Idris Sultan: Watu wametafuna pesa zangu mpaka zimeisha

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Mshindi wa big brother mwaka 2014 idris sultan tetesi zilizozagaa mitandaoni kwamba kuna mtu alimpa pesa zake kwa ajili ya lakini alizitumia kinyume na makubaliano.

1462031883851.jpg


Ikumbukwe mshindi huyo wa Big Brother Africa 2014, alipata zaidi ya milioni 500. Pesa ambayo alidai aliitumia kuwekeza katika biashara mbalimbali, na baadae aliweka wazi kwamba pesa hizo zilishaisha.

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Idris amesema ni kweli kuna mtu alikuwa anafanye naye biashara lakini akamwingiza mkenge. “Kuna watu ambao nimeweza kufanya nao kazi, lakini wakaharibu baadhi ya mambo, nisingependa kuliongelea kwa sababu kuna baadhi ya vitu ambavyo wameviharibu sana, na hawakuweza kuviweka sawa,” alisema Idris.

Aliongeza, “Yaani kama kupunyua, hivi vitu vinatokeaga katika sehemu yoyote, kwenye kampuni, kwenye nini. Kuna watu wanaweza wakafuja mali zako au wakafanya vitu vibaya kinyume na mlivyo kubaliana. Kwa hiyo siyo inshu kubwa sana kwangu, kwa sababu maisha yanaendelea na milango inafunguka,”

Stori ambazo zilikuwa katika mitandao ya kijamii zilikuwa zinadai kuwa meneja wa zamani wa Idris, ndiye ambaye alimwingiza mkenge Idris, kitu ambacho Idris hakupenda kukizungumzia zaidi. Pia Idris amesema kwa sasa amepata menejimenti mpya ambayo itakuwa inamwongoka katika kazi mbalimbali.


Chanzo: Bongo5
 
vijana, hawa wakaombewe wana mapepo. Hivi unaweza ukapata Ml 500 ukaishia kufulia?

Pombe,wanawake na starehe, kujidai wewe ni star ndicho kinacho wagharimu hawa vijana wa bongo movie.

Kalimeni, fungueni mabiashara, wacheni starehe, hiyo pesa ukimpa mtu, mwenye vitu kichwani anakuwa bilionea mkubwa sana.
 
Mburulaz huyo wacha aisome namba *****! alaaah!!! Unadate na wema sepetu unategemea nini? na bado utakuja kusikia ni mpiga debe wa daladala teh teh teheeeeee.......... chezea wadada wa mjini weye utalima lami!
 
Huyo dogo nilishangaa alivyopata million 500 eti akataka kufanya biashara ya T-shirt.. Angerudi Arusha, akachukua ofisi kali na leseni ya kuuza madini akatafuta nyoka akanunua Costa ya kuwapeleka nyoka wake Mererani kutafuta Tanzanite yeye anakuja kununua then anaenda kuuza US na China.. Pia angeweza kununua gold kuanzia kilo na kuendelea then anaenda kuuza huko mbele.. Within a year angekuwa anacheza kwenye billion kadhaa huko
 
Back
Top Bottom