If there is no foul play, then please release that report asap

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,832
287,782
Posted Date:: 24.12.2007 @03:18 EAT

No foul play on BoT-Epa report
By Bernard James
THE CITIZEN

Controller and Auditor General Ludovic Utouh denied yesterday that the Government was masterminding a plot to�doctor� the much awaited probe report on the Banl of Tanzania�s External Payments Arrears.

Mr Utouh said in a two-page statement that his office was acting independently, adding that there would be no alteration of the contents of the EPA reports.

�I have received this report today. I will go through the report before forwarding it the President in the first week of January next year,� he said.

Mr Utouh�s statement comes in the wake of pressure from the Opposition, which has demanded that the findings be published immediately, saying delayed release of the report suggested that there was a plot to�doctor� its contents.

The CAG said the delay had nothing to do with any such moves to hide the truth on the EPA investigation.�The report has not been deliberately sat upon as is believed.

This is a crucial document which must be carefully studied to make sure that all recommendations it contains are appropriate,� Mr Utouh said.

He also defended the international auditing firm Ernst &Young which carried out the investigation, saying it had used well trained experts from Japan, Britain, South Africa, Kenya and Tanzania.

But while the CAG states that the report will be handed over to the President next week, Finance minister Zakia Meghji said on Friday that the findings would be released early this week.

According to the Terms of Reference, Ernst & Young was also tasked to review the BoT audit report for the financial year 2005/6.

The firm was thus required to submit two reports � one on EPA accounts and the other on BoT�s accounts for 2005/6.

The EPA issue has rocked BoT in recent years with the Opposition claiming that $800 million (Sh960 billion at current exchange rates) was stashed away through shady transactions.

It is alleged that a phantom company, Kagoda Investments Co, was paid $30 million (Sh36 billion) in September 2005 in one of the dubious transactions.

Investigations conducted by Deloitte and Touche, which was tasked to audit BoT accounts before their contract was suspended, established that the company presented forged documents to claim EPA money.

The company was formed in September 2005 and existed for just three months before its registration documents vanished from the Business Registration and Licensing Authority offices.
 
CAG ajitetea

na Tamali Vullu
Tanzania Daima

SIKU kadhaa baada ya baadhi ya wanasiasa kuonyesha wasiwasi juu ya uwezekano wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuishughulikia ripoti ya ukaguzi wa Benki Kuu, CAG amejitetea kuwa ofisi yake inamudu kazi hiyo.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, alisema katika taarifa aliyoisambaza jana kuwa ripoti hiyo, ambayo iliwasilishwa ofisini kwake Novemba, haijakaliwa makusudi.

"Ripoti hii ni muhimu sana kwa taifa, hivyo ni lazima ifanyiwe kazi kwa umakini mkubwa na kuhakikisha mapendekezo yatolewayo ni sahihi," anasema Utouh katika taarifa yake ya kurasa mbili.

Aidha, aliwahakikishia Watanzania kuwa ofisi yake haiwezi kuivuruga taarifa ya ripoti hiyo kama ambavyo baadhi ya wanasiasa walionyesha wasiwasi huo.

"Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ni ofisi iliyo na uhuru kamili wa kufanya kazi zake kwa kufuata sheria, kanuni na viwango vya taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu vya kimataifa.

"Vile vile ikumbukwe kuwa uchunguzi huu umefanywa na kampuni ya ukaguzi ya kimataifa, Ernst & Young ambayo ilitumia wataalam kutoka sehemu mbalimbali dunaini, zikiwemo Uingereza, Afrika Kusini, Japan, Kenya na Tanzania. Uchunguzi huu umefanyika kitaalam kwa kuzingatia taratibu na viwango vya ukaguzi wa hesabu vya kimataifa," alisema Utouh.

Utetezi huo wa Utouh, kwa kiasi kikubwa, umechochewa na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kikionyesha wasiwasi wake kuhusu jinsi ripoti kuhusu uchunguzi uliofanywa BoT inavyoshughulikiwa.

Katika tamko la chama hicho lililotolewa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, kiliitaka serikali kuiweka hadharani ripoti ya ukaguzi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT, ambayo tayari mkaguzi ameiwasilisha kwa CAG.

Mbowe alisema inashangaza kuona kuwa muda uliotolewa kwa Kampuni ya Ernest and Young kuchunguza tuhuma hizo ulishamalizika, huku ripoti ya uchunguzi huo ikiwa imekumbatiwa serikalini.

"Hivyo, tunamtaka Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji watupe ripoti hiyo," alisema Mbowe.

Alisema ameshangazwa kusikia ripoti hiyo kwamba imepelekwa kwa CAG kwa ajili ya kupitiwa, kitendo alichodai kuwa, kinatia shaka huenda kuna njama za makusudi zinazofanywa na serikali ili kutaka kuificha.

