#COVID19 If you cannot question it, it's not science, It's propaganda

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Mimi nimechanjwa chanjo ya P fizer muda mrefu wakati hapa kwetu tukihubiri malimao na matangawizi, Tuliimba pambio wote za ujasiri wakati huo kuwa beberu hafai na chanjo hazifai

Leo bila aibu na Haya wana CCM tumegeuka ghafla na kuanza kudance ngoma ya mwenyekiti wa chama

Nimeandika uzi huu baada ya kuona nchi ya Israel inawapa watu wake kitu kinaitwa Booster baada ya chanjo, Yaani baada ya miezi kadhaa ya watu kuchanja Nchini Israel sasa wanaongezewa nguvu kama gari bovu iitwayo Booster kupambana na corona

Gwajima ana hoja ya msingi, Ajibiwe kwa hoja na Facts

Prof Kabudi alionekana akinywa dawa ya miti shamba ya madagaska mbele ya uma wakati sayansi ikiendelea na tafiti,

Maprofesa wa afya Muhimbili walionekana wakisisitiza ujenzi wa mabanda ya kufukiza nyungu pale Muhimbili

Waziri wa afya Dkt Dorothy Gwajima alionekana akinywa mchanganyiko wa limao, tangawizi na vitunguu

Questions?
Lengo la profesa Kabudi, Waziri wa afya Doroth Gwajima, na Maprofesa wa afya Muhimbili ilikuwa ina lengo gani kuhimiza mambo ya miti shamba badala ya Science?

Lengo Lao la sasa kwenye chanjo ni kitu gani?

Je? Wana uhakika ndimu na malimao jumlisha miti shamba haitibu tena Corona?

Je? Chanjo wanazosifia sasa hasa Waziri wa afya ana uhakika hazina madhara ya muda mrefu au mfupi

Je, hii booster mpya ambayo watu wanaongezewa baada ya kuchanja wataalamu wetu wanafahamu na wamewaambia Raia wanaowachanja

Je, ni Propaganda za kisiasa wanazifanya kwa kuangalia uelekeo wa anayeongoza?

Hoja za kisayansi zijibiwe kisayansi na si kuzijibu kwa propaganda
 
Et mambo ya miti shamba badala ya science, mitishamba sio kinyume cha sayansi ndio maana hata hizo dawa za kutengenezwa maabara hutumia pia hiyo mitishamba.

Cha msingi ni utafiti na ushahidi wa kisayansi ndio maana hiyo mitishamba ipo ambayo imefanyiwa tafiti za kisayansi na ikajulikana hiyo mitishamba inatibu aina gani za magonjwa na ina faida gani mwilini lakikini pia ipo mitishamba ambayo haijafanyiwa tafiti za kisayansi hivyo tatizo sio kuwa mitishamba tu.
 
tuulizeni sisi tuliopo huku vjjn,yaani watu hawana mpango wa hizo chanjo,juz nimepita haashauri fulani nimekuta wanatoa elimu juu ya chanjo.huku vjjn watu wako biz na maisha ya kutafuta mkate wa siku.kuna shule ya msingi moja wakawq wanatoa chanjo ,wanafunzi wakatoroka wote,waliobaki wazazi wakawafuata watoto wao
 
Mkuu, kwanza hongera sana kwa kua mmoja kati ya watu waliopata chanjo, hongera sana.

Pili, nilitaka kujibu kidogo kuhusu booster wanazopewa huko israel. Kitu muhimu cha kufahamu ni kwamba chanjo zote hizi zitolewazo kwa sasa zilitengenezwa kwa ajili ya kuzuia kirusi cha wimbi la kwanza. Kwa tafiti zilizopo ni kwamba mtu aliechomwa chanjo hawezi pata kirusi kilichosambaa phase 1.

Jambo jingine, la muhimu ni kwamba side effects zipo, ila kwa sasa zionekanazo nyingi ni za muda mfupi.

Kwa kumalizia tu, napenda kusema covid-19, imetuonyesha ni jinsi gani wataalamu wetu wa afya ambavyo hawana weledi na ni wavivu wa kufanya tafiti, pia viongozi wetu wengi ni watu wenye tamaa ya madaraka na wasiojali wananchi wao na wengi wao ni wanafiki.

Respect......
 
Binafsi nimejitoa sadaka, sitachanja ila nazingatia mtizi, menyu na usafi (mfano kunawa na maji tiririka)

Acha nikae zangu bush napiga zangu jembe.

Nimekwisha watonya watu wangu wa karibu.
 
Lengo la profesa Kabudi, Waziri wa afya Doroth Gwajima, na Maprofesa wa afya Muhimbili ilikuwa ina lengo gani kuhimiza mambo ya miti shamba badala ya Science?
Prof Kabudi kwa sasa, mtoe kwenye kuwajibika kujibu swali hili tafadhali. Vinginevyo useme una hila juu yake.
 
Back
Top Bottom