Utakuwa huwatendei haki wananchi wa jimbo la Kinondoni kutokana na uamuzi wako wa kutogombea tena ubunge jimbo la Kinondoni. Hao akina Tarimba, Madabida wanaoliwania jimbo la Kinondoni wasikunyime raha. Kuna msemo unasema ukisusa sisi twala.
Una kila sababu ya kugombea tena ubunge wa jimbo la Kinondoni katika uchaguzi mkuu wa 2015. Unatarajiwa kuwepo katika baraza la mawaziri la serikali itakayoundwa. Usiwe na jazba, umefanya maendeleo makubwa katika jimbo la Kinondoni.
Nimesikitika kusikia kwamba wana CCM hawa wenzako wakishirikiana na kijana wa usalama wa Taifa wakitumia vyombo vya habari kukuchafua ati unafanya biashara ya madawa ya kulevya. Walidiriki hata kutaka kukubambikia madawa nyumbani kwako, hii yote ni harakati za kukumaliza kisiasa. Lakini pamoja na hayo unatakiwa ujikaze kiume, usiyumbe.
Wanakuchafua ati pesa zako zinatokana na madawa ya kulevya. Sisi tuliokaribu na wewe tunajua jinsi ulivyohangaika kutafuta pesa kihalali kuanzia udereva wa taxi, mkopo wa kigari cha mizigo mpaka sasa unamiliki kampuni kubwa ya malori. Tunajua jinsi unavyofanya biashara ya kupeleka simenti Congo, Rwanda, Burundi, Uganda na nchi nyingine za Afrika. Hii hoja ya wewe kujihusisha na madawa inatokea wapi ?
Mchango wako kwa ajili ya maendeleo ya wana Kinondoni unahitajika. USIWATELEKEZE WANANCHI WA JIMBO LAKO KWA KUTOGOMBEA TENA UBUNGE. BADILI MSIMAMO WAKO.