If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! | Page 8 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 28, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndiye mshindi wa urais Tanzania kwa mwaka huu wa 2015-2025 and may be more!, anayesubiri tuu kutangazwa rasmi na kuapishwa. Nimesema 2015 -2025 sio kwa bahati mbaya as if hakuna uchaguzi 2020, no!, nimesema 2015-2025 kwa sababu huu ndio ukweli ninaouona mimi muona mbali ni kuwa kwa nature ya udikiteta huu wa Magufuli, kama hautakuwa countered through proper channels kupitia instruments zilizopo, then, mwaka 2020 hakutakuwa na uchaguzi wa rais wala uchaguzi wa vyama vingi!, bali litafanyika igizo tuu la uchaguzi, ambao utakuwa ni uchaguzi wa chama kimoja tuu CCM!. Uchaguzi mwingine wa vyama vingi wa rais na wabunge ni 2025 tena only if hatautumia udikiteta wake kubadili katiba kwa mlango wa nyuma, ili aendelee kama Mkuruzinza, Kagame, Museveni na Mugabe!.

  Kuna walioshindana nae ndani ya CCM, hawa ni washindani, kati nyao kuna waliopingana nae, hawa ni wapingani, kuna waliopigana nae vikumbo!, hawa ni wapigani, na kuna waliopingana naye kisiasa, hawa ni wapinzani. Kwa vile sasa mshindi ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hii inamaanisha, hao wengine wote who were fighting, they tried to fight him but couldn't beat him!, as a result thay lost, hivyo as of now, wote walioshindwa, are all are the looses!. Kwenye unrepresentative democracy, the winner takes it all, and the looser standing small!. Kura ni zile milioni 8 tuu!, zile milioni 6 is nothing!, ukiishashindwa unasimama pembeni, ama uendelee kulia na kuugumia maumivu ya kushindwa, au ukubali kushindwa, na kujipanga upya kwa mpambano unaofuata!.

  Kuna huu msemo wa wahenga usemao, "if you can't beat them, join them!". Nawashauri makundi hayo yote walioshindwa, kwanza kukubali kushindwa, kwani asiyekubali kushindwa sio mshindani, hivyo natoa mwito kwa washindwa wote, ku surrender kwa kuweka silaha zao chini na to join him, sio kwa kupenda, but they have to join him because, there is no any other way out, or any options but they have either to join him or to fall out!, hiyo ndio salama yao wakati wa kusikilizia kama atakuwa dikiteta kweli au a benevolent one!. Akiwa dikiteta kweli usipomjoin, umekwisha!, hivyo Tanzania tunaelekea kwenye totalitarian nakurudi kuwa nchi ya chama kimoja!. Hata akiwa a benevolent one, bado upinzani hatafurukuta hata kule kwenye ubunge na udiwani, wapinzani wataokarudi bungeni 2020 ni by personal merits only, as of now, namuona mpinzani mmoja tuu mwenye uhakika wa kurejea bungeni 2020, huyu ni ZZK pekee, wapinzani wewngine wote ni majaaliwa!.

  Wito huu wa kumjoin Magufuli, unatolewa regardless umeshindwaje!, iwe ni kwa ushindi halali, ushindi haramu, bao la mkono, etc, etc, kwenye uchaguzi, the end will always justify the means!, mshindi ni Magufuli, sasa tumpatie tuu kila aina ya ushirikiano wa kutosha kwa kum join himn ili aweze kulitawala viruzi taifa letu hili.

  Tena hapa mtawashuhudia baadhi ya wale ma-opportunists waliojiengua CCM kumfuata Edward Lowassa upinzani, wakitumaini Lowassa angeshinda lakini kwa vile Lowassa ameshindwa, na CCM ndio imeshinda, they see no more opportunities in Chadema, mtawashuhudia wakipiga magoti na kulamba matapishi yao kwa kurejea CCM, because walijiunga upinzani just in search of opoortunities tuu, now they see no more opportunities they expected kwenye opposition, hivyo watajilambia tuu matapishi yao na kujirejeleza zao nyumbani kwao CCM kama alivyofanya mwana mpotevu, na watapokelewa kwa shangwe hadi wengine kufanyiwa karamu!.

  Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM nilipandisha uzi huu,
  Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5,

  Makundi hayo ni ..."The Top Ten who can make the worst dictators
  Kundi la 8: The Top Ten who can make the worst dictators
  Nikizungumzia kuhusu baadhi ya wagombea urais wa CCM, wakipita wana hatari ya ku make the worst dictators, John Pombe Magufuli was number 2 ya Rais who can make the worst dictator this country has ever had!.


