Idara ya ustawi wa jamii ni yatima? Haionekani kwa Wizara ya Kufikia

Profesa

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
905
624
Idara hii ni nyeti kuliko mtu yeyote anavyoweza kufikiri, ila imekuwa ikiiendelea kunyong'onyezwa kwa makusudi kabisa au kwa kutokujua (ujinga/makusudi?) ya viongozi wa serikali. Idara hii ndiyo yenye wataalamu wa kutatua migogoro ya ndoa, kusaidia watoto ambao hawana malezi maalum au yatima, yenye kusimamia haki za mtoto anapokuwa kwenye migogoro aidha ya kijamii au ya ki-mahakama, wenye kujenga maadili ya watoto, vijana na jamii yetu kwa ujumla; wenye kulea na kusaidia wazee, wenye kusimamia haki za watoto walio telekezwa. Kwa Ujumla ni Idara yenye kushu7ghulikia maswala ya kijamii hasa ya wanyonge.

Je kuna kiongozi anaeliona hili? Maaana kila wakati Idara hii hurushwa kutoka Wizara Moja kwenda nyingine, na sasa haionekani kabisa ndani ya Wizara ya Afya hata ukisikiliza mjadala wa Bunge na Budget ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Au je ni janja ya serikali kuhakiksiha wanyonge na watu walio katika maisha duni hawatetewi na hawapati huduma wanazostahili? Kwa kuwa miradi mingi iliyopaswa kusimamiwa na idara hii imeangukia kwa wafadhili, na wanaelekea kupungua kila siku.

Lini Serikali itatambua umuhimu wa Idara hii na kuiundia Wizara yake, na kuiondoa Idara ya Familia na Idara ya Watoto kule Maendeleo ya Jamii na kuiunganisha humu na kuw ana idara ya sera, na idara za utekelezaji mbalimbali.

Au ni makusudi ya kuhakikisha NGOs zao zinaendelea kushamiri? Maana Waheshimiwa Wengi wana NGOs zao nyingi tu zinazofanya kazi za Ustawi wa jamii.

Hata ukiingia kwenye website ya Wizara ya Afya, link ya Ustawi wa Jamii ipo lakini haiko active na haifanyi kazi. Kuna tatizo gani? Cheki: http://www.moh.go.tz/moh-dsw/
 
Ustawi wa jamii hakuna hela.. Hakuna mikataba ya uwizi... Kila mtu anataka wizara au idara yenye hela sio hizo za kushuhulika na watoto au ndoa za kazi gani
 
Back
Top Bottom