If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! | Page 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 28, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndiye mshindi wa urais Tanzania kwa mwaka huu wa 2015-2025 and may be more!, anayesubiri tuu kutangazwa rasmi na kuapishwa. Nimesema 2015 -2025 sio kwa bahati mbaya as if hakuna uchaguzi 2020, no!, nimesema 2015-2025 kwa sababu huu ndio ukweli ninaouona mimi muona mbali ni kuwa kwa nature ya udikiteta huu wa Magufuli, kama hautakuwa countered through proper channels kupitia instruments zilizopo, then, mwaka 2020 hakutakuwa na uchaguzi wa rais wala uchaguzi wa vyama vingi!, bali litafanyika igizo tuu la uchaguzi, ambao utakuwa ni uchaguzi wa chama kimoja tuu CCM!. Uchaguzi mwingine wa vyama vingi wa rais na wabunge ni 2025 tena only if hatautumia udikiteta wake kubadili katiba kwa mlango wa nyuma, ili aendelee kama Mkuruzinza, Kagame, Museveni na Mugabe!.

  Kuna walioshindana nae ndani ya CCM, hawa ni washindani, kati nyao kuna waliopingana nae, hawa ni wapingani, kuna waliopigana nae vikumbo!, hawa ni wapigani, na kuna waliopingana naye kisiasa, hawa ni wapinzani. Kwa vile sasa mshindi ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hii inamaanisha, hao wengine wote who were fighting, they tried to fight him but couldn't beat him!, as a result thay lost, hivyo as of now, wote walioshindwa, are all are the looses!. Kwenye unrepresentative democracy, the winner takes it all, and the looser standing small!. Kura ni zile milioni 8 tuu!, zile milioni 6 is nothing!, ukiishashindwa unasimama pembeni, ama uendelee kulia na kuugumia maumivu ya kushindwa, au ukubali kushindwa, na kujipanga upya kwa mpambano unaofuata!.

  Kuna huu msemo wa wahenga usemao, "if you can't beat them, join them!". Nawashauri makundi hayo yote walioshindwa, kwanza kukubali kushindwa, kwani asiyekubali kushindwa sio mshindani, hivyo natoa mwito kwa washindwa wote, ku surrender kwa kuweka silaha zao chini na to join him, sio kwa kupenda, but they have to join him because, there is no any other way out, or any options but they have either to join him or to fall out!, hiyo ndio salama yao wakati wa kusikilizia kama atakuwa dikiteta kweli au a benevolent one!. Akiwa dikiteta kweli usipomjoin, umekwisha!, hivyo Tanzania tunaelekea kwenye totalitarian nakurudi kuwa nchi ya chama kimoja!. Hata akiwa a benevolent one, bado upinzani hatafurukuta hata kule kwenye ubunge na udiwani, wapinzani wataokarudi bungeni 2020 ni by personal merits only, as of now, namuona mpinzani mmoja tuu mwenye uhakika wa kurejea bungeni 2020, huyu ni ZZK pekee, wapinzani wewngine wote ni majaaliwa!.

  Wito huu wa kumjoin Magufuli, unatolewa regardless umeshindwaje!, iwe ni kwa ushindi halali, ushindi haramu, bao la mkono, etc, etc, kwenye uchaguzi, the end will always justify the means!, mshindi ni Magufuli, sasa tumpatie tuu kila aina ya ushirikiano wa kutosha kwa kum join himn ili aweze kulitawala viruzi taifa letu hili.

  Tena hapa mtawashuhudia baadhi ya wale ma-opportunists waliojiengua CCM kumfuata Edward Lowassa upinzani, wakitumaini Lowassa angeshinda lakini kwa vile Lowassa ameshindwa, na CCM ndio imeshinda, they see no more opportunities in Chadema, mtawashuhudia wakipiga magoti na kulamba matapishi yao kwa kurejea CCM, because walijiunga upinzani just in search of opoortunities tuu, now they see no more opportunities they expected kwenye opposition, hivyo watajilambia tuu matapishi yao na kujirejeleza zao nyumbani kwao CCM kama alivyofanya mwana mpotevu, na watapokelewa kwa shangwe hadi wengine kufanyiwa karamu!.

  Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa CCM nilipandisha uzi huu,
  Yajue Makundi 10 Top Ten wa CCM, Ambamo Watatoa Top 5,

  Makundi hayo ni ..."The Top Ten who can make the worst dictators
  Kundi la 8: The Top Ten who can make the worst dictators
  Nikizungumzia kuhusu baadhi ya wagombea urais wa CCM, wakipita wana hatari ya ku make the worst dictators, John Pombe Magufuli was number 2 ya Rais who can make the worst dictator this country has ever had!.


