Idara yatumia milioni 350 kukarimu wageni - Nishati na Madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idara yatumia milioni 350 kukarimu wageni - Nishati na Madini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 1, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja
  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imeshtushwa na matumizi makubwa ya Sh. milioni 350 ambazo zimetumiwa na idara moja kati ya saba kununua karanga, maji, soda na vitu vidogo vidogo kwa ajili ya kukarimu wageni ndani ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2010/2011.

  Kadhalika, kamati hiyo imeshtushwa na idara moja kulipa wafanyakazi wake Sh. milioni 160 kwa mwezi kwa ajili muda wa ziada wa kazi (Overtime) wakati mishahara yao ni Sh. milioni 177 kwa mwezi. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Januari Makamba alisema, kamati yake ilibaini matumizi hayo ya fedha ilipokuwa ikipitia taarifa ya fedha ya wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa kwao.

  Alisema fedha kwa ajili ya kukarimu wageni ambazo zimetumiwa na idara moja ni nyingi ikilinganishwa na hali halisi ya uchumi wa nchi na mahitaji ya Watanzania. Kamati hiyo jana ilimhoji Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na watalaam wake ili kuangalia kama fedha walizotengewa na Bunge zimetumika kama ilivyokusudiwa.

  Kuhusu ulipaji wa posho kuwa mkubwa, Makamba alisema kamati yake imeshikwa na mshangao kuona fedha hizo zinakaribiana na mshahara kamili. Aliongeza kuwa kamati imebaini kuwa wafanyakazi wanalipana "overtime" nyingi inayokaribiana na mshahara hatua ambayo wajumbe waliitilia shaka kama matumizi hayo ni halali. Hata hivyo, Makamba hakufafanua hatua ambazo kamati yake itachukua kuhusu matumizi hayo kwa kuwa wajumbe wake jana walikuwa bado wanapitia taarifa ya fedha ndani ya wizara hiyo.

  IPPMedia
   
 2. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu Makamba ibn Magamba anaitaka hii Wizara kwa nguvu zote!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Uozo huo unafumuka wakati CCM yenyewe ndio imeshika dola, sasa chama kingine kitakaposhika hatamu tutaduwaa kuona hata yake ya kule kusingiingilika kirahisi magogoni.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Ndivyo alivyoelekezwa na mzee wake, mzee wa kaya, aka Yusuf Makamba, ili aukwae uwaziri, vinginevyo kazi nzito kwani watu wanapigana vikumbo kuingia huko kupata mlo uso na jasho.
   
 5. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana Mh.Makamba karanga na sod milioni 350, wakati watu vijijini hawana huduma bora za afya,maji na elimu,inasikitisha sana
   
 6. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  aiseee?!!
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kibaya ni kwamba hata yeye kala hizo karanga!!
   
 8. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu geleja lazima awe waziri? Mbona nachanganyikiwa nikisoma hii habari? Makamba kaza buti kuendelea kuonesha uozo wa hawa watu. Mimi wamenichosha kweli. Thanks Makamba na wenzako kwa hili.
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Du!..vitafunwa tu jamani hela yote hiyo!!..

  This is very serious..OT should be discouraged kwa mtindo huu!!..
   
 10. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo angechekacheka tu ili kuonesha haitaki. *****.
   
 11. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  350 + 160 Just for leisure. This is exactly how the money of tax payers is spent in Tz. No ONE is there to address big issues that are hurting Tz economy. Imagine a single section spending such an amount to buy Karangas! More surprisingly is that, the President is well informed about this uozos and it has been happening for yrs.
  and what makes me even more frustrated is this last para here;

  "Hata hivyo, Makamba hakufafanua hatua ambazo kamati yake itachukua kuhusu matumizi hayo kwa kuwa wajumbe wake jana walikuwa bado wanapitia taarifa ya fedha ndani ya wizara hiyo'"

  Kama sio cheap politics ni nini? Maana haya ya pesa kuibiwa ni kila halmashauri ni kila taasisi! Wanafanywa nini! Absolutely nothing! Nani alikuambia mwizi wa mali ya umma huwa anasamehewa?
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  CCM badala ya kushughulikia hayo wapo mikoani kuhangaikia kuchafua jina la Slaa, watakaporudi nyuma mambo yamebomoka zaidi. Kwa upande fulani huyu Januari Makamba anaonekana kama msaliti kwa CCM, sijali itikadi zake, ila kwa hili nakubaliana naye.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Matumizi hayo ni Idara moja tu ndani ya wizara, je idara za wizara yote? Na mambo kama hayo yapo karibu kila wizara. Tukigeukia na kule magogoni ambako katiba inawalinda kisheria mambo mabaya zaidi yanaweza kuibuliwa baadaye. Magogoni Mkuu wa Idara ya habari alijikinga kifua kwamba hawataki mambo ya uzabizabina. Wanataka wachume watakavyo bila bughudha.
   
 14. m

  mariabeno Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mgosi na kamati yako ninawafagilia na kuwakubali angalau kwa hili. Hili ni moja na dogo sana lakini kubwa ni pale serekali inapokuwa na kigugumizi kuwashughulikia wahusika. Inauma na inakera sana kuona kazi nzuri kama hiyo ya kufichuwa madudu inaishia kwenye makaratasi ambayo baada ya muda yanachomwa moto na habari kushnei. Hili ndio linalowaudhi na kuwakerehesha wa Tz. Ni bora hizo habari zisisemwe kabisa na badala yake tusikie tu kuwa jamaa wahusika na ubadhirifu (baada ya kamati ya Mgosi kupita) wamehukumiwa kunyongwa au hata kufilisiwa pamoja na kufukuzwa kazi. Pamoja na yote tumeona justification ya posho mliyovuta.
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  January Makamnbaaa aache usanii. Hiyo milioni 350 ni matumizi madogo sanaaaaa . Aulize Wizara aliyofanya kazi ya Mambo ya nje Kiasi gani kimetuka kwenye fungu hiloooooooo. Hilo ni tatizo na serikali zima sio wizara

  Pia January makamba ajiulize inakawje wafanyaazi wa serikali wanalipwa mshahara mdogo lakini wanauwezo wa kunua magari.kujenga nyumba.!!!!!!

  Serikali haitaki kuwalipa mishahara mizuri wafanyakzi kukweka kulipa Pesnion. Wanawalipa overtime ambayo kwenye wizara na idara nyingi ni kubwa kuliko mshahara. Hayo yanafanyika kwenye serikali yoooooote

  Watanzana tunataka umeme hata wakilipwa bilioni kwa overtime kama wamefanya kazi hakuna shida shida kama hakuna kinachofanyika.

  Katika hali ya uchumi wetu hawa wabunge mshahara wa ni mkubwa. katika hali ua uchumi wetu Makamaba aonyeshe mfano wa kuomba wakatwe kodi. HIzo overtime kama anataka kumlipua kikwete asiguze teh teh teh teh . Mzimu wa Mgaya utaamka tena
   
Loading...