  Hoja kuwa Magufuli ni dictator haina mjadala, kwa watu wenye jicho la tatu, wanaona the fire on his eyes, and then fear is the weapon on his heart kwa kutoa hotuba za ukali kama agamba!, ambayo ni kiashiria cha seriousness ya hasira ambayo inaweza kugeuka chuki na kupelekea visasi toka moyoni mwake, kwa kila atakayetofautiana naye!, na wenye sikio la tatu wanaisikia tone ya ukali wa ukatili kwenye sauti yake!, hii ni ishara kuwa huyu sio mmtu wa masaihara, watakaotofautiana nae, wanaweza kuumia au hata ...(God forbid). Kitu cha muhimu sana cha kufanya kwa sasa ni sisi waote Watanzania, katika umoja wetu, kumuombea tuu kwa Mungu, very seriously angalau Mungu amfanye kuwa ni a benevolent one ili huo udikiteta wake ulisaidie taifa kusonga mbele kiuchumi na kiustawi at a price of dead democracy!, vinginevyo akiwa the real one, tutajuta!.

  Jakaya Kikwete ukiondoa mambo yake ya uswahili swahili, alikuwa ni mtu wa watu, ni mtu mwenye huruma sana iliyopitiliza kiasi cha kutafsiriwa kuwa Kikwete alikuwa ni Rais dhaifu, hivyo CCM ya Kikwete ilikuwa ni CCM dhaifu! hivyo Kikwete alibezwa, alitukanwa, na kufanywa CCM ya mchezo mchezo, lakini CCM ya Magufuli itakuwa sio CCM ya mchezo mechezo, au CCM ya huruma huruma, itakuwa hakuna mchezo wala mswalie Mtume, hii CCM ya hapa kazi tuu!, CCM imara ni kitu hatari sana kwa majaaliwa ya upinzani!.

  Upinzani Tanzania umeweza kushamiri kutokana na CCM lege lege, hivyo Magufuli akijenga CCM imara, huu upinzani lege lege uliopo nchini Tanzania hivi sasa, mwisho wake utakuwa ni 2020, Tanzania tunarudi kule kule kwenye nchi ya chama kimoja!. Ndio maana nimesema 2020 hakuna uchaguzi wa rais kutafanyika tuu igizo la uchaguzi!.

  Kwenye uzi wangu huu,
  Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour!, nilimzungumzia JK kuwa sifa kubwa iliyomfanya CCM impitishe ni cheko na bashasha zake!, hivyo JK tumemchekea, tumemdhihaki, tumembeza, tumemkejeli, hadi kumchezea sharubu kama babu na wajukuu zake huku yeye akicheka tuu na kuyaacha yapite. Lakini kwa Magufuli, sijui kama kutakuwepo kuchekacheka au kuchekeana, kubezana na kuchezeana, na kubembelezana, kwa Magufuli ni mambo serious kwa kwenda mbele na hakuna mchezo mchezo, ni kazi tuu!.

  Wajameni japo kwa sasa naongea kama utani au mzaha, lakini hili ni angalizo muhimu sana kwa majaaliwa ya freedom of expression, freedom of speech, na freedom of press ya uhuru huu usio na mipaka tulionao sasa nchini mwetu, tukiwemo sisi humu jf, tulio enjoy wakati wa Kikwete, lakini mbele ya unpredictable dictator kama Magufuli, kiukweli kabisa huko tuendako, kama hatabadilika, then ni mashaka matupu!, salama yetu hata sisi jf pia ni tumjoin him kwa kumsifu kwa nyimbo na mapambio, vinginevyo....

  Thanks God, mimi ni mmoja wa wana jf wachache, waliopata priviledge ya kujua huyu Magufuli aliibukia wapi na ilikuwaje kuwaje hadi akawa ndie akawa mgombea wa CCM na sababu ni zipi zilifanya awe ni yeye. Ukilisoma bandiko hili ukazijua sababu zilizosababisha akawa Magufuli, labda utanielewa nazungumzia nini!.
  Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli!

  Hivyo kwa nature na hulka ya udikiteta wa Magufuli, let's hope, kuwa zile sababu zilizopelekea kuwa mgombea wa urais wa CCM ndizo pekee (the ones and only) zitakazo weza kumcheck and balance him in between being a real dictator and a benevolent dictator vinginevyo hata hao CCM wanaoshangilia ushindi kwa sasa, akitokea kuwa a real one, hata CCM wenyewe nap watakuja kujuta!, therefore, to be on a safe side, it's better if you can't beat them, just join them, to be on a safe side!.

