Idea ya kuanzisha TIB (Tanzania Investment Bank) ilikuwa ni nzuri sana

CHASHA FARMING

Verified Member
Jun 4, 2011
7,037
2,000
Nimeshangaa sana kusikia benki ya TIB imeunganishwa na Benki ya Posta ambayo nayo isha unganishwa na benki kibao hapo nyuma.

TIB nazani ilikuwa benki ya Mitaji kama zilivyo kwenye nchi zingine Duniani, Sasa nashangaa kusikia inatakiwa ianze kushindana na wakina CRDB

Idea ya TIB na Idea ya Tanzania Agriculture Bank zinafanana sana sema moja ni kilimo na nyingine ilikuwa ina cover kila kitu

Wazo lake la awali lilikuwa bora shida nazani imekosa mtaji na na kwa speede ya kununua ndege nazani pia hii bank ingepata mtaji wa kutosha ingefanya mambo

Sitashangaa mwakani kusikia imeinganishwa tena na Banki ya Kilimo
images%20-%202020-06-01T183708.962.jpeg
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
6,613
2,000
Tatizo la TIB sio mtaji, bali mikopo mibovu isiyolipika, benki imetoa mikopo hovyo hovyo hailipiki.

Na hiyo mikopo mibovu isiyolipika, usikute wamekopeshana wenyewe kwa wenyewe (Wanasiasa) na hivyo mwisho wa siku wanaoneana aibu kudaiana kama ilivyotokea kwenye ile benki nyingine ya Twiga!
 

aloycious

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
5,954
2,000
lakini mabenki mengine yanatengeneza faida, kwa nini wao watengeneze hasara?
Since 2015 mabenki yanapata faida kwa amana na si kwa loan facility. Sekta ya mikopo imesinyaa "shrinking" toka 2016.

Benki nyingi sasa wanaelekeza nguvu katika mikopo kwa wafanyakazi na sio SME's mzee. Mikopo mingi hailipiki SME's nyingi ever since 2016.

Pia ujue mikopo ni kitengo tuu katika benki. Benki wana vyanzo vingi vya kukua kimtaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom