuthibitisha kauli ya maoni yangu kwa sababu maoni yangu ni yangu na yanabaki kuwa yangu. Kama hukubaliani nayo, basi unakaribishwa kufanya hivyo.

Lakini mimi silazimiki kuyathibitisha hata kidogo.

kwa nini Magufuli unamuona "least qualified"? Hilo umeshindwa/hutaki kunijibu.

Sijashindwa kulijibu. Nimekujibu lakini pengine jibu langu si jiibu ambalo unalitaka wewe.

Sorry, can't help you with that.
 
Tatizo lenu mlifikiri nchi hii wapiga kura ni madereva wa bodaboda peke yao. Mkawapa na viroba ili wakatukane na kuzomea nguo za kijani. Kwa sasa sijui watajificha wapi. Acheni siasa za Ghilba na uongo. Watanzania wanaujua uongo wakiusikia. wewe umeahidi kila kitu buree na bado ukapoteza its a shame!!
 
Anhaa...kama ambavyo kuuliza si lazima umalizie kwa kuweka alama ya kuuliza baada ya sentensi basi hata kutoa maoni yangu si lazima nianzie au kumalizia kwa kuandika 'haya ni maoni yangu'.
..Hata mimi sijasema popote kuwa ni "lazima" uandike hivyo. Lakini katika uandishi, maneno kama "nadhani, nafikiri, naamini" hutumika kuonyesha kuwa alisemalo mhusika ni maoni binafsi, anaposema "ni ukweli usiopingika, takwimu zinaonyesha" hii humaanisha kuwa ana uhakika toka vyanzo vilivyothibitishwa kisheria au kitakwimu.

Sihitaji kuthibitisha kauli ya maoni yangu kwa sababu maoni yangu ni yangu na yanabaki kuwa yangu. Kama hukubaliani nayo, basi unakaribishwa kufanya hivyo.

Lakini mimi silazimiki kuyathibitisha hata kidogo.

Sijashindwa kulijibu. Nimekujibu lakini pengine jibu langu si jiibu ambalo unalitaka wewe.

Sorry, can't help you with that.

Nimekusoma kiongozi!!
 
..Hata mimi sijasema popote kuwa ni "lazima" uandike hivyo.

Naam, hata mimi sijasema kuwa wewe umesema kuwa ni 'lazima' kuandika hivyo.

Lakini katika uandishi, maneno kama "nadhani, nafikiri, naamini" hutumika kuonyesha kuwa alisemalo mhusika ni maoni binafsi,

Hiyo ni kweli. Lakini kumbuka kwamba humu ndani si mara zote watu hufuata kanuni za uandishi hususan pale ambapo tunapokuwa tunachangia maoni yetu. Na ndo maana wakati mwingine unaweza ukaona mtu kaliandika jina la mtu fulani kwa herufi zote ndogo, kaandi kwa kutumia mikato, kaweka 'x' badala ya 's' na kadhalika.

Kwa hiyo, nami nilipokuwa naandika yale, nilifanya hivyo kama mtoa maoni tu juu ya kile kilichokuwa kimeandikwa na mwanzisha mada. Sikuwa naandika makala rasmi wala sikuwa naandika kuhusu habari.

Setting ya humu, hususan kwenye uchangiaji mada, ni informal. Wakati mwingine watu tunatiririka tu bila kufuata kanuni za uandishi zinazotumiwa kwenye formal setting.

Sasa, unless mtu uwe unataka ligi tu kwa kutafuta kasoro katika mabandiko ya wengine [jambo ambalo hata mimi nakiri huwa nalifanya hapa na pale], lakini kwa kiasi kikubwa watu huwa tunachangia mada kwa kutoa maoni yetu ambayo mengine kwa kweli huwa hayana misingi yoyote katika ukweli au uhalisia kama wa takwimu, na kadhalika.

anaposema "ni ukweli usiopingika, takwimu zinaonyesha" hii humaanisha kuwa ana uhakika toka vyanzo vilivyothibitishwa kisheria au kitakwimu.

Kaka, ya humu yachukulie hivyo hivyo tu wakati mwingine. Kama ningekuwa naleta taarifa rasmi au naandika andiko rasmi basi nisingekuwa na budi ya kufuata hizo kanuni. Hilo nalitambua kabisa kwani hata mimi ni 'trained journalist', just in case you didn't know.

Nimekusoma kiongozi!!

Nami nimekusoma na nadhani sasa umenielewa.
 
Back
Top Bottom