Elections 2010 Idea: Siku ya uchaguzi na matokeo ya uchaguzi

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Imekuwa ni kawaida kabisa kwa thread kugongana na hivyo MODs kuunganisha thread hizo.
Siku ya Uchaguzi, huenda zikagongana nyingi zaidi na hivyo nyingine zikakoswa kusomwa. Ni kipindi hicho huenda users wa JF wakawa wengi zaidi.
Nilikuwa nina pendekezo moja; Kila Mkoa uandalie thread yake na matokeo ya Kila Mkoa yawe yanaripotiwa hapo kabla ya kuunganishwa na kufanya thread ya nchi nzima. Kwa matukio ya siku ya uchaguzi juu ya mwenendo mzima nadhani moja inatosha.
 
Nadhani hiyo imekaa poa sana, na katika kila mkoa inabidi tuweke kila jimbo kama itawezekana.
 
hakutakuwa na uchakachuaji? utazuiaje member wa dsm asiripoti za idodomia au arusha?
 
Matokeo ya nini tena wakati mnajua Slaa na Chadema wanaingia Ikulu? Teh teh teh!
 
hakutakuwa na uchakachuaji? utazuiaje member wa dsm asiripoti za idodomia au arusha?
Mwenendo wa Uchaguzi wa DAR utaripotiwa kwenye thread ya DAR na ule wa DODOMA kwenye thread ya Dodoma. Otherwise itakuwa kazi siku hiyo kujua nini kinachoendelea. Nadhani mchakato wa kura za maoni ulisababisha mkanganyiko wa kutosha, watu wanarudia maswali ambayo yameshajadiliwa. Sasa kwenye uchaguzi itahusu vyama vingi kwahiyo mkanganyiko huenda ukawa mkubwa zaidi. Si hivyo tu na pia baadhi ya watu wanainterest na majimbo fulani tu huenda hata matokeo ya kila kata yakawa yanaripotiwa km ilivyokuwa Busanda.
 
Back
Top Bottom