Idris Elba Kuanzisha Studio ya Filamu ya Kimataifa Zanzibar

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
283
619
Serikali ya Zanzibar imetenga ekari 80 za ardhi katika kijiji cha Fumba kwa ajili ya msanii maarufu Idris Elba kuanzisha Studio ya Kimataifa ya Filamu.

Hatua hii inalenga kuimarisha hadhi ya Tanzania kama kitovu kinachochipukia cha uzalishaji wa filamu na kubadilishana tamaduni.

Waziri wa Uwekezaji wa Zanzibar, Shariff Ali Shariff, alitoa tangazo hilo wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar la 27 (ZIFF). Alieleza matumaini yake kuwa studio hiyo mpya itawavutia watengenezaji wa filamu wa kimataifa na kutoa fursa muhimu kwa vipaji vya ndani kujihusisha na tasnia ya filamu ya kimataifa.

Mradi huo ni uwekezaji mkubwa katika sekta ya ubunifu ya Zanzibar, ukiwa na ahadi ya kuleta ajira mpya, mafunzo ya stadi, na kutambuliwa kimataifa. Unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika mazingira ya kijamii na kiuchumi ya Zanzibar, na kuonyesha uwezo wa kisiwa hicho kama eneo la kutengeneza filamu.

======================For English Audience===================
The government of Zanzibar has allocated 80 hectares of land in the village of Fumba for the renowned actor Idris Elba to establish an International Film Studio.

This initiative is set to bolster Tanzania's status as a budding hub for film production and cultural exchange.
Zanzibar's Minister of Investment, Shariff Ali Shariff, made the announcement during the opening ceremony of the 27th Zanzibar International Film Festival (ZIFF).

He expressed optimism that the new studio will attract international filmmakers and provide local talent with valuable opportunities to engage in the global film industry.

The project marks a significant investment in Zanzibar's creative sector, promising to bring new jobs, skills training, and international recognition.

SOURCE: THE CITIZEN
 
Sasa muda wetu sisi upcaming director....
Sio ma director wa miziki...
Naongelea vichwa kama kina Timotheo (Timamu)
Kina Farid Uwezo
 
Ngoja nijiandae nikauze scripts zangu za zanzibar revolution " the 3 hours revolution" maana nilikaa nazo tu kwa miaka 4 sasa ngoja nijaribu bahati yangu..
 
Back
Top Bottom