Idris Sultan afikishwa katika Mahakama ya Kisutu. Ashtakiwa kwa kumiliki laini ya simu isiyo na jina lake. Aachiwa kwa dhamana

Hivi kuicheka picha ya rais ni kitu kimoja na kumcheka rais??
rejea kisa cha Abunuwas na mlio wa punda

SIKU moja abunuwas alipata dinari zake mia. Akaenda sokoni akanunua punda mzuri, akampanda. Akaenda naye mpaka nyumbani kwake. Hata siku moja akaja mtu kuazima punda wake Abunuwas. Abunuwas akanena, Punda hayuko. Mara Yule punda akalia. Yule mtu akanena, punda si huyo analia, na wewe wasema hayuko? Abunuwas akajibu, sasa wewe umekuja kuazima punda ama umekuja kuazima mlio? Kama umekuja kuazima mlio na mimi nitalia. Abunuwas akalia, Ho! Ho! Ho! Akamwambia, haya panda uende zako.
 
nchi (y) africa mtoto chini ya miaka 14 tu alichora picha ya mkuu wao wa nchi ila kisanga walichopata ile familia nahisi hawatokuja kusahau kwenye ulimwengu huu.Simwombei mabaya kijana idd ila nawaza tu alithubutu vp kupost ile video.
 
Mimi sizungumzii kama ana kosa au hana kosa.

Nimesema kuhusu video aliopost idris.

Ilikuwa anacheka na pembeni kuna picha ya raisi.

Mbona mi naona hili la kudhalilisha picha ya mh. Ni jambo lililopo tu akilini kwa watazamaji?

Yaani kucheka imekua ni kosa baada tu ya kuwepo kwa picha ya mhishimiwa!?

Kwani wewe ulijuaje kama alikuwa anaicheka picha!?
Aise inashangaza watu mnavyojitoa ufahamu kutetea ujinga wa huyu dogo, hizi siasa zinatupeleka mahali tunasahau maadili yetu kama watanzania. Watanzania tumelelewa katika maadili ya kuheshimu watu waliotuzidi umri, chukulia mfano angekuwa baba yako mzazi amepostiwa na Idris Kama alivyo fanya we ungejisikiaje kama mtoto. Achilia mbali siasa Raisi JPM ana familia ana watoto, wanajisikiaje wanapoona mzee wao amespostiwa kwa kejeli namna ile. Jpm kiumri ni mzazi kwa Idris kwa hiyo kwa mtu uliyelelewa katika maadili ya Kitanzania na ni mfuasi wa dini muislamu au mkristu huwezi kusapoti ujinga aliofanya Idris.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye picha ya mzazi/wazazi wake tafadhali aiweke hapa alafu tuite comedian waifanyie mambo yao then tuanze kuizodoa, kucheka, kuikejeli nk, ili tupate taswira ya hiki kinnachoendelea.
 
Aise inashangaza watu mnavyojitoa ufahamu kutetea ujinga wa huyu dogo, hizi siasa zinatupeleka mahali tunasahau maadili yetu kama watanzania. Watanzania tumelelewa katika maadili ya kuheshimu watu waliotuzidi umri, chukulia mfano angekuwa baba yako mzazi amepostiwa na Idris Kama alivyo fanya we ungejisikiaje kama mtoto. Achilia mbali siasa Raisi JPM ana familia ana watoto, wanajisikiaje wanapoona mzee wao amespostiwa kwa kejeli namna ile. Jpm kiumri ni mzazi kwa Idris kwa hiyo kwa mtu uliyelelewa katika maadili ya Kitanzania na ni mfuasi wa dini muislamu au mkristu huwezi kusapoti ujinga aliofanya Idris.

Sent using Jamii Forums mobile app
Suti kama ile ningegaragara kabisa hata kama ingekuwa picha ya baba mzazi, na zipo mbona majumbani huwa tunazicheka saanaa, ni comedy tosha

Ila wametusaidia sana kipindi hiki cha Corona there were a lot to distract us from the distress
 
Amekosea saana Idris kwa kumshiaki na kumcheka Rais. Imagine hata watoto wa Rais wanajisikiaje Baba wanahemuheshimu anadhiakiwa hovyo hovyo!
 
Back
Top Bottom