  Wapinzani wote wakiwemo wana Chadema, wana UKAWA, na Watanzania wenzangu kwa ujumla, najua wengi wenu mlimtaka Lowassa, mmemkosa!, na badala yake mkapewa Magufuli, hivyo natoa wito wa "If you can't get what you want, just take what you get!", ukikosa ulichotaka, then pokea ulichopewa!, tumkubali Magufuli kwa moyo mkunjufu, hivyo hivyo alivyo na udikiteta wake, tumpokee na kumpatia kila aina ya ushirikiano wote unaohitajika kumuwezesha kuiongoza vema na sala hii Tanzania yetu. Tanzania sio nchi ya Magufuli wala Tanzania sio mali ya CCM, Tanzania ni ya Watanzania wote, ni nchi yetu sote, hivyo it can be done kama kila mmoja wetu will play his part!.

  Sio tumjoin Magufuli kwa sababu sasa ndio tunampenda hivyo tumemkubali, no way, tumjoin Magufuli kwa kumkubali ndie the only one rais tuliyepatiwa na Mungu, hivyo we have duty and a responsibility to join him kwa lazima, tutake tusitake, tupende tusipende, yeye ndie rais wetu hivyo we have to join him and support him because we have to!.

  Kwa kuweka tuu kumbukumbu sawa, hata mwaka 2010 Chadema waliposhindwa, walisusia matokeo walijidai kunsusa na kujidai hawamtambui JK, lakini hatima yake ilikuja kuwa hivi

  Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza!

  Bandiko hili liliwaudhi sana Chadema humu jf, Mwana JF, Regia Mtema (RIP) akanitaka niombe radhi
  Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya ....

  Radhi iliombwa
  Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya ...

  This same, same scenario inataka kujirudia kwa Chadema na Ukawa kujidai kutaka kumsusia Magufuli!. Kuna vitu mtu unaweza kususa na kuna vitu huwezi kususa!,kwa hata 2010 Chadema walisusa lakini tukawashuhudia makamanda wakifakamia chai, juice na vitafunwa vya ikulu, huku meno 32 nje kwa vicheko, hivyo hata awamu hii ya Magufuli, msije kushangaa Mbowe akiwaongoza tena makamanda, akiwemo Lowassa kubisha hodi ikulu na kumpongeza Magufuli.

  Paskali
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #141
  Aug 7, 2016
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 13,081
  Likes Received: 6,869
  Trophy Points: 280
  Brother ...jicho lako ni hatari. Utabiri wako wa 2020 upinzani utakuwa kwenye hatari kubwa naona dhahiri linaenda kutokea labda yafanyike mabadiliko makubwa. Wengine tunachukiwa kwa kusema ukweli huu. Tunataka upinzani imara lakini upinzani wanaishi kwa kusubiri huruma ya Rais aliyeko madarakani na kwa umri wote wa upinzani wameshindwa kujiwekea misingi muhimu kukamata dola.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #142
  Nov 25, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Kama taasisi ya umma inayojua thamani ya pesa imefungua FD ili fedha hizo zizae na kuongezeka imehukumiwa kifo, then nasisitiza tuzidishe maombi kwa Mungu amjaalie rais wetu Magufuli afunguke macho ya kiuchumi aone mwanga, vinginevyo. ..

  Paskali
   
 4. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #143
  Nov 25, 2016
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,466
  Likes Received: 6,778
  Trophy Points: 280
  Ni majanga sana...sasa alitaka watu wafanyeje? watu wamekuwa creative kuirahisishia serikali...Mimi nadhani tuna tatizo kubwa sana...huyu mtu huyu sidhani kama anashaurika....

  Uchumi wetu anauua huyu mtu alafu tunamwangalia tuuuu
   
 5. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #144
  Nov 25, 2016
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,466
  Likes Received: 6,778
  Trophy Points: 280

  Mkuu..zaidi ya kulalamika ume play part gani kuleta hayo mabadiliko..ujue mimi na wewe tunapishana sehemu moja...wewe ni mfuasi wa mtu sio wa itikadi...ndio maana umebaki kama mwanamke aliyeachwa na mumewe ilihali bado anampenda
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #145
  Nov 25, 2016
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,139
  Likes Received: 22,410
  Trophy Points: 280

  Leo hujavuta bangi!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #146
  Nov 25, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Mkuu Dada yangu Faiza, mimi sivuti bangi ila imetokea tuu wengine akili zimekaa kibangi bangi hadi kudhaniwa tunavuta bangi, ila nakiri kwenye ujana niliisha ijaribu na humu jf nimewahi kuitetea iruhusiwe kwa wale ambao bangi inawatuma vizuri.

  https://www.jamiiforums.com/threads/moral-question-morphine-drug-iruhusiwe-kupunguza-maumivu-makali.