"CAG anaipitia nini? Au wanataka kuificha? Fedha zetu tumeibiwa, tumewatangazia, sasa tunataka ripoti iwekwe hadharani," alisema Mbowe.

Hata hivyo, Utouh alisema jana kuwa Novemba mwaka huu alipokea rasimu ya awali ya ripoti ya uchunguzi huo kutoka Kampuni ya Ernst & Young.

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alieleza kuwa baada ya kupokea ripoti hiyo, ilifanyiwa kazi na ofisi yake na kisha kurudishwa kwa wataalamu walioifanyia kazi, ili kukamilisha ripoti hiyo.

"Huu ni utaratibu wa kawaida wa kufanya kazi za ukaguzi hasa ikichukuliwa maanani kuwa Kampuni ya Ernest & Young imefanya kazi hii kwa niaba yangu.

"Mbali na kuchunguza EPA Account ya Benki ya Tanzaia, hadidu za rejea za kazi hii ziliwataka wachunguzi kurejea ukaguzi wa hesabu za Benki Kuu za mwaka 2005/2006 kazi iliyofanywa na kampuni ya hesabu ya TAC Associates ikishirikiana na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi," alisema Utouh.

Alisema wachuguzi hao wametakiwa kutoa ripoti mbili tofauti, moja ikiwa ni ya EPA Account na nyingine ikihusu rejea ya ukaguzi wa hesabu za Benki Kuu kwa hesabu za mwaka 2005/2006.

Kutokana na hali hiyo, Utouh alisema kuwa juzi alipokea taarifa za mwisho za ukaguzi huo na kwamba sasa atazipitia, ili kujihakikishia usahihi wa yaliyomo kabla ya ripoti hizo kuwasilishwa kwa Rais Jakaya Kiwete katika wiki ya kwanza ya Januari mwakani, baada ya kumaliza likizo yake.
 
Jamaa wameshikwa pabaya, hii report ingelikuwa na mema kwa CCM na serikali yake, wangeitoa haraka haraka kama ile report ya polisi kuua raia wema.

Hii chelewa chelew yote ni kujaribu kutafuta njia ya kupunguza makali ya hiyo report. Nyie mnaamini kweli JK hajaiona hiyo report mpaka sasa?

Dr. Slaa ni dume na kwa kweli amewakamata CCM pabaya. Wengine tunaombea aendelee kuwaminya vizuri ili siri zote zitoke.

Kibaya tu ni kwamba wakati Watanzania labda laki tano tunajua kuna report inakuja na tunaisubiri kwa hamu, mamilioni ya Watanzania wenzetu hawana habari hata kwamba kuna wajanja wametuibia.
 
Ni wajibu wa hao laki tano kulinda maslahi ya milioni 35 waliobaki. Elimu waliyopewa hao laki tano ni kwa faida ya wote. Wenye elimu wana wajibu wa kupinga uporaji unaoendeshwa na wezi wa ndani na nje ya nchi, hata kama wizi huo unasimamiwa na chama tawala.

Tukumbuke vile vile kwamba ripoti ingeweza kutolewa bila serikali kuikubali. Ni ulaghai kuchelewesha hiyo ripoti kwa madai ya kuipitia. Kwani wakiitoa watanyimwa kuendelea kuipitia? Na "kuipitia" maana yake nini hasa? Ni kuisahihisha au kuirekebisha?

Kama serikali haina cha kuficha, basi iitoe hiyo ripoti kama ilivyo, na itoe tamko kwamba bado haijaikubali.
 
tatizo la watanzania ni kuwa tumekosa solution ya matatizo yetu,hivyo serikali kwa maana ya vigogo wanafanya kila wanalotaka bila usumbufu wala mikwaruzo.hata wakitoa leo ripoti hakuna mabadiliko yatakayofanyika ikizingatiwa wahusika wakuu ndio wao wenyewe.
tutafute solution ya matatizo yanayotukabili ktk kuwashughulikia wale wote wanaoliujumu taifa letu.
tukiamua kuandamana kwenda majumbani mwao na kuwapigia kelele watueleze kwa nini wametuibia na sio kuandamana kwenda jangwani na kupiga kelele kisha kila mmoja anarudi nyumbani kulala na ndio imetoka.
TUWAFUATE MAJUMBANI KWAO,SI TUNAWAJUA WOTE.TUANZE MMOJA BAADA YA MWINGINE.
 
Katibu Tarafa umekosea. Hatutaki fujo. Hatutaki kupigana majumbani kwa watu. Tunapenda tuendelee kuwa na amani.

Ikitolewa hiyo ripoti, basi inaweza kutumika kama evidence (sasa, au baadaye). Tuna viongozi shupavu kama Wilbrod Slaa ambao wataweza kuitumia kuwaajibisha wahusika sasa au baadaye. Vile vile, ripoti itasaidia Watanzania kujua ukweli wa yaliyotendeka BoT. Na kwa uelewa kama huo, wataamua wachague watu gani kuwaongoza.
 
