DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 302
- 274
Wanabodi,
Kabla ya yote, tukubaliane kwamba wana CHADEMA ndio wanaojitoa muwanga katika sakata hili la kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi
Nina amini kwamba kila tatizo lina umuhimu wa kutafutiwa suluhisho. Vile vile katika kukosoa, kuna umuhimu sana wa kuwa na ukosoaji unaojenga na sio ukosoaji unaodhalilisha bila kuleta manufaa yoyote. Ukosoaji huu unahitaji sana kitu kinachoitwa "Open-mindedness" ili kuruhusu majadiliano yenye tija na yenye kuwezesha upatikanaji wa suluhisho mbali mbali. Mengi yanaendelea katika sakata hili la kudai tume huru na katiba mpya lakini swali la kujiuliza ni kama juhudi za wana CHADEMA kufanya mikutano ya hadhara na makongamano yana nguvu za kutosha kuwafikia walengwa. Kitu ninachokiona kwa wana CHADEMA ni kwamba wana amini kabisa kwamba mabadiliko ya katiba na tume ya uchaguzi yanahitaji maamuzi ya mtu mmoja tu iliku idhinisha. Wana kubali kabisa kwamba Rais Samia peke yake, anatosha kubadilisha hali ya siasa nchini kwa kutia saini makubaliano ya kubadilisha katiba na tume ya uchaguzi.
Kama miradi ya kimakakati ya serikali ilivyo, lazima kuwe na sababu iliyofanyiwa tafiti kwa muda mrefu mpaka kufikia hatua ya kuwa na uhakika na kutekeleza miradi hiyo. Wana CHADEMA wanaweza wakawa wana fahamu hilo lakini wana amini kabisa kwamba hawawezi kupata madai yao kwa amani na kwasababu hiyo kutafuta haki barabarani. Sio sahihi kumlaumu Rais kwa kila kitu kisichokuwa sawa kwenye siasa zetu vile vile ni vyema kwa wana CHADEMA kupeleka mfano wa katiba wanayo pendekeza pamoja na mapendekezo yao ya tume huru kwa wahusika kwanza. Ni muhimu kuwa na viongozi ambao wako tayari kusikiliza maoni ya wengine kuhusu kitu chochote hata kama hawakubaliani nao...
Mungu ni mwema, wakati wote