• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Idara ya uhamiaji na tatizo la ajira Tanzania

jamii01

jamii01

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Messages
1,885
Points
2,000
jamii01

jamii01

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2010
1,885 2,000
Watanzania wenzangu walamika hakuna ajira hata ile ya kuuza nguo kariakoo imechukuliwa na wageni wakijiita wawekaji au wafanyabiashara wakubwa na huku hata mtaji wa 10 Mill.hawana,na mara nyingi tumezoea kuwaita kwa majina ya mchina au msomali,muhindi n.k huku tukiendelea kuwachekelea kama ndugu zetu lakini ni adui zetu na wengine wakiwanyanyasa watanzania wenzetu kwenye Nchi yao na sisi kuwatetea kwa nguvu zetu zote na kuwaona watanzania wenzeu ni maadui.

Idara ya uhamiaji kuna mambo mengi sana yakupaswa kulaumiwa,naweza kusema kuwa kuna ajira rasmi zaidi ya 300,000 zimekamatwa na wageni huku watanzania wakisugua viatu kutafuta kazi,naweza kutoa mifano mbali mbali hapo sekta hizo zilizokamatwa na wageni,jaribu kutembelea katika hotel zetu za kawaida na zile za kitalii utakuta wanafanya kazi na wengine ni wapishi,supervisor n.k najiuliza ni kwamba hakuna watanzania wanweza kufanya kazi kama hizo?naweza kusema shida si Lugha kama baadhi ya waajiri wakitumia kama kigezo.kuna watanzania wenzangu wanaweza kuzungumza Kiingeleza vizuri tu..na watu hawa hufanya kazi bila kuwa na vibali,niliweza kubahatika kukutana na watu mbali mbali katika nchi toafuti waliokwisha kufanya kazi katika sehemu hizo wamekaa Tanzania kuanzia miaka miaka 2 hadi 13 hadi wanapochoka wanaamua kuondoka wenyewe.

Nilibahatika kukutana na raia wa kimarekani alikwenda Tanzania kutalii baada ya mda mwenye Hotel alimshawishi afanye kazi pale alimpe dollar 4000 pesa yake ya mfukoni kila kitu atampa sababu alikuwa anataka mfanyakazi wakigeni lakini yule bwana alikataa kwa sababu hakutaka kukaa Africa.ulikwisha fikiria mtanzania hapo anaweza kulipwa hata dollar 500 the some post?

kwenye makampuni ya utalii mambo ni yale yale,migoni ukitemebelea kwa sasa ndiyo hivyo utakutana wa wacongo,wanageria,,waghana, mataifa ya mengine wakifanya kazi bila kuwa na vibali na wala hofu yoyote na idara ya uhamiaji zipo na wakati mwingine ndiyo rafiki zao wakinywa pombe bar wote na afisa huyu huyu anajua huyu mtu ni raia wa nchi fulani na hana kibali cha kukaa hapa wala kufanya kazi.

Kwenye sekta za nyingine tunazoziita za uwekazaji napo ni janga jingine,wanadai wanakuja na administration yao lakini utakuta hata casher wao,markerting offer wao ,n.k jamani hakuna watanzania wanaoweza kufanya hata hilo?system nzima ya utawala ni ya wageni hakuna wanatanzania kweli wanaoweza kufanya kazi.hawa wote wanatafuna nyama na kuiacha Tanzania mifupa kisha kuondoka zao.


Uhamiaji na kutoa passport na uraia kwa njaa ya pesa ..niliweza kukutana na wageni wakiwa na passport za Tanzania katika nchi za nje anakwambia yeye si mtanzania lakini ana hold passport ya Tanzania nayeye anakwamba alipata kwa sababu alikuwa anahitaji kusafiri katika nchi fulani fulani,kwa passport ya nchi yake ni ngumu kupata VISA..ni wazi kuna baadhi ya nchi ukiwa na passport ya Tanzania ni free entry. mtu huyu hata ajui kuongea kiswahili ajui ametokea mtaa gani,unajiuliza kwa nini ndugu zetu hawa wa idara ya uhamiaji wanauza haki yetu kwa njaa ya pesa?kuna mwingine nilikutanaye ni raia ya Nepal anafanya kazi katika restaurant Hongkong aliingia Tanzania akaa arusha kwa miaka 2 kiasha akapata passport kisha akaondoka zake.