Katibu Tarafa umekosea. Hatutaki fujo. Hatutaki kupigana majumbani kwa watu. Tunapenda tuendelee kuwa na amani.

Ikitolewa hiyo ripoti, basi inaweza kutumika kama evidence (sasa, au baadaye). Tuna viongozi shupavu kama Wilbrod Slaa ambao wataweza kuitumia kuwaajibisha wahusika sasa au baadaye. Vile vile, ripoti itasaidia Watanzania kujua ukweli wa yaliyotendeka BoT. Na kwa uelewa kama huo, wataamua wachague watu gani kuwaongoza.
Wakubwa wa anga ni bora mkafanya hima kuiweka hiyo hapa JF airport basi mtaona wanavyokurupuka ,maana watakuwa kama wamepoteza nyoka chumbani.Ila kuchelewa kuianika watazidi kuichomekea mauzauza au mnasubiri watoe ronyo hapa muweke origino.
 
This Heat is on, the government cant avoid this one.

Hii ndio matokeo ya upinzani ulio komaa. Good work opposition especially Dr Slaa you are The Tanzanian Hero for the year 2007. Keep it up Dr Slaa Mungu akubariki kwa mchango wako mzuri.
 
AM,
Ufisadi upo kila mahali na sasa hakuna pa kukanyaga,hiyo ripoti niyao wao wenyewe na si yetu kama mnavyofikiria,na si zungumzii ripoti pekeyake ni ubadhirifu kwa ujumla wao ni kuanzia katibu tarafa hadi ikulu.punda ahendi mpaka kwa mjeledi,dawa ni kuwafuata huko huko majumbani kwao na kuwauliza na watupe majibu ya kina sio ya kina kingunge,kama hawataki tuwachape viboko muda wa kubembelezana umekwisha.
 
Naona kuna ujinga wa hali ya juu na Red tapes nyingi tuu , Ripoti imeandaliwa hiko tayari , waziri anasema inabidi tuiangalie upya kabla atujairelease ...huu ni ujinga wa hali ya juu , sasa logic ilikuwa ya kuunda hiyo tume ilikuwa ni nini ? Tume zipewe nguvu za kurelease findings zao kwa raia directly.
 
Naona kuna ujinga wa hali ya juu na Red tapes nyingi tuu , Ripoti imeandaliwa hiko tayari , waziri anasema inabidi tuiangalie upya kabla atujairelease ...huu ni ujinga wa hali ya juu , sasa logic ilikuwa ya kuunda hiyo tume ilikuwa ni nini ? Tume zipewe nguvu za kurelease findings zao kwa raia directly.
Sijui nani atakuwa wa mwanzo kupata mchapo huu wa kufungia mwaka zimebaki siku tano tu ,naweza kusema ni JF last but not list competishon.Yaani hapa ni uhuru na utulivu.
 
tatizo la watanzania ni kuwa tumekosa solution ya matatizo yetu,hivyo serikali kwa maana ya vigogo wanafanya kila wanalotaka bila usumbufu wala mikwaruzo.hata wakitoa leo ripoti hakuna mabadiliko yatakayofanyika ikizingatiwa wahusika wakuu ndio wao wenyewe.
tutafute solution ya matatizo yanayotukabili ktk kuwashughulikia wale wote wanaoliujumu taifa letu. tukiamua kuandamana kwenda majumbani mwao na kuwapigia kelele watueleze kwa nini wametuibia na sio kuandamana kwenda jangwani na kupiga kelele kisha kila mmoja anarudi nyumbani kulala na ndio imetoka.
TUWAFUATE MAJUMBANI KWAO,SI TUNAWAJUA WOTE.TUANZE MMOJA BAADA YA MWINGINE.


Katibu Tarafa
Tatizo ni kweli kuwa tumekosa solution za matatizo yetu, lakini at least sasa hivi tunaonesha kuwa tunafahamu kuwa tuna matatizo. Kama ilivyokuwa huko nyuma, hii ripoti haitafanya lolote, hakuna aliyehusika atakayeshughulikiwa kama Balali usidani kama atakuja tena Tanzania ni mmarekani huyo aliyetolewa kafara, sana sana mimi naona atakayeshughulikiwa ni Slaa mwenyewe kwa njia konakona.
Watanzania ni wazuri sana unawapiga kofi kulia wanasahau, baada ya muda unawapiga kushoto wanasahau. Hii inaelekea huko huko ripoti wataichuja na kuiacha nyeupe, utasikia watu wanasema imetusaidia tutaitumia kuziba mianya ili matatizo kama haya yasitokee, na watanzania wataambiwa watulie, that will be it. This is Tanzania bwana.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom