singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma, Naibu Kamishina Maurice Kitinusa, akizungumzia zoezi la kukamata wahamiaji waishio nchini bila vibali. (Picha na Emmanuel Senny).
Na Emmanuel Senny, Kigoma
Idara ya Uhamiaji mkoani Kigoma imefanikiwa kukamata wahamiaji 1088 wanaoishi nchini bila vibali mara baada ya kuanza zoezi hilo katika wilaya zote mkoani humo mwanzoni kwa mwaka jana.
Akizungumza na blog hii hapo jana, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kigoma Naibu Kamishina, Maurice Kitinusa, alisema kuwa takwimu hiyo ni ilianza mwezi Aprili mwaka jana mpaka mwezi Januari mwaka huu na kufanikiwa kukamata wahamiaji 1088 kutoka maeneo yote ya mkoa wa Kigoma.
Alisema kuwa, baada ya kuwakamata wahamiaji hao wapo waliorudishwa nchini kwao na wengine kupelekwa mahakamni huku wengine wakipunguziwa vibari vyao vya kuishi nchini baada ya kukiuka sheria.l
Aidha Kitinusa alisema kuwa, wahamiaji 453 walipelekwa mahakamani ili kuchukuliwa hatua za kisheria ambapo katika hao 15 walihalarishwa ukazi wao baada ya kupewa vibari vya muda mfupi (CTA) na wahamiaji 750 walifukuzwa nchini baada ya kukutwa na makosa.
“Katika idadi hiyo watu 117 tuliwakabidhi kwa idara ya wakimbizi baada ya kugundua kuwa ni wakimbizi waliokuwa wakiishi vijijini, pia watu 206 tuliwaachia huru baada ya kuthibitisha uhalali wao wa kuwepo nchini baada ya kuleta vitambulisho ambavyo wakati wanakamatwa hawakuwa navyo,” alisema Kitinusa.
Kitinusa aliongeza kuwa, kuna watu 104 ambao walifupishiwa vibali vyao vya kuwepo nchini baada ya kuonekana hawana sababu za msingi zilizowaleta nchini kama walikuwa na vibali vya miezi mitatu walipunguziwa mpaka wiki moja wawe wameondoka.
“Pia kuna watuhumiwa 163 ambao uraia wao unautata mana wao wanasema ni raia watanzania lakini viashiria vingi vinaonyesha sio raia wa watanzania kwahiyo hawa uchunguzi unaendelea kulingana na taarifa walizozitoa,” alisema Kitinusa.
Pamoja na hayo Kitinusa aliwataka watanzania ambao wanamiliki nyumba za kulala wageni kufuata sheria inayowataka kuwa orodhesha wageni wote wanaofika katika nyumba zao ili kufahamu kama wamepata wageni ambao sio raia.
“Mpaka sasa tuna kesi tatu mahakamani za wamiliki wa nyumba za wageni kwa makosa ya kuwalaza wahamiaji wasio na vibali, na ifahamike kuwa kuwalaza watu bila kuwaorodhesha ni makosa awe mtanzania au raia kutoka nchi nyingeine na sisi tunawapeleka mahakamani wanaokutwa na makosa hayo pia wale ambao wanawapokea wageni na kukaa nao bila kutoa taarifa katika ofisi za uhamiaji sambamba na wanaowatumikisha mashambani,” alisema Kitinusa.