Idd Amin: Kituko cha kusisimua alichomfanyia Arube.

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,720
amin_13.jpg

Mr. Amin is carried by four British businessmen during a party for diplomats in 1975. A Swedish businessman holds an umbrella in the manner of servants who once shielded tribal rulers from the sun.

Charles Arube:

Huyu alikuwa mmoja kati ya Makamanda wa ngazi za juu kabisa wa jeshi la Idd Amin Dadda, mtu wa kabila lake Amin liitwalo Kakwa, akitumikia nafasi ya Mkuu wa Majeshi, huku akiwa na cheo cha Ubrigadia Jenerali.

Arube,akiwa mkristo, alichukizwa sana na kasi ya uondolewaji wa wanajeshi wa jamii na kabila za Waacholi, Langi na wengineo wa dini ya Kikiristo jeshini, na nafasi zao kuchukuliwa na watu wa makabila mengine, mpango ambao ulikuwa ukibuniwa na mtukufu rais, Amin, aliyejiita Big Daddy.

Inasemekana huyu jamaa kwa kutumia nafasi yake hiyo alipanga mapinduzi kumng'oa Amin, lakini baada ya intelijenisia ya Amin kuhisi jambo hilo, huyu jamaa alipelekwa kwenye mafunzo huko Jamhuri ya Soviet,na aliporudi alikuta Askari wa kukodiwa(mercenary) wa Kisudani aliyekuwa rafiki yake Amin ameshapewa nafasi yake ya Ukuu wa Majeshi, jambo ambalo lilimzidishia hasira.

Arube aliunda kwa siri kikosi cha mauajia ambacho kilikuwa kimvamie Amin nyumbani kwake, Kokolo Hill huko Kampala.

Usiku wa manane, kikosi hiki kiliwasili nyumbani kwa Amin na kwa mshangao walimkosa, hakuwepo!

Matokeo yake, Arube alizingirwa na askari wa Amin na kupigwa risasi, akafa.

Amin alipoambiwa jambo hilo alienda moja kwa moja mochwari kutazama na kuhakikisha kama kweli huyu mtu alikuwa maiti, na alipofika kwenye chumba hicho aliwafukuza nje waganga wote na wahudumu wa mochwari, akabaki na maiti hiyo peke yake kwa zaidi ya dakika ishirini, akiwa amejifungia makomeo, na hadi leo haijajulikana alikuwa anafanya nini huko chumbani na maiti ile!..Alipotoka aliingia kwenye gari na kuondoka!
 
Mimi mpaka leo naamini idd amin alistahili kifo cha mateso kuliko alichokufa
 
au ndo huyu niliona kwenye muvi akikata nyama ya sehem na kula?
 
its one of the exagerated myths!:( about the man; Amin! But kwa upande mwingine alikuwa mzalendo wa kweli!

Kuna nyingine wakati ule tuliambiwa kuwa alikuwa anaweza kujigeuza joka kubwa!
 
amin_13.jpg

Mr. Amin is carried by four British businessmen during a party for diplomats in 1975. A Swedish businessman holds an umbrella in the manner of servants who once shielded tribal rulers from the sun.

Charles Arube:

Huyu alikuwa mmoja kati ya Makamanda wa ngazi za juu kabisa wa jeshi la Idd Amin Dadda, mtu wa kabila lake Amin liitwalo Kakwa, akitumikia nafasi ya Mkuu wa Majeshi, huku akiwa na cheo cha Ubrigadia Jenerali.

Arube,akiwa mkristo, alichukizwa sana na kasi ya uondolewaji wa wanajeshi wa jamii na kabila za Waacholi, Langi na wengineo wa dini ya Kikiristo jeshini, na nafasi zao kuchukuliwa na watu wa makabila mengine, mpango ambao ulikuwa ukibuniwa na mtukufu rais, Amin, aliyejiita Big Daddy.

Inasemekana huyu jamaa kwa kutumia nafasi yake hiyo alipanga mapinduzi kumng'oa Amin, lakini baada ya intelijenisia ya Amin kuhisi jambo hilo, huyu jamaa alipelekwa kwenye mafunzo huko Jamhuri ya Soviet,na aliporudi alikuta Askari wa kukodiwa(mercenary) wa Kisudani aliyekuwa rafiki yake Amin ameshapewa nafasi yake ya Ukuu wa Majeshi, jambo ambalo lilimzidishia hasira.

Arube aliunda kwa siri kikosi cha mauajia ambacho kilikuwa kimvamie Amin nyumbani kwake, Kokolo Hill huko Kampala.

Usiku wa manane, kikosi hiki kiliwasili nyumbani kwa Amin na kwa mshangao walimkosa, hakuwepo!

Matokeo yake, Arube alizingirwa na askari wa Amin na kupigwa risasi, akafa.

Amin alipoambiwa jambo hilo alienda moja kwa moja mochwari kutazama na kuhakikisha kama kweli huyu mtu alikuwa maiti, na alipofika kwenye chumba hicho aliwafukuza nje waganga wote na wahudumu wa mochwari, akabaki na maiti hiyo peke yake kwa zaidi ya dakika ishirini, akiwa amejifungia makomeo, na hadi leo haijajulikana alikuwa anafanya nini huko chumbani na maiti ile!..Alipotoka aliingia kwenye gari na kuondoka!

Heshima kwako PakaJimmy,

Huyu jamaa kweli alikuwa mkatili sana tena sana lakini kuna baadhi ya mambo alikuwa yuko sahihi kabisa.

[1] Wazungu kumbeba lilikuwa jambo zuri sana kuwahi kufanywa na mwafrika.Naona fahari kubwa mbele ya wazungu kila nitazamapo hii picha.Viongozi wengi wa kiafrika wamekubali kuwa mateka wa wazungu kwa kuwaachia watawale rasilimali zetu kama migodi ya dhahabu kwa hakika Amin pamaoja na madhaifu yake mengi asingekubali mambo ya Geita,bulyankulu na nk.

[2] Alikuwa sahihi kuwatimua wahindi ambao mpaka leo kila wanachochuma kwenye nchi nyingi za kiafrika wanakimbizia UK or Canada.
 
Kuna movie yake moja niliwahi kuingalia inaitwa The Last King of Scotland inafurahisha na kuchekesha pia.
 
Huytu jamaa ndio alikuwa mkatili lakini ukatili wake sidhani kama unazidi huu tunaofanyiwa na watawala wetu, Wanaokufa mhimbili na sehemu nyingine kweli walikuwa wastahili kufa? Nirahisi kulaumu lakini ukijaribu kufikiria saana utagundua yanayotendwa na wanasiasa wetu ni zaidi ya unyama anaohukumiwa nao Dr, Al Haj, Field Marshal, Life President of Uganda IDD AMIN, waganda wengi wanamwona kama shujaa, aliweza kumilikisha uchumi wa Uganda kwa wanganda wenyewe, na naamini asilimia karibia 90 ya uchumi uko mikononi mwa wauganda.
 
Huyu Jamaa pamoja na propaganda zote zilizozungumziwa juu yake alikuwa kwenye kundi moja na viongozi wengi wa Africa katika kuonea wananchi lakini yeye zaidi ya hilo alikuwa mzalendo wa kweli kabisa

[ame]http://video.google.co.uk/videoplay?docid=4169600956573058582&hl=en[/ame]
[ame]http://video.google.co.uk/videoplay?docid=6806802914235278576&hl=en[/ame][ame="http://video.google.co.uk/videoplay?docid=6806802914235278576&hl=en"][/ame]
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom