Elections 2010 Ieleweke wazi siichukii CCM wala Kikwete, nachukia matendo yao wao nawapenda sana

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
SIICHUKII CCM Ni kweli kuna mengi mazuri yamefanywa na CCM niichukieje?
SIMCHUKII RAIS WETU MPENDWA KIKWETE - Yeye naye ni mtu mzuri tu na amefanya mengi mazuri.
NINAYOYACHUKIA.
1. NINAUCHUKIA UMASKINI HASA WA KUJITAKIA KWA KUWAKUMBATIA MAFISADI
2. NINACHUKIA UJINGA HASA PANAPOKOSEKANA UTASHI WA KUUONDOA KWA KUTOA ELIMU BURE KWA GHARAMA ZINAZOTOKANA NA KUZIBA MIANYA YA RUSHWA NA UFISADI.
3. NINACHUKIA SABABU NYEPESI ZINAZOTOLEWA NA VIONGOZI KUWA TUNAPOUNGA MKONO HOJA ZINAZOONYESHA MABADILIKO BASI NI KWA SABABU YA UDINI AU UKABILA.
4. NACHUKIA HALI YA KUPUUZA WANANCHI WALIOCHUKIA UFISADI KWA KUWATAKASA WENYE KESI ZA UFISADI KUWA WANAFAA.
5. HILO LIKILETA HASIRA IJULIKANE SIO SABABU ZA KIDINI WALA KIKABILA NI SUALA LA WATU KUKATA TAMAA NA KUTAKA MABADILIKO.
6. SIONI MWENYE UFAHAMU WA KAWAIDA ATAUNGAJE MKONO WANAOWAUNGA MKONO WENYE TUHUMA NZITO ZA UFISADI HATA KAMA MAHAKAMA HAIJAWATIA HATIANI.
7. WANANCHI WA KAWAIDA WANAONA MAHAKAMA HAIWEZI TENA KUWATIA HATIANI KWANI ANAYEWATEUA MAJAJI AMESHASEMA WAO NI SAFI NA KATIKA JIMBO ZIMA HANA MFANO BORA KULIKO HAO.
 
Ni vema sababu zinazotolewa za dini, ukabila zikaepukwa na kukimbiwa. Kila dalili inaonekana zikitafutwa sababu za uongo kwa nini ccm iwe na wakati mgumu sasa?
 
Nakubaliana na wewe kuwa sababu zinatengenezwa pale ambapo watu wanakataa makusudi kuukubali na kuukabili ukweli. Kutoa visingizio ni kosa kubwa. Sababu za kutokukubalika kwa ccm ni wao wenyewe na sio kitu kingine.
 
Kwa sababu hizo nawachukia wote na vyote vinavyoshabikia hayo i.e kimantik huo uzuri unapotezwa na lundo la ubaya
 
Nadhani hata neno wapinzani sio neno sahihi kwa kiswahili ni vyema wale wa upande mwingine wakaitwa washindani. Ila ni rahisi kama watu wamejikita katika hayo unayoyachukia wao nafsi zao zikachanganyika humo na hivyo itawawia vigumu kuona tofauti ya kuwachukia wao na kuyachukia matendo yao.
 
WALE WALIOZOEA KUFANYA MAMBO KWA NAMNA ILEILE , WATARAJIE KUPATA MATOKEO YALE YALE WALIYOZOEA KUYAPATA.
HUWEZI KUPATA MATUNDA TOFAUTI KWA KUPANDA MBEGU ZILE ZILE ZILE.

HUWEZI KUFIKA UNAKOTAKA KWA KUBAKIA PALEPALE ULIPO.:A S thumbs_up:
 
SIICHUKII CCM Ni kweli kuna mengi mazuri yamefanywa na CCM niichukieje?
SIMCHUKII RAIS WETU MPENDWA KIKWETE - Yeye naye ni mtu mzuri tu na amefanya mengi mazuri.
NINAYOYACHUKIA.
1. NINAUCHUKIA UMASKINI HASA WA KUJITAKIA KWA KUWAKUMBATIA MAFISADI
2. NINACHUKIA UJINGA HASA PANAPOKOSEKANA UTASHI WA KUUONDOA KWA KUTOA ELIMU BURE KWA GHARAMA ZINAZOTOKANA NA KUZIBA MIANYA YA RUSHWA NA UFISADI.
3. NINACHUKIA SABABU NYEPESI ZINAZOTOLEWA NA VIONGOZI KUWA TUNAPOUNGA MKONO HOJA ZINAZOONYESHA MABADILIKO BASI NI KWA SABABU YA UDINI AU UKABILA.
4. NACHUKIA HALI YA KUPUUZA WANANCHI WALIOCHUKIA UFISADI KWA KUWATAKASA WENYE KESI ZA UFISADI KUWA WANAFAA.
5. HILO LIKILETA HASIRA IJULIKANE SIO SABABU ZA KIDINI WALA KIKABILA NI SUALA LA WATU KUKATA TAMAA NA KUTAKA MABADILIKO.
6. SIONI MWENYE UFAHAMU WA KAWAIDA ATAUNGAJE MKONO WANAOWAUNGA MKONO WENYE TUHUMA NZITO ZA UFISADI HATA KAMA MAHAKAMA HAIJAWATIA HATIANI.
7. WANANCHI WA KAWAIDA WANAONA MAHAKAMA HAIWEZI TENA KUWATIA HATIANI KWANI ANAYEWATEUA MAJAJI AMESHASEMA WAO NI SAFI NA KATIKA JIMBO ZIMA HANA MFANO BORA KULIKO HAO.

NIPO PAMOJA na wewe ila mimi namchukia kwa kukumbatia mafisadi!
 
Back
Top Bottom