  Hoja kuwa Magufuli ni dictator haina mjadala, kwa watu wenye jicho la tatu, wanaona the fire on his eyes, and then fear is the weapon on his heart kwa kutoa hotuba za ukali kama agamba!, ambayo ni kiashiria cha seriousness ya hasira ambayo inaweza kugeuka chuki na kupelekea visasi toka moyoni mwake, kwa kila atakayetofautiana naye!, na wenye sikio la tatu wanaisikia tone ya ukali wa ukatili kwenye sauti yake!, hii ni ishara kuwa huyu sio mmtu wa masaihara, watakaotofautiana nae, wanaweza kuumia au hata ...(God forbid). Kitu cha muhimu sana cha kufanya kwa sasa ni sisi waote Watanzania, katika umoja wetu, kumuombea tuu kwa Mungu, very seriously angalau Mungu amfanye kuwa ni a benevolent one ili huo udikiteta wake ulisaidie taifa kusonga mbele kiuchumi na kiustawi at a price of dead democracy!, vinginevyo akiwa the real one, tutajuta!.

  Jakaya Kikwete ukiondoa mambo yake ya uswahili swahili, alikuwa ni mtu wa watu, ni mtu mwenye huruma sana iliyopitiliza kiasi cha kutafsiriwa kuwa Kikwete alikuwa ni Rais dhaifu, hivyo CCM ya Kikwete ilikuwa ni CCM dhaifu! hivyo Kikwete alibezwa, alitukanwa, na kufanywa CCM ya mchezo mchezo, lakini CCM ya Magufuli itakuwa sio CCM ya mchezo mechezo, au CCM ya huruma huruma, itakuwa hakuna mchezo wala mswalie Mtume, hii CCM ya hapa kazi tuu!, CCM imara ni kitu hatari sana kwa majaaliwa ya upinzani!.

  Upinzani Tanzania umeweza kushamiri kutokana na CCM lege lege, hivyo Magufuli akijenga CCM imara, huu upinzani lege lege uliopo nchini Tanzania hivi sasa, mwisho wake utakuwa ni 2020, Tanzania tunarudi kule kule kwenye nchi ya chama kimoja!. Ndio maana nimesema 2020 hakuna uchaguzi wa rais kutafanyika tuu igizo la uchaguzi!.

  Kwenye uzi wangu huu,
  Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour!, nilimzungumzia JK kuwa sifa kubwa iliyomfanya CCM impitishe ni cheko na bashasha zake!, hivyo JK tumemchekea, tumemdhihaki, tumembeza, tumemkejeli, hadi kumchezea sharubu kama babu na wajukuu zake huku yeye akicheka tuu na kuyaacha yapite. Lakini kwa Magufuli, sijui kama kutakuwepo kuchekacheka au kuchekeana, kubezana na kuchezeana, na kubembelezana, kwa Magufuli ni mambo serious kwa kwenda mbele na hakuna mchezo mchezo, ni kazi tuu!.

  Wajameni japo kwa sasa naongea kama utani au mzaha, lakini hili ni angalizo muhimu sana kwa majaaliwa ya freedom of expression, freedom of speech, na freedom of press ya uhuru huu usio na mipaka tulionao sasa nchini mwetu, tukiwemo sisi humu jf, tulio enjoy wakati wa Kikwete, lakini mbele ya unpredictable dictator kama Magufuli, kiukweli kabisa huko tuendako, kama hatabadilika, then ni mashaka matupu!, salama yetu hata sisi jf pia ni tumjoin him kwa kumsifu kwa nyimbo na mapambio, vinginevyo....

  Thanks God, mimi ni mmoja wa wana jf wachache, waliopata priviledge ya kujua huyu Magufuli aliibukia wapi na ilikuwaje kuwaje hadi akawa ndie akawa mgombea wa CCM na sababu ni zipi zilifanya awe ni yeye. Ukilisoma bandiko hili ukazijua sababu zilizosababisha akawa Magufuli, labda utanielewa nazungumzia nini!.
  Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli!

  Hivyo kwa nature na hulka ya udikiteta wa Magufuli, let's hope, kuwa zile sababu zilizopelekea kuwa mgombea wa urais wa CCM ndizo pekee (the ones and only) zitakazo weza kumcheck and balance him in between being a real dictator and a benevolent dictator vinginevyo hata hao CCM wanaoshangilia ushindi kwa sasa, akitokea kuwa a real one, hata CCM wenyewe nap watakuja kujuta!, therefore, to be on a safe side, it's better if you can't beat them, just join them, to be on a safe side!.

