Idris Sultani awajia juu wachungaji makanisa ya kiroho

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
Kupitia ukurasa wake wa Tweeter ameandika hivi!!
IMG_20200413_094910.jpeg
IMG_20200413_094935.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imani,hasa za kidini,ni chanzo cha ujinga kwa wanadamu walio wengi.

Dini imegeuka biashara huku imani zikipumbaza watu kiasi cha kushindwa kuona huu usanii.

Ukitaka kumchota akili mnyama, mpe chakula atakuwa rafiki kwako hata kama una nia ya kumdhuru,na ukitaka kumchota akili mwanadamu,mjengee imani unaweza kumchezea kama mdoli.

Wafuasi wa Kibwetere na viongozi wao bado wanaishi na wataendelea kuwepo mpaka mwisho wa hii dunia.
 
4 Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye.

5 Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

6 Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara.

7 Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu.
 
Ila kwa Africa hao wahubiri watenda miujiza ni baraka kwa wanasiasa dhaifu. Unadhani ni kwa nini watu wanajaa kufuata miujiza ya uponyaji ama ya baraka za utajiri kama si kutokana na mifumo ya uendeshaji wa nchi zao kushindwa kuwasaidia?

Kuachiwa kwao kuendelea kunatokana na kuwa wanasiasa hawana majibu kwa matatizo ya watu wanaowaongoza. YESU siyo daktari na muujiza kwa jina lenyewe tu si jambo linalotarajiwa kutokea kila mara, sasa ni kwa nini kila siku mtu awaalike watu kuja kupata miujiza?

Watu wanaambiwa hakuna lisilowezekana kwa YESU lakini YESU mwenyewe aliondoka duniani akiwa ametenda miujiza ambayo haijai hata kwenye kiganja. Sasa huyu mfuasi wake ambaye kila siku anataka kutenda miujiza kama dozi anawezaje?

Afrika mifumo ya Ajira, Afya na mahusiano imeharibiwa kiasi kwamba hao watenda miujiza ndiyo wanakimbiliwa angalau kidogo wawatulize hao waafrika wenzao kisaikolojia kwa mazingaombwe yao.
 
Ile video ya yule mchungaji wa jana ni upuuzi mkubwa,unatoa zaka halafu unapewa chanjo ya corona na maombi juu.

Waumini wengi nao wamekuwa wajinga kweli wanamsikiliza,chanjo ya corona itolewe kanisani?halafu bado wanamsikiliza,hawa wachungaji wanabuni tu mbinu za kupata hela kwa njia za uogo

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Idris amechelewa kujua, na nimkumbushe tu pia kwamba hata huko upande wa pili wapo hawa.

Ni jana tu nilikuwa namsikia Bw aliyejiita "Sheikh" (sina uhakika kama hiki ni cheo maalum au yeyote aweza kujiita) mmoja kupitia moja ya redio ya mkoani akiwatangazia watu kwamba ana mafuta ya ajabu ambayo Mtu akijipaka ataondokana na matatizo yote yanayomkabili.

Ingawa hakuitaja moja kwa moja corona ila ni wale wale tu wanaotumia kivuli cha dini kufanya upuuzi wao....na ili kuboresha chambo chake alikuwa haishi ku refer vifungu vya msaafu.
 
Hahaha toa sadaka usipate korona. Dini imepumbaza waafrika wengi sana hadi huruma, cha kushangaza wenye dini wengi duniani ndiyo masikini, what a waste of 🧠
Sio masikini tu, na ndio wasio na uwezo wa akili ya kutatua matatizo yao na jamii zao.

Watu ni mabingwa wa kusali na kukesha makanisani na kumtaja Mungu kwa kila jambo lakini karibu 95% ya maisha yao wanategemea teknolojia ya Mjapani asiyeamini hata 1% ya hicho wanachoamini wao.
 
1 TIMOTHEO 4
1: Roho anasema wazi wazi kwamba katika siku za mwisho watu wengine wataiacha imani yao na kusikiliza roho za udanganyifu na mafundisho ya mashetani.
2: Mafundisho hayo yanaletwa na wanafiki waongo ambao dhamiri zao zimekufa kama vile zimechomwa kwa chuma cha moto.

Je wewe unafuata imani yako au unamsikiliza fulani anasema nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwa Africa hao wahubiri watenda miujiza ni baraka kwa wanasiasa dhaifu. Unadhani ni kwa nini watu wanajaa kufuata miujiza ya uponyaji ama ya baraka za utajiri kama si kutokana na mifumo ya uendeshaji wa nchi zao kushindwa kuwasaidia?

Kuachiwa kwao kuendelea kunatokana na kuwa wanasiasa hawana majibu kwa matatizo ya watu wanaowaong0za. YESU siyo daktari na muujiza kwa jina lenyewe tu si jambo linalotarajiwa kutokea kila mara, sasa ni kwa nini kila siku mtu awaalike watu kuja kupata miujiza?

Watu wanaambiwa hakuna lisilowezekana kwa YESU lakini YESU mwenyewe aliondoka duniani akiwa ametenda miujiza ambayo haijai hata kwenye kiganja. Sasa huyu mfuasi wake ambaye kila siku anataka kutenda miujiza kama dozi anawezaje?

Afrika mifumo ya Ajira, Afya na mahusiano imeharibiwa kiasi kwamba hao watenda miujiza ndiyo wanakimbiliwa angalau kidogo wawatulize hao waafrika wenzao kisaikolojia kwa mazingaombwe yao.
Hata USA makanisa ya kiroho yanajaa...
 
1 TIMOTHEO 4
1: Roho anasema wazi wazi kwamba katika siku za mwisho watu wengine wataiacha imani yao na kusikiliza roho za udanganyifu na mafundisho ya mashetani.
2: Mafundisho hayo yanaletwa na wanafiki waongo ambao dhamiri zao zimekufa kama vile zimechomwa kwa chuma cha moto.

Je wewe unafuata imani yako au unamsikiliza fulani anasema nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Roho amesema au mwandishi wa hicho kitabu ndio amesema kua roho alisema?
 
Back
Top Bottom