  Ila pía sikuitetea bangi peke yake, bali pía nimeitetea ile biashara ya profesionalprofesion yako nayo ihalalishwe.

  https://www.jamiiforums.com/threads/opinion-is-it-not-its-high-time-tanzania-tuhalalishe-the-oldest-profession.

  Paskali
   
 8. Kibao

  Kibao JF-Expert Member

  #147
  Nov 27, 2016
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 633
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 80
  Rukwa?????
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #148
  Mar 12, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Najikumbusha tuu nilisema nini in light ya hiki kinachotokea CCM sasa. Wenye uwezo wa kudetect tone ya visasi watakuwa wameona!. 2020 hakutakuwa na uchaguzi wa rais bali igizo la uchaguzi na CCM imara, majaaliwa ya upinzani ni mashakani sana! .

  Paskali
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #149
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  In light ya muongozo uliotolewa leo pale Ubungo kuhusu majadiliano kwenye mitandao ya kijamii, tunatakiwa tusi discuss watu, tudiscuss ideas, hivyo nashauri kuanzia leo tusizungumzie kabisa mtu yoyote kuwa dikteta bali tusizungumzie udikteta tuu na sio watu.

  Paskali
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #150
  Mar 23, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Tetesi: - Trend Reading: Mabadiliko Madogo ya Baraza la Mawaziri Yananukia!. Head-hunting Imeishaanza!.
  Magufuli kiboko!.
  Any way, Kabudi ni jembe, na Mwakyembe ni mwanahabari.
  Jina la Nape limeandikwa kwenye kitabu cha majina ya mashujaa wa taifa hili, na uwaziri sio kitu mbele ya karma!.
  Paskali
  Kuna vitu niliwahi kusema siku nyingi, sasa naanza kuvishuhudia little by little!.
  We are doomed!.
  Paskali
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #151
  Jul 19, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Hii ni mbolea kwenye hoja za udikiteta

  Paskali
   
 13. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #152
  Oct 3, 2017
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 8,155
  Likes Received: 6,541
  Trophy Points: 280
  Ukifuga kuku kuna vitu anavyofanya vilivyo tofauti na kufunga ng'ombe au mbwa. Vivyo hivyo kujiita (kuwa) binadamu kuna vitu unavitarajia kutoka kwa kiumbe huyu vilivyo tofauti na viumbe wengine. Tunachofanya sisi ni kudharirisha ubinadamu!
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #153
  Dec 13, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Kwenye hoja ya udikiteta wa rais Magufuli, kuna madikiteta wabaya na madikiteta wazuri au madikiteta wema.
  Madikiteta wazuri ni wale ambao wanafanya vitendo vya udikiteta kwa nia njema, hata ikibidi kuivunja katiba, au kukiuka sheria, taratibu na kanuni, kwa nia njema, ni udikiteta unaokubalika, mfano katiba inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano, rais Magufuli anataka watu wafanye kazi na sio kuwa wazururaji kwa kisingizio cha kufanya maandamano, au kuwa ni watu wanaokaa bure tuu kwa kisingizio cha kuhudhuria mikutano ya siasa, watu wenye muda wa kuhudhuria mikutano ya siasa kila siku ni watu wasio na kazi, hivyo kama tangazo lake la kupiga marufuku mikutano ya siasa na maandamano ni ili watu wasizurure ovyo, na wasikae onyo bila kufanya kazi, then huu ni udikiteta mzuri. Dikiteta wa aina hii anaitwa a benevolent dictator.

  Hata kuachiwa kwa Babu Seya, sheria hairuhusu wabakaji na wauwaji kuachiliwa kwa msamaha wa rais, kilichofanyika pia ni udikiteta, ila umefanywa kwa nia njema kuwa vipindi walivyotumikia gerezani, wamejirekebisa, na sasa ni watu wema, hivyo udikiteta is not necessarily ni udikiteta mbaya, udikiteta mwingine ni udikiteta mzuri.

  Big up sana rais Magufuli.

  Paskali
   
 15. Antonio Conte

  Antonio Conte JF-Expert Member

  #154
  Dec 13, 2017
  Joined: Dec 6, 2017
  Messages: 275
  Likes Received: 310
  Trophy Points: 80
  Wewe inabidi tuoongee kisukusu ndo tuaelewana....

  Kinyume cha dictator ni nini???
   
