Idris Sultan, wenzake wafutiwa mashtaka na mahakama

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,903
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi na kumwachia huru msanii wa vichekesho, Idris Sultani na wenzake wawili baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) akielezea mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Sultan na wenzake walikuwa wanakabiliwa na shtaka moja la kuchapisha picha mtandaoni bila kuwa na kibali.

Washtakiwa hao wamefutiwa mashtaka chini ya kifungu namba 91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo, umetolewa leo, Jumanne Agosti 17, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga, baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Wakili wa Serikali, Neema Mosha, ameieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imewekwa kwa ajili ya Ushahidi, lakini Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Wakili Mosha, baada ya kueleza hayo, Hakimu Ruboroga, alisema kupitia kifungu hicho, Mahakama imewafutia mashtaka washtakiwa wote na kuwaachia huru

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Daktari Ulimwengu (28) mkazi wa Mbezi Beach na Isihaka Mwinyimvua (22) mwanamke wa Gongolamboto.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 8, 2016 na Machi 13, 2020 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Loko Motion, walichapisha faili katika mtandao huo bila kuwa na kibali kutoka kwa mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA), habari zilizo na sheria.

Mwananchi
 
Inabidi wataalamu wa sheria waje watufafanulie.

Hiki kipengele kinatumika ndivyo sivyo
Kuna aina mbili za Mwendesha Mashtaka kutoendelea na mashtaka.

Aina ya kifungu na. 98(a) cha Sheria ya Uendeshaji wa Mashauri ya Jinai ambayo hufanyika kabla ya mshtakiwa kujitetea mbele ya Mahakama. Ikitumika aina hii maana yake ni kwamba mshtakiwa ataachiwa huru lakini anaweza akashtakiwa tena wakati wowote.

Ukiachiwa kwa aina hii huwezi kushtaki kwamba umeshtakiwa kwa nia ovu.

Aina ya kifungu na. 98(b) cha sheria hiyohiyo hutolewa baada ya mshtakiwa kuwa ameshajitetea mbele ya mahakama. Ikitumika aina hii mshtakiwa anaachiwa huru na hawezi kushtakiwa tena kwa tuhuma zilezile ambazo alishajitetea, na Mwendesha Mashtaka akaomba kutoendelea na mashtaka baada ya kuwa ameshasikiliza utetezi wa mshtakiwa.

Mshtakiwa anayeachiwa kwa kifungu 98(b) anaweza akashtaki na kushinda katika kesi ya madai ya kushtakiwa kwa nia ovu.
 
Back
Top Bottom