Idara ya uhamiaji na mabadiliko ya baraza la mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idara ya uhamiaji na mabadiliko ya baraza la mawaziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Juliani Mumbi, May 20, 2012.

 1. J

  Juliani Mumbi Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mabadiliko ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni yametoa ahueni kwa taasi za wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na hasa Idara ya Uhamiaji na Zimamoto. Aliyekuwa Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha alisababisha matabaka ndani ya Idara hiyo hasa kwa kutoa upendeleo kwa maswahiba wake na hasa baadhi ya Wazanzibari. Tatizo kubwa lililokuwapo ni waziri huyo kufanyia kazi taarifa zisizo rasmi alizokuwa akipelekewa na Afisa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam ambazo ni za fitina majungu kwa ajili ya kutaka nafasi jambo ambalo alifanikiwa na sasa amekalia nafasi za juu baada ya kuwatoa viongozi aliowafitini. Bila woga na tafakuli Nahodha akampachika mpika majungu huyo ambaye alishindwa kuiongoza Idara ya Uhamiaji Zanzibar akatolewa na kupangiwa mkoa wa Kilimanjaro ambao nao ulimshinda, akahamishiwa Chuoni, huko alishindwa vibaya kwakuwa hana elimu bali anatumia usanii. Kabla ya kuingia Uhamiaji Afisa huyo alikuwa Usalama ambao nao walimtema kwakuwa na majungu na uchonganishi, dharau na kujikomba. Afisa huyu zama za Nahodha alikuwa Mungu mtu hakumtii yeyote bali Nahodha na baadhi ya watendaji wa wizara.Tatizo jingine ni Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye ameonekana dhahiri kuchukua Madaraka ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kwa kutoa uamuzi wa kibabe na kusababisha vurugu kubwa ndani ya Wizara hiyo. Naibu Katibu huyo alikuwa akimruka mkuu wake na kwenda mojakwamoja kwa Nahodha amabaye bila kupata ukweli aliamua kutoa uamuzi usiofaa na kuwaumiza watendaji waliochini. Naibu Katibu huyo naye alitolewa Usalama baada ya kuonekana kashindwa kazi na zaidi anatumia haiba yake kuwahadaa viongozi wa juu yake. Baadhi ya uamuzi wake ulisababisha mkuu wa utawala kuomba kuhama Wizara,alimtoa Mkuu wa Zimamoto, aliwatoa wakuu watatu wa Uhamiaji na kibaya zaidi amekuwa hata akiandika barua za mojakwamoja kwa watendaji wa chini bila ya kufuata utaratibu.Naibu katibu huyo anaongoza kwa dharau,kejeli, vitisho, ubabe na matusi kwa watendaji wa chini yake. Anapowaita watumishi muda wote amekuwa akitumia lugha isiyofaa, kejeli na matusi.Katibu huyo kama alivyokuwa Nahodha amekuwa akiifuatafuta sana Idara ya Uhamiaji, lakini yeye ni kwa maslahi zaidi. Akitumia ubabe amefanikiwa kupachika kampuni zake za usafi na Ulizi wa Makao Makuu ya Uhamiaji, kampuni zote mbili hazina sifa wala hadhi ya kazi kwakukosa. Sasa hivi yuko katika vita kubwa ya kuhakikisha kampuni aliyo na maslahi nayo inapata tenda ya kununua mitambo mbalimbali ya kazi za uhamiaji. Kampuni ya mwanzo iliyokuwa inafanya kazi hiyo imeonekana kutomjali hivyo amepika fitina kali imepigwa chini.Watendaji wa Idara ya Uhamiaji kipindi chote cha Nahodha na Naibu Katibu mkuu wamekuwa wanyonge kwa kuwa hawakuwa na pa kukimbilia bali kusubili kudra za Mungu.Tunampongeza sana Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuona mambo yalivyokuwa hayaendi katika Wizara hii kubwa na nyeti na kufanya mabadiliko makubwa.Kama ulivyoahidi kuwaondoa viongozi wasiofaa tunakuomba unapofanya mabadiliko muondoe Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani.Mwisho tunakuomba Mh. Nchimbi pia uyafanyie kazi matatizo haya maana Wizara ilipoteza muelekeo kwa kushindwa kufuata utawala wa sheria bali ubabe.AlamsikiJulian M. Mwakanosya, May, 2012.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Ngoja wanaojua kusuta waje.
   
 3. K

  Kama kawaii New Member

  #3
  May 26, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Julian wewe ni mnafiki ulkuwa wapi??? Mbona Leo???? Umetumwa au??? Walokutuma wamechemka:A S-baby::A S cry::A S 12::ranger::A S 114: au wewe ndo haohao hata sisi pia tunao ndugu huko kwenu ! Ache majungu watt wafanye kazi
   
Loading...