 16. LebronWade

  LebronWade JF-Expert Member

  #155
  Dec 13, 2017
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,619
  Likes Received: 1,040
  Trophy Points: 280
  Mkuu tukienda kwa utashi wa mtu mmoja mmoja hivyo nchi itakua banana republic..ndio maana kuna katiba...utashi wa Magufuli kwa muono wake anaweza ona sahihi ila kwa wengine sio sahihi,kipimo ni kipi?Hakuna kipimo kingine kuacha katiba

  There is a reason katiba kuwepo na iheshimiwe.Binadamu anafanya makosa,Magufuli ni mwanadamu wa kawaida kabisa,kosa lake moja tu la bahati mbaya linaweza tukausha wananchi milioni 50.......

  Eti kuwaachia Babu Seya nalo ni jambo jema,hivi Paskali mzima kweli ndugu yangu?Mtu kadhibitishwa na mahakama zote ni mbakaji na mlawiti,kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka mahakama ya rufaa imedhibitisha hilo,wewe ni nani mpaka uje useme eti ni jambo jema?

  Mtu anaetetea udikteta wa aina yoyote ile decision making skills zake ni very suspect.

  Eti dikteta mzuri...ridiculous premise kabisa.......Watu mil 50 waishi kwa IQ very suspect ya mtu mmoja anaeitwa Rais?Itakua Tanzania kama jamii hatujafikia civilization stage collectively......Yaani mtu atoe maamuzi kuendesha watu mil50 bila kuwekwa kwenye scrutiny na peers wake ni hatari mnooo,ni hatari kama kulala na binti yako wa kumzaa.Tanzania kama civilization hatuwezi rudi nyuma kiasi hiki,ni insult to Tanzanians' intelligence

  Paskali kubali unakua academically dishonest na unatoa lip services kwa mtawala.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #156
  Dec 18, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Karibu pande hizi, haya yanayotokea leo, angalia akina sisi tulianza kuyaona lini!.
  Paskali
   
 18. i

  interconsult Senior Member

  #157
  Dec 21, 2017
  Joined: Dec 8, 2017
  Messages: 114
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Pascle usiwe mkata tamaa,siasa ni uga wa upepo. Upinzani unasoma yanayojili kwa mda huu hasa watu kuama kwa vishawishi. Genge la wanunuzi lingefanya mchezo huu januari ya 2020 naamini wangefanyikiwa san. Rushwa ya kisiasa sasa tanzania iko waz. Ushahidi wa waz wa akina nasari ni turufu nzur upinzan ukiitumia ku reverse ujinga wote huu. Wapinzan naiona their bright future kama watabadili gia ya kisiasa kufuatana na hali ya sasa. Bahati mbaya watesi wao hanawa uvumilivu.wanaweka silaha ya hela kununua watu mchana kweupe. Cku zote ukiona mtu anaalalisha kuungwa mkono na watu ujue kaishiwa sera. Msiogope utamaduni huu wa kununua watu utazoeleka mwishoni utakwisha na wasionunulika watawaumbua WANUNUZI. Tena wenye AUDIO CLIP za Maongez ya biashara hizo ebu rusheni hewani TUZIFANYE CALLER TUNE YA CM ZETU ili tuwakomeshe.
   
 19. x

  xaracter JF-Expert Member

  #158
  Dec 21, 2017
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 935
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 180
  Maishani kuna pande mbili za ubaya na wema utakuwa mwendawazimu kujiunga upande wa ubaya kwasababu tu wao ndio walioshinda,Hata kama kuna asilimia moja ya ushindi na tisini na tisa za kushinda .
   
 20. ChoiceVariable

  ChoiceVariable JF-Expert Member

  #159
  Dec 24, 2017
  Joined: May 23, 2017
  Messages: 1,483
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Ccm hii sio imara bali ccm ya dictator,ya Lisu yanaogopesha,,kwa dictator bora kumpenda kwa unafiki na kumsifu unaweza kuwa safe kuliko kumpinga,ameshasema takwimu ambazo hazina authority ya NBS marufuku,vinginevyo jela itamhusu mtu,hatari sana.
  "Natamani malaika ashuke afungie mitandao"
   
 21. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #160
  Jan 9, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,623
  Likes Received: 23,765
  Trophy Points: 280
  Hili la Lowassa kwenda ikulu, limewashangaza baadhi ya watu, kwetu sisi wengine ni kufanya tuu rejea, siku ya Mbowe Lema na Lissu na makamanda wengine kupiga hodi ikulu kumshukuru rais Magufuli na kumpongeza pia itafika, nawaomba msishangae!.

  Paskali
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...