  Wapinzani wote wakiwemo wana Chadema, wana UKAWA, na Watanzania wenzangu kwa ujumla, najua wengi wenu mlimtaka Lowassa, mmemkosa!, na badala yake mkapewa Magufuli, hivyo natoa wito wa "If you can't get what you want, just take what you get!", ukikosa ulichotaka, then pokea ulichopewa!, tumkubali Magufuli kwa moyo mkunjufu, hivyo hivyo alivyo na udikiteta wake, tumpokee na kumpatia kila aina ya ushirikiano wote unaohitajika kumuwezesha kuiongoza vema na sala hii Tanzania yetu. Tanzania sio nchi ya Magufuli wala Tanzania sio mali ya CCM, Tanzania ni ya Watanzania wote, ni nchi yetu sote, hivyo it can be done kama kila mmoja wetu will play his part!.

  Sio tumjoin Magufuli kwa sababu sasa ndio tunampenda hivyo tumemkubali, no way, tumjoin Magufuli kwa kumkubali ndie the only one rais tuliyepatiwa na Mungu, hivyo we have duty and a responsibility to join him kwa lazima, tutake tusitake, tupende tusipende, yeye ndie rais wetu hivyo we have to join him and support him because we have to!.

  Kwa kuweka tuu kumbukumbu sawa, hata mwaka 2010 Chadema waliposhindwa, walisusia matokeo walijidai kunsusa na kujidai hawamtambui JK, lakini hatima yake ilikuja kuwa hivi

  Chadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza!

  Bandiko hili liliwaudhi sana Chadema humu jf, Mwana JF, Regia Mtema (RIP) akanitaka niombe radhi
  Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya ....

  Radhi iliombwa
  Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya ...

  This same, same scenario inataka kujirudia kwa Chadema na Ukawa kujidai kutaka kumsusia Magufuli!. Kuna vitu mtu unaweza kususa na kuna vitu huwezi kususa!,kwa hata 2010 Chadema walisusa lakini tukawashuhudia makamanda wakifakamia chai, juice na vitafunwa vya ikulu, huku meno 32 nje kwa vicheko, hivyo hata awamu hii ya Magufuli, msije kushangaa Mbowe akiwaongoza tena makamanda, akiwemo Lowassa kubisha hodi ikulu na kumpongeza Magufuli.

  Paskali
   
 2. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #121
  Oct 28, 2015
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,211
  Likes Received: 703
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli!@Junior
  Bora kuwa moto au baridi..., full stop!!
   
 3. S

  Serena Senior Member

  #122
  Oct 28, 2015
  Joined: Apr 4, 2014
  Messages: 124
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35

  Mkuu,
  Kama vile ulikuwa kwenye akili yangu. Magufuli atakuwa mtumishi wa JK, na nataka nikuambie tu kwamba kwa Magufuli tutaendelea kuongozwa na Kikwete na Mkapa kwa miaka 5 au 10 ijayo. Hakika ni majuto kwa watanzania.
   
 4. pumzihaiuzwi

  pumzihaiuzwi JF-Expert Member

  #123
  Oct 29, 2015
  Joined: Mar 27, 2015
  Messages: 2,553
  Likes Received: 1,927
  Trophy Points: 280
  tumegoma kuandaliwa ki saikolojia aluta continuaaaa!
   
 5. Masunga Maziku

  Masunga Maziku JF-Expert Member

  #124
  Oct 29, 2015
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 4,026
  Likes Received: 1,983
  Trophy Points: 280
  Pasco hivi wewe huwa uko upande gani.??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #125
  Oct 29, 2015
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,229
  Likes Received: 5,992
  Trophy Points: 280
  Upande wa faida.Kwani nani anataka hasara.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #126
  Oct 29, 2015
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  The problem is that the opposition hasn't given us a worthy replacement and has alienated sane Tanzanians with its sheningan. They joined forces so they have now labeled themselves collectively this Ukawa brand which is non existent and weak. What we need is a separate platform to organize on!
   
 8. leonwillian

  leonwillian Member

  #127
  Oct 29, 2015
  Joined: Jan 7, 2015
  Messages: 17
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 5
  Thing is CCM is trying so hard maintain its ruling party position and is doing whatever it takes even if its faking ballot papers or whatever...
  It also sickens me that people when they get into power there's not too much they do to contribute to development of our economy.. Thats why we just lag behind other african countries..
  I respect all those who voted CCM politicians but i feel sorry for them at the same time.. I mean CCM should trust that they have all of you "CCM" to vote for them With no need to rig the elections..
  :rolleyes:
   
 9. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #128
  Oct 29, 2015
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,229
  Likes Received: 5,992
  Trophy Points: 280
  Aleselema...
   
 10. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #129
  Oct 29, 2015
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,229
  Likes Received: 5,992
  Trophy Points: 280
  Rais:DK Magufuli PM:DK Mwakyembe SPEAKER:SITTA NISHATI&MADINI:pROF MUHONGO(Mengi lazima aharishe mfululizo) .Patachimbika Mazeee...."KAZI TUUU"
   
 11. J

  Jizzy1 JF-Expert Member

  #130
  Oct 29, 2015
  Joined: Sep 29, 2013
  Messages: 464
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watu wenye ufahamu ndio wapotoshaji wakubwa, mmekosa uzalendo badala yake mmetanguliza ubinafsi mbele, ulichokisimamia jana leo hukitaki, unachokisema leo baadae unakikana alimradi maslahi yenu yafanikiwe, aibu sanaaa!
   
 12. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #131
  Nov 7, 2015
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,229
  Likes Received: 5,992
  Trophy Points: 280
  Wanapotosha nini?
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #132
  Nov 23, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Nafanya tuu rejea ni kwa mujibu wa sheia, taratibu na kanuni ipi iliyompa rais wetu mamlaka ya kuamuru matumizi sahihi ya private money za michango?!.

  Jee rais anayo mamlaka ya kuifuta parade ya uhuru?!.

  Pasco
   
 14. t

  tukuzi Member

  #133
  Nov 23, 2015
  Joined: Jul 12, 2015
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anachosikitika lowasa sio kupata uraisi bali kukosa phd ya kupewa@@@@@
   
 15. M

  Mtimbo JF-Expert Member

  #134
  Nov 23, 2015
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 1,316
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Kapitie public holiday Act
   
 16. Manjagata

  Manjagata JF-Expert Member

  #135
  Nov 23, 2015
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 4,249
  Likes Received: 1,789
  Trophy Points: 280
  Mkuu ulishamaliza kila kitu! Nakasirika sana ninapokumbuka wa-TZ tulichofanyiwa na akina Lubuva na wenzake! Huyu hatukumchagua sisi! Kwa wale wanaopiga mbinja sasa hivi nawahurumia sana!! Na wote tuseme "ALANIWE LUBUVA NA WENZAKE"
   
 17. twahil

  twahil JF-Expert Member

  #136
  Nov 23, 2015
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 3,590
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Sisi watanzania tunaangalia maamuzi ambayo yana tija kwetu.....ni kwamba sherehe ya uhuru/parede kwa mwaka huu kufutwa ni jambo jema na litasaidia pesa za kugharamia zoezi zitimike kwenye huduma za kijamii...

  Pasco watanzania tumelialia sana kuwa na dictator na tumempata...hata luwasa alikuwa doctator kwani alikuwa akitutaka wapinzani wake kufunga midomo....

  Magufuli anafaa awe dictator ili kupambana na uvivu wa watanzania...ili wafanye kazi...
   
 18. MGILEADI

  MGILEADI JF-Expert Member

  #137
  Nov 24, 2015
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 1,406
  Likes Received: 1,266
  Trophy Points: 280
  Japo umechanganya lugha niseme tu: Awe dikteta mkaidi ama dikteta muungwana, Rais wa sasa anaunganisha mielekeo miwili ya uongozi; anajali wananchi yaani watu na pia majukumu yake kama kiongozi mkuu wa nchi. Yeye anayatolea maongozi mambo yanayolisibu taifa letu. Huo si udikteta pitilizi bali uongozi unaotafuta uwiiano unaofaa kuliongoza taifa katika njozi zake za kimaendeleo - NJONZI YA KITANZANIA - kumiliki rasilimail zetu kwa manufaa ya watu wote na hivyo kuondosha matabaka ya kijamii-uchumi, umaskini wa kujitakia na utumwa wa kiuchumi nchini mwetu. Mhe. Maghufuli ni nyota ya mapambazuko ya uamsho mpya wa kitaifa wa Tanzania.
   
 19. mganione

  mganione JF-Expert Member

  #138
  Nov 24, 2015
  Joined: Aug 31, 2015
  Messages: 462
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 80
  Who laughs last , laughs best
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #139
  Jun 25, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Nafanya tuu rejea!, "CCM ya Magufuli itakuwa ni CCM sasa kazi tuu, ambayo ni hatari kwa waliozoea CCM lege lege, hivyo akijenga CCM imara sana, huu upinzani mwisho ni 2020!."

  Kwa haya yanatotokea, nawashangaa wanaoshangaa, as if hawakutegemea!.
  Pasco
   
 21. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #140
  Aug 6, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Rejea......

  P.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...