Kwenye kutoa uraia ndiyo usiseme hasa ndugu zetu wakihindi sijui huwa ni kigezo gani kinatumika kutoa uraia,ila kwa macho ya nyama naweza kusema siyo..hawa naweza kusema wanakuja kuficha njaa zao na umskini wao katika Tanzania,mbona hawakati miguu kwenda india mara kwa mara?

Wachina nao kariakoo usiseme yaani walikwisha fanya kama nchi yao,hawa si wawekezaji hata kidogo ni wamachinga waliokuja kuchukua ajira ya Mtanzania hata yule anayejitahidi kujikwamua na umaskini wanamfunika huku serikali yetu ikwachekelea na kuwakamata kwa mikono wasidondoke..ni wazi kuwa hawa ni magent wa viwanda vyao huko China.

Sekta ya miundombinu kwenye kutenegeneza barabara anaongzoza gari Mchina, driver mchina sasa Watanzania wafanye nini zaidi ya kukaa vijiweni na kupiga story?

Uhamiaji hawa hawa ukienda Mtanzania unaomba passaport unataka kusafiri wanavyokusumbua kama vile siyo haki yako hata kidogo,au wewe si mtanzania.wanakuuliza unaenda nje kufanya nini,nani anayekulipia gharama na mengineyo mengi yanayokela imradi du anataka umpe rushwa.
 
SHIEKA

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Messages
8,271
Points
2,000
SHIEKA

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2011
8,271 2,000
Kuwakubalia wageni kufanya watakalo kwa kuhonga baadhi ya watanzania waliokabidhiwa kazi ya kusimamia uhamiaji
kumefanya vijana wetu kukosa kazi, kunyanyaswa na kufanyiwa vitendo ambavyo huwezi kufifanya nchi yoyote hapa duniani ila Tanzania tu! Halafu wizara zipo na hazishtuki malalamiko yanapotolewa.Nchi hii kama imeoza na kulaaniwa vile!
 
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Messages
5,790
Points
1,250
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2011
5,790 1,250
Dah kweli m2wangu hapa niko pritoria kuna wa somari 2 wana tumia mkoba wa kibongo kinacho niudhi hawawezi kuongea kiswahili hata kidogo mpaka mi nashangaa wame pataje hizi parsport
 
pererge

pererge

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2012
Messages
570
Points
225
pererge

pererge

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2012
570 225
kweli kabisa bongo hali ni mbaya. wananchi ni kama wapangaji kwenye nyumba hawana haki, haki anayo baba mwenye myumba tu. akiamua kizina umeme au kufunga maji hakuna wa kumpinga. kwakweli hata mimi siwapendi wachina kurundikana hapa mjini, ongezeko lao linatisha. wanatuongezea tatizo la ajira na makazi pia. Waondokeee!
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,478
Points
2,000
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,478 2,000
Kwenye tatizo la ajira Tz uhamiaji wanahusika moja kwa moja najua foreignors wanaoruhusiwa kufanya kazi per company ni watano tena wawe wenye taaluma zao
sasa kuna makampuni wanafika zaidi ya kumi which means izo post ni za watz wageni wameamua kuzihodhi kwa kuwahonga jamaa wa uhamiaji
 
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Messages
4,694
Points
2,000
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2012
4,694 2,000
Halafu kwa haya yote kwanini Mzanzibari asichoke kutanga na nyika? Hata mimi ningekuwa mzenji ningejitoa tu kwenye huu uozo wa hili li dubwasha linaloitwa Tanzania.
 
Anthony Lawrence

Anthony Lawrence

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2011
Messages
1,546
Points
1,500
Anthony Lawrence

Anthony Lawrence

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2011
1,546 1,500
Lawama hizi zisiishie kwa uhamiaji tu, hata Idara ya Kazi pia wana husika. Uhamiaji huwa wanatoa vibali vya wageni baada ya ya Idara ya Kazi kumwidhinisha mwombaji, kuwa ana stahili kupewa kibali.
 

Forum statistics

Threads 1,405,651
Members 532,074
Posts 34,492,007
Top