Idris Sultan akamatwa na Polisi, anahojiwa na Kitengo cha Makosa ya Mtandaoni

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
B9AA780C-FBF4-43B6-AC9E-41959AD7258D.png


Mchekeshaji huyo mwenye miaka 27 anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar na anahojiwa katika Kitengo cha Makosa ya Mtandaoni

Anashikiliwa baada ya kuwasili Kituoni hapo kufuatia wito wa Polisi na inadaiwa atahamishiwa Polisi Makao Makuu

Oktoba 2019, alikamatwa kwa kuhariri picha ya Rais Magufuli na alihojiwa kwa saa 5 katika Kituo cha Polisi Central, kisha kuachiwa kwa dhamana

Aidha, Idris aliyewahi kushinda tuzo ya Big Brother Africa mwaka 2014, Machi mwaka huu alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu kwa kuweka maudhui mtandaoni bila leseni
 
Huyu dogo nae anatafuta kiki tu sasa. Unafanyaje kosa lile lile mara 2 hata kama ndani ya nafsi yako unaamini uko sawa.

Baada ya kuachiwa mara ya kwanza kwa kufanya uchekeshaji wa maudhui yale alitakiwa aachane nayo.

Mbona kuna maudhuhi mengi tu ya kuchekesha. Bila kujali kuwa ni sawa au haki au si sawa hatakiwi kulazimisha baadhi ya makosa.

Aache tu kama utawala huu haupendi kuchekeshewa Boss wao awe mpole tu asubiri utawala ujao amcheke huyo Boss.
 
Back
Top Bottom