Idol Gives Back yatumia clip za hospitali ya amana kuelezea Kenya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idol Gives Back yatumia clip za hospitali ya amana kuelezea Kenya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jingoist, Apr 23, 2010.

 1. j

  jingoist Member

  #1
  Apr 23, 2010
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu jana katika kipindi special cha American Pop Idol (BSS ya US) kiitwacho Idol Gives Back niliona kitu sikukielewa. Kipindi hicho ambacho ni mahususi kwa kuchangisha pesa kutoka kwa watazamaji luninga walio majumbani kwa ajili ya kusaidia watoto masikini kinatumia umaarufu wake, wa viongozi na wasanii maarufu duniani. Jana Obama na mkewe walikuwa live kupitia luninga kufungua kipindi hicho. Wengine walioshiriki ni Ban ki Moon, Morgan Freeman and Victoria Bekham. Kwa ujumla kilukuwa na watu wengine wengi maarufu akiwemo queen latifa.

  Ni jambo zuri sana wanalifanya hakuna ubishi katika hilo. Ila mimi nlishangaa waliporusha clip yao moja waliyorekodi inayoonyesha watoto taabani wakiwa wanaugua maleria hospitali. Ilionyesha magari mawili yenye namba za SM na mojawapo ni landcruiser iliyoandikwa ubavuni 'hospitali ya amana manispaa ya Ilala'. Aliyekuwa ananarrate video akadai "our recent visit to Kenya encountered children in a hospital in Kenya...blabla....na ndipo gari hizo zinaonekana zikiingia hospitali ambayo nadhani itakuwa ndo Amana!!

  Je ni makosa ya kiufundi au ni yale yale ya usanii wa wakenya dhidi ya Tanzania. Wanapotumia matukio ya Tanzania kuelezea Kenya kwenye tukio kubwa na maaruku kama hilo wana maana gani. Pesa zinazopatikana na hata mind set na huruma ya hao watoa misaada si itaelekea Kenya japo hali halisi (picha) iliyowatia huruma ni ya Tanzania? Ni yale yale ya Mlima Kilimanjaro kusemwa uko Kenya? Nikichanganya hili na hoja za ushirikiano wa afrika mashariki naungana kabisa na wanaopinga kushirikiana na especially wakenya...nadhani wana ubinafsi na utapeli flani wenye madhara makubwa!!

  Naliacha kwenu kwa kuliwazua na kutoa maoni!!
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Watani wa jadi na njaa zao
   
 3. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Yaani hili liko wazi Mkuu, Tanzania ilikwisha anza kumezwa hata kabla ya mazungumzo ya EAF kuanza. Kwani unadhani kinachowafanya watake hiyo fasttrack nini? Walikwisha onja wakaona tulivyo wajinga, hatujua biashara, wala kuingia makubaliano, tunaweka sahihi makubaliano na mikataba bila hata kuisoma, hatuna viongozi wazalendo kwahiyo wanaharakisha ili nia zao zipate timia wakati huu wa uongozi huu kabla mambo hayajabadilika akaingia mtu anayeipenda nchi ikawa full stop!.
  Ngoja uone ujenzi wa huo uwanja hapo mpakani, Taveta utakapokamilika viwanda vingi vitaanza kujengwa pale vya ku-repackage bidhaa zitokazo Tanzania kuwekwa lable ya Kenya as if produced in Kenya then exported elsewhere, Europe, Asia nk.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wakenya wako tayari hata kuua ili mradi tu wapate pesa
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  lakini tusiwalaum sana jirani ni ujinga wa viongozi wetu. Wakenya wamekuwa ktk upepari kwa miaka mingi na hawana uzalendo kwa hiyo ni jukumu la watanzania kubadilika na kutowalegezea wakenya hasa kwenye ardhi.
   
 6. j

  jingoist Member

  #6
  Apr 23, 2010
  Joined: Mar 24, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuzidi kujitahidi kuwapa viongozi wetu changamoto. Tuwape pressure kwa kadri inavowezekana tukiwa na nia ya wao kutambua kuwa tumeshachoka na inatosha kutuingiza sehemu na katika maisha yasiyofaa. Hizi shule za kata (japo hazina waalimu na vitabu) zitasaidia sana..darasa la saba na ziro ya form 4 nadhani afadhali ile ziro ya form 4..that is what we have and can afford. Watanzania watakaokuwa wamezaliwa kuanzia miaka ya 90 na kuendelea nadhani watakuwa na mtizamo na thubutu ya kupambana na viongozi wabaya na majirani wasanii zaidi...then tunaendelea hivo hivo.

  Hii nchi yetu ina rasilimali na utajiri wa hatari, tunakwama tu kuufaidi. Kuna jamaa juzi alinambia " you people from dar es salaam always keep on trying for years and years but in the end all the money goes to nairobi"! Nilimchekiiiiiii nikauchuna tu maana kuna ukweli ndani yake, na anayesema hivi ni kibabu cha kizungu, nikasema kweli hata watu wa mbali wanajuaga tunavotapatapa na huu umafia!! Tanzania is the richest, (at leats in bioresources I am sure) in Africa except DRC and South Africa! East Africa ndo eneo ambalo linaongoza kwa kuwa na asilimia kubwa ya ardhi ambayo ni jangwa au kavu (drylands), sasa jiulize haya maeneo yako nchi gani!! Drylands za tanzania ni chache. madowezi tu wanatuandama, we need to work this out smartly! Inaumiza sana lakini one day yes wanasema!!